Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro na mkewe wakamatwa na vikosi vya Marekani

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro na mkewe wakamatwa na vikosi vya Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa Marekani imefanya mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Venezuela na kufanikiwa kumkamata Rais wa nchi hiyo, Nicolás Maduro, pamoja na mke wake.

Kupitia taarifa aliyotoa kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema operesheni hiyo ilifanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Marekani, huku akieleza kuwa maelezo zaidi yatatolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliopangwa kufanyika saa 11:00 asubuhi kwa saa za Marekani Mashariki, katika makazi yake ya Mar-a-Lago, Florida.

Hata hivyo, Rais Trump hakutoa maelezo ya kina kuhusu jinsi Maduro alivyokamatwa wala amepelekwa wapi, wakati serikali ya Venezuela bado haijathibitisha rasmi taarifa hizo.
View attachment 3524572
==========​
WASHINGTON, Jan 3 (Reuters) - The U.S. has struck Venezuela and captured its President Nicolas Maduro, who has been taken out of the country, President Donald Trump said on Saturday.

The U.S. has not made such a direct intervention in Latin America since the invasion of Panama in 1989 to depose military leader Manuel Noriega.

"The United States of America has successfully carried out a large scale strike against Venezuela and its leader, President Nicolas Maduro, who has been, along with his wife, captured and flown out of the country," Trump said in a Truth Social post.

There was no immediate confirmation from the Venezuelan government.
The U.S. has accused Maduro of running a "narco-state" and rigging an election. The Venezuelan leader, who succeeded Hugo Chavez to take power in 2013, has said Washington wants to take control of its oil reserves, the largest in the world.

Source: Reuters
Safi sana...
 
Safi sana...
😂😂

Itikadi kali wamenuna kinomaaaa
20260103_143014.jpg
 
Russia hajawahi msaidia mshirika wake hata mmoja mpaka mwisho.
Sio Syria, Armenia, Iran na sasa Venezuela.

Russia huwa anajaribu kidogo baadae anakutelekeza. Ingawa huu uvamizi wa Marekani sikubaliani nao kabisa sasa kesho na China akiamua si anavamia Taiwan au nchi yoyote.

Russia anajiamulia anavamia, Marekani nayo imevamia. China ikianza nayo si dunia itarudi kulekule kwa unanijua mimi ni nani.
Dunia ya wenye nguvu hii..

Hii lazima ni "inside job"....ina maana Maduro hana kikosi cha ulinzi cha Rais au kauzwa..?
 
Russia hajawahi msaidia mshirika wake hata mmoja mpaka mwisho.
Sio Syria, Armenia, Iran na sasa Venezuela.

Russia huwa anajaribu kidogo baadae anakutelekeza. Ingawa huu uvamizi wa Marekani sikubaliani nao kabisa sasa kesho na China akiamua si anavamia Taiwan au nchi yoyote.

Russia anajiamulia anavamia, Marekani nayo imevamia. China ikianza nayo si dunia itarudi kulekule kwa unanijua mimi ni nani.
Na china aivamie Taiwan
 
Maduro ni Fala siku zote hizo alikua hajui Kama anawindwa?

wote huwa hivyo gadafi south afrika walimtumia airforce kumchukua bado akagoma akifikiri ni michezo, sadamu husein mpaka alipewa masaa 48 kuondoka na watoto wake lkn bado alifikiri utani mwishowe wakamyonga kwa kamba live on tv, mjanja alikuwa assad tu alipoona mambo si mambo kachukuwa mke wake huyo akasepa, nafikiri power huwalevya labda, ngoja tusubiri kwetu itakavyo play out …
 
Back
Top Bottom