Rais wa Ukraine aliamini kabisa kuwa NATO wangemsaidia endapo angevamiwa na Urusi

Rais wa Ukraine aliamini kabisa kuwa NATO wangemsaidia endapo angevamiwa na Urusi

Hivi Putin baada ya kumalizana na Ukraine,hawezi kuwapiga beat kwamba nifungulieni vikwazo vyote au nitawashambulia kwa nyuklia!?
Nalog off
Kaongea leo kuwa hizo sanctions zitageuka kuwa vita kweli. Huko tunakoelekea ndo atakachofanya ila si kuwablackmail kwa nuclear. Maana nuclear hata NATO wanazo.
 
Harafu hilo Jina la Rais wa Ukraine muwe mnalisoma sio mnalipita kisa tu mmeshalikariri
 
Huyu mchekeshaji mjinga.. hajui kuwa hizi mambo ni serious. Sio ujinga anaofikiri
😂😂 ila ni msanii wa kutunukiwa holywood... ushamcheck akihutubia ndani ya handaki hajanyoa ndevu nk anahutubia kwa sauti chungu? Sa vita hata havijaingia mjini niaje huyu wanamwita shujaa tayari kajificha shimoni niaje hapo
 
Kiongozi mwingine mwandamizi wa Jeshi la Urusi ,Major General,auwawa Ukraine
Screenshot_20220311-154403.png


Screenshot_20220311-154437.png
 
Rais wa Ukraine aliamini kabisa kuwa NATO wangemsaidia endapo angevamiwa na URUSI. Mabeberu walimvimbisha kichwa, hata hakuweza kabisa kuheshimu makucha marefu ya URUSI.

Malengo ya MAREKANI na NATO kwa ujumla ilikuwa ni kuitumia UKRAINE katika kujaribu kuidhoofisha URUSI. Ili kufanikisha lengo la NATO ilibidi kumlaghai UKRAINE aamini kuwa atajiunga na NATO kwa urahisi hivyo kudhani kuwa URUSI itaogopa kuvamia Ukraine iliyo ndani ya NATO.

Lengo mahususi la NATO ilikuwa ni kuandaa mazingira yatakayoilazimisha URUSI kuvamia UKRAINE. Kwa mazingira waliyoandaa ya kuihakikishia kuwa UKRAINE hatazuiwa kuwa mwanachama wa NATO, nchi za magharibi zilikuwa na uhakika asilimia 100 kuwa kwa kuuvuka MSTARI MWEKUNDU wa URUSI lazima Urusi itaivamia Ukraine, na haswa hicho ndicho walichokuwa wanakitafuta. Walikuwa wanatafuta Urusi ivamie Uraine ili wapate uhalali wa KUIWEKEA VIKWAZO VIKUBWA SANA vya kiuchumi.

Lengo ni kuidhoofisha Urusi kiuchumi ili hatimaye ishindwe kuendelea kujiimarisha kijeshi. Jeshi imara linahitaji uchumi imara.
Amini usiamini, siku Urusi amevamia UKRAINE, Marekani na NATO kwa ujumla walishangilia sana, kwa kuwa tayari URUSI alilazimika kuingia kwenye mtego aliokuwa anaujua wazi lakini akalazimika kuchagua BAYA MOJA KATI YA MABAYA MAWILI!!

Baya alilochagua ambalo angalau ni nafuu kwake kwa kutunza heshima yake ni kuvamia, huku akijua madhara yake kiuchumi. Baya aliloamua kulikataa ambayo ni baya zaidi kwake ni kuruhusu UKRAINE kujiunga na NATO hivyo kukaribisha adui mkubwa alimbikize silaha za maangamizi mlangono kwake!! Hilo aliona litamdhoofisha zaidi na kumwondolea heshima yote. Sasa yote haya inaelekea Rais wa Ukraine hakuwa anayajua!

Yeye alidhani nchi za magharibi zinampenda sana na zitamlinda kwenye vita ambayo imeandaliwa mazingira ya kutokuepukika!!
Sasa alipotumbukia kwenye vita, na Mrusi akatumia njia ya kuchoma sindano na kuiacha ndani ili maumivu yanyong'onyee ( kuzingira miji yote muhimu, ili kuzuia misaada ya kijeshi kuwafikia wanajeshi wake waliozingirwa), sasa Rais huyo msanii akaomba NATO waweke "NO FLY ZONE" (kuzuia ndege za Urusi za kivita zisiruke), na NATO wakamruka "kimanga"!!

Kwa sababu NATO wanajua utaizuiaje ndege ya URUSI kuruka kwa mfano! Inabidi uishambulie!! Hii maana yake uingie vitani na URUSI, kitu ambacho hakikuwa lengo tangu mwanzo!! Kuingia vitani na URUSI maana yake ni vita kuu ya tatu ya dunia!!! hapo hakuna mshindi!! Urusi ndio inaongoza duniani kwa kuwa na silaha nyingi za Nyuklia!! Hivi Rais wa UKRAINE alidhani kuwa NATO watakuwa tayari kuingia vitani na Uruisi?

Aozee tu kwenye choo cha kike, NATO hawana ubavu huo!!!!
Mwenyewe ndiyo alikuambia anavyofikria?
 
Mkuu mbona ni rahisi sana kufahamu ukweli, technology haidanganyi .Chukua Hila Jina search utapata details Sasa hivi huwezi danganya[emoji848]
Kumbuka taarifa ni za upande mmoja za Russia no network.

So its just a propaganda

Halafu kama una akili ushawahi kuona wapi Major Gen akaenda uwanjwa wa vita.

Mnaoangalia Movies mnatusumbua sana
 
Kumbuka taarifa ni za upande mmoja za Russia no network.

So its just a propaganda

Halafu kama una akili ushawahi kuona wapi Major Gen akaenda uwanjwa wa vita.

Mnaoangalia Movies mnatusumbua sana
Pro Putin BBC wameConfirm!
Screenshot_20220311-211533.png
 
Sisi wote humu ni wapumbavu sana, hivi tunawezaje kuwaza kuwa siku zote hizi ukraine yupo peke?...kuna wanajeshi wa NATO kibao wapo ukraine hapo
 
Back
Top Bottom