Rais wa Tanzania kufanya ziara ndani ya nchi ni ghali kuliko nje

Mleta mada usije tushauri tu kuwa ili Kupunguza gharama Rais ahamie huko huko nje ya nchi.
 
Tanzania tunakwenda vizuri sana,
 
economy class
Rais anatumia Economy?? Viongozi wateule watumie Economy? Nahisi unatania.

Pili, Msafara ukifika huko nje unafirikiri hawatumii magari?

Tatu, hujazungumzia perdiem zinalipwa kwa Dola na bado hotel za nyota 5 wa viongozi na wengineo.

Nne, umesema Land cruiser V8 lililotumika kama haya yetu linatumia Lita 45.5 kwa umbali wa km 100 (45.5L/100Km ) huu ni uongo wa wazi kwamba Lita 1 inatembea 2.2KM, madereva wako humu watatusaidia Lita 1 inaenda kama 5KM au zaidi.

Rudia kupitia hizi gharama zako upya labda kama ni PAMBIO LA KUSIFU.
 
Safari za ndani hutumia AirTanzania, hizo v8 hutumika ndani ya mikoa husika, lakini sio kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine labda kama hiyo mikoa iwe karibu, mfano Dsm - Pwani au Kilimanjaro - Arusha, lakini sio Mwanza - Dar thats too far.
jiwe alikuwa na pacemaker na alikuwa anapiga ruti hadi Zambia, Kenya, Malawi, Rwanda, Zimbabwe, Msumbiji, bado sasa juu kuna helcopter 2. Ukija hapa ndani msafara wa jiwe ulikuwa magari 113 na helcopter 3 na pesa taslimu za kugawia wamama wanyonge barabarani. JIWE HILO. Bora SIR GOD alituona.
 
Jiwe
alikuwa anatembd yeye, makamu, waziri mkuu, speaker, jaji mkuu, mkuu wa majeshi, igp, mkuu zimamoto, mkurugenzi usalama, katibu mkuu kiongozi., wabunge wote wa mkoa husika, mawaziri kama 12, walinzi 1000,.,.. YULE MTU KAUMIZA MNO KODI ZETU.
 
Hatari tupu aise,
 
Asante Sana kwa hii makala Jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…