PreGE2025 Rais wa TLS Adv Mwabukusi amkaanga Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi

PreGE2025 Rais wa TLS Adv Mwabukusi amkaanga Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sasa linganisha hayo malengo na anachokifanya Mwabukusi!!
Ndiyo hivyo sasa anamtaka Mutungi kufuata sheria za nchi na siyo kuendekeza uchawa uchwara katika utendaji wake wa kazi!
 
Akitolea mfano kutoka NCCR Mageuzi alizungumzia jinsi Ofisi ya Msajili inavyohusika kuvuruga Vyama vya kweli vya upinzani, sasa tunashuhudia kinachoendelea CHADEMA, ambapo amesema;

"Shetani hawezi kumfukuza Pepo, hakuna Ufalme unaojifitini. Msajili anajua kwanini Vyama vipo."

"Nimekuuliza, kuna Vyama havijawahi kufanya Mikutano Mikuu. Kuna Vyama havijawahi kufanya Mkutano Mkuu hata siku moja lakini bado vipo na vinatembea. Kuna Vyama viongozi wake wamemaliza muda wao. Kuna Chama kina Katibu tu, hakina Mwenyekiti; kingine kina Mwenyekiti tu, hakina Katibu. Umeshawahi kumsikia Msajili wa Vyama akienda huko?"

"Utamkuta akizunguka NCCR wakitaka kufufuka, anaipiga nyundo. Anazunguka CHADEMA kuwachochea, lakini uzuri CHADEMA wamejiimarisha vizuri, na ndiyo maana mara nyingi wameonekana wakipangua."

"Wewe unaweza kuona Msajili wa Vyama ambavyo kuna Wabunge waliotangazwa na Mahakama kwamba si Wabunge, wakaendelea kuwepo Bungeni, halafu ukasema hii ni Ofisi ya Msajili wa Vyama? Anajiita mlezi wa Vyama, lakini yule si mlezi wa Vyama ni Ofisi ya muuwaji wa Vyama vya ukweli vya upinzani."

Kula chuma hicho 🙌🙌
 
Kajifunze kutofautisha "r" na "l". Mtu akiandika jadiri badala ya jadili ananikosesha hata hamu ya ku argue naye. Namuona ni ngumbaro
Wasomi wa masomo ya lugha mnasumbuaga sana. Kuna na mwingine aliwahi kunitambia kuhusu shule na elimu yake ya lugha kama wewe, anyway, Kiswahili nilipataga D so sio kosa langu. Masomo yasio na formula yalikua yakinisumbua sana O level so nisamehe na nivumilie. Tuendelee mbele, JADILI ujumbe sio MJUMBE. Watu makini wapo hivo
 
Back
Top Bottom