Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

The Rise and Fall of Malinzi Jamal. Kuna mdau mmoja alinitukana humu kisa Malinzi nilipomuambia huyo ni fisadi namtafuta kwa udi na uvumba.

Nadhani utakuwa unamsema mwenye Malinzi wake Frank Wanjiru Mkuu au? Leo sijui atakuja na ' mbeleko ' gani tena humu ya kumbeba na kumtetea Kipenzi chake Rais wa TFF Jamal E. Malinzi.
 
The Rise and Fall of Malinzi Jamal. Kuna mdau mmoja alinitukana humu kisa Malinzi nilipomuambia huyo ni fisadi namtafuta kwa udi na uvumba.
Ilibidi akutukane, una ushahidi gani kuwa ni fisadi? Mbona kuitwa PCCB ni kawaida kwa watu wenye majukumu, wana maadui wengi kiasi lazima wapeleke umbea pccb. Sioni ajabu.
 
Ambazo hata hivyo zimezaa matunda. Na ' Wajuvi ' wa mambo hapa ndipo tunasema " Mission Accomplished ".
Time target! Hongereni japo ni mapema mno maana yupo mdudu anayeitwa 'kuahirisha' anaweza kuingia kwenye embe hata kama limeiva
 
unamjua ally mayai au unaongea tu huyo ni officer wa wizara na watu tuliosoma vyuo vya mjini tunamjua ndio alikuwa rais wa chuo na sasa hv ana masters
Kumbe na wewe umesoma CBE, hicho chuo siwezi kumpeleka mwanangu asome.Chuo kumbakumba sana hicho.Hata divisheni ziro anadailiwa CBE!
 
Ngoja tusubiri tuone kwani wakati siku zote huwa unatoa majibu sahihi zaidi kuliko hisia na isitoshe nakubaliana kabisa na wewe michezo michafu kwenye chaguzi ni jambo la kawaida sana na ndio maana mwanzo nimekwambia kwamba huu inawezekana ikawa ni mchezo na unapangwa kimkakati lakini kwa bahati mbaya mkakati wenyewe unaonekana wazi kabisa lengo lake ni kumzuia Malinzi asiwe rais, na mpaka unaona mbinu za namna hii na za waziwazi zikitumika maana yake Malinzi kawashinda tayari sanasana wanajazia ushindi wake tu. Kuhusu system siamini kama system inaweza kufanya mambo yake kwa akili ndogo kiasi hiki, hapana
 
Unaushahidi wowote wa kukanusha hili au unaleta utetezi usikuwa na tija? Mpaka sasa ni tetesi na habari hizo ziko kila kona basi ajitokeze akanushe sio kukutuma wewe bila data
Anakurupuka tuu huyu! Hizi habar tangu jana usiku zipo hewan, na Takukuru wamethibitisha kumkamata kwa uchunguz wa mambo fulan
 


Rais wa TFF na mwenzake wakamatwa na polisi

mkuu wa kitengo cha habari wa TAKUKURU amesibitisha kukamatwa kwao
 
Hizi ni figisu tu hakuna kitu hapo
Definitely, wanataka asigombee. Lakini FIFA ina taratibu zake! Let us wait and see. Si mara ya kwanza kumuita huko, sema hili ni la uchaguzi
 
Habari njema kwa wana msimbazi.....

Habari mbaya kwa wana jangwani......


ANGUKO LA YANGA LINAKWENDA SAMBAMBA NA VIBARAKA WAO PALE TIFUA TIFUA.....

KILA MTU ATAVUNA KILE ALICHOKIPANDA....


CELEBRATIONS TIME.....

Ally Mayai alikuwa kepteni wa timu gani?
 
Definitely, wanataka asigombee. Lakini FIFA ina taratibu zake! Let us wait and see. Si mara ya kwanza kumuita huko, sema hili ni la uchaguzi
Hapo ndio patakuwa pagum,yatatokea kama yaliyotokea ya Ndolanga na usishangae tukafyata mkia
 
unamjua ally mayai au unaongea tu huyo ni officer wa wizara na watu tuliosoma vyuo vya mjini tunamjua ndio alikuwa rais wa chuo na sasa hv ana masters

Na hapa ndipo ambapo huwa ' nagombana ' na Watanzania wanaojiita ' Wasomi ' kila mara. Jamani kuongoza ' Taasisi ' fulani ni zaidi ya kuwa na hizi sijui Degree, Masters na PhD na hebu tuacheni huu ' umbwigira / ushamba ' wa kutaka kutumia ' Usomi ' wenu wa ' Kukariri ' kama ndiyo Fimbo ya kuwapigia au kuwadharau wengine. Someni kwa faida yenu na siyo ' kuwatambia ' wengine. Benki Kuu ya Tanzania kuna ' PhD ' 17 lakini kwa miaka 17 kama siyo 18 hizo ' Hopeless ' PhD's zimeshindwa kujua kuwa nchi yetu inaibiwa na inapoteza Hela nyingi sana hadi sasa Wananchi wetu bado wanataabika tu na ' umasikini '.

Hatumpeleki Ally Mayai Tembele pale TFF kwakuwa ana hiyo Masters Degree yake bali tunampeleka pale tukijua kuwa kwakuwa amecheza mpira tena wa Kiwango kikubwa sana basi kwa kushirikiana na Kaka yake Mzee Mtemi Ramadhan ambaye nae pia ana rekodi yake nzuri tu ya ' Kutukuka ' katika mpira wanaweza wakatusogeza Kimaendeleo kutoka hapa tulipo sasa.

Naheshimu mno hizo Elimu zenu kubwa ambazo kutwa ' mnajitapa ' nazo humu ila ningependa tu badala ya kuzitumia kwa ' kujishebedua ' nazo basi zitumieni kuisadia nchi hasa katika kupambana na changamoto kubwa na nyingi zinazowakabili Wananchi. Usomi mzuri ni ule ambo uko ' pragmatic ' na siyo tu huu wa ' Kujisifia ' Vijiweni na humu Mitandaoni.

The so called ' Wasomi ' wa Tanzania ' badilikeni '.
 
Time target! Hongereni japo ni mapema mno maana yupo mdudu anayeitwa 'kuahirisha' anaweza kuingia kwenye embe hata kama limeiva

Nikuakikishie tu tena Mkuu kuwa hapo kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi " Mission Accomplished ". Hapana chezea ' System '.
 
Kumbe na wewe umesoma CBE, hicho chuo siwezi kumpeleka mwanangu asome.Chuo kumbakumba sana hicho.Hata divisheni ziro anadailiwa CBE!

Naona ' Wasomi ' mnapeana ' Shombo ' sasa. Ngoja sisi ' Mangumbaru / Tusiosoma ' tukae pembeni tuwaangalieni tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…