TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Mwamba na Jemedari ameondoka.! Pumzika Mzee Pumzika Baba.

Kuna maumivu nayapata ndani kwa ndani, tokea nimepokea taarifa hizi jana saa sita usiku kwenye Mitandao ya Kijamii.! Naumia sijui kwanini lakini ..! [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Maisha ni fumbo.

Tumia muda wako kufanya mazuri kwani siku moja utapotea kama nukta moja ya mchanga baharini na kitakachobaki ni historia yako iwe ya mabaya au mazuri.
Hata kama ulimchukia au kumpenda ila kifo ni kifo. upendo na chuki vyote havina faida sasa hivi.
Binadamu wenye moyo watanielewa.

Sifurahii wala Sisikitiki.

Have a good sleep mr. president.

Umeeleweka vyema Kamanda.!
 
Tunataka chanjo zianze kuja. Hatutaki kuendelea kufa

Mataga walikaza mafuvu Yao sasa wataanza kuelewa.
 
Mwamba na Jemedari ameondoka.! Pumzika Mzee Pumzika Baba.

Kuna maumivu nayapata ndani kwa ndani, tokea nimepokea taarifa hizi jana saa sita usiku kwenye Mitandao ya Kijamii.! Naumia sijui kwanini lakini ..! [emoji24][emoji24][emoji24]
Tenda mema ishi na watu vizuri mche Mungu acha kulilia marehemu ililie nafsi yako na wanaokuzunguka kwamba saa ikifika watakutwa katika mazingira gani
 
Nadhani wote MAJALIWA, SAMIA,BASHE,CHALAMILA wanapaswa kuachia ngazi mara moja.
Sioni tatizo kwa mama Samia. Nadhani hapo juu huyu mama ana hekima na diplomacy itoshayo kuiongoza Tanzania. Hawa wengine nitoe fursa kwa muda... Kesho nisikose cha kusema au nisihukumiwe kwa "unafiki"!!!
 
Si ya makumbusho hiyo? Something like that! Kwy qns why atoke JMKHI aende mzena sijawai hata kuwaza? Why not flying him to SA au hata Kenya apo baada ya kupata nafuu kwa uangalizi zaidi! Anyway yote tumuachie Mungu

Umeambiwa alitoka JMKHI baada ya kuwa na ahueni ila hali ilibadilika ghafla tar 14 March ndio kupelekwa Mzena vhini ya uangalizi wa wauguzi na madaktari wa JMKHI.
 
Maisha ya mwanadamu ni mafupi nayo yamejaa shida na majaribu mengi - cha msingi na kikubwa zaidi ni kuishi hapa duniani kwa kumpendeza Mungu - Tenda HAKI ili umesabiwe HAKI hiyo hiyo ili parapanda litakapolia na jina lako kusomwa kwamba ni lazima uiache dunia basi uwe tayari.

Sisi tunasonga mbele - Yaani maisha ni lazima yaendelee - huu ndiyo mpango (utaratibu) wa Mungu wetu Mwenyezi alioufanya tangu uumbaji.
 
Haya Chadema furahieni sasa mliyoyaomba yamejibiwa
Chadema hawana mamlaka juu ya kifo.walionena na kuandika hawakuandika kama chadema. Walitoa maoni yao na kuhabarisha umma juu ya yanayoendelea hata hivyo kutokana na chuki na ushabiki wa kijinga watu mkaanza kuishambulia chadema. Huu no ujinga uliopitiliza !!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom