Rais wangu Magufuli, na mwezi huu wa nne utapokea mshahara kama watumishi wengine?

Rais wangu Magufuli, na mwezi huu wa nne utapokea mshahara kama watumishi wengine?

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Rais wangu salamu kwako.

Rais wangu, kusema kweli umeniangusha sana na umezidi kuondoa imani yangu kwako. Swali ninalokuuliza: Je, na mwezi huu wa nne utapokea mshahara kama watumishi wengine?

Nimeuliza swali hilo kwakuwa bila ya kuhadaa wala kubwabwaja umenifanya mimi pamoja na Watanzania wengi kukumbwa na majonzi kwa tunayoyaona na kuyashuhudia. Nalia kwa huzuni kubwa na nina mashaka makuu na kesho yangu pamoja na ya wenzangu.

Nakumbuka siku unaondoka Dar kwenda mkoani ukiwa Dodoma ulituambia tusitishane, tuchape kazi, tena ukasema kaugonjwa haka wala siyo tunavyokachukulia. Ni mwepesi kuliko malaria na UKIMWI. Baada ya kauli yako hiyo unajua ni nini kilitokea? Wasaidizi wako walianza kuyaishi yale uliyosema, hawakujiandaa kuchukua hatua. Wakatuzodoa kuwa Corona si chochote wala lolote. Sasa tunalia!

Pengine ungekuwa na kauli tofauti na ile hali ingekuwa tofauti Rais wangu. Pengine ungechukua tahadhari za kimamlaka kama mkuu wa nchi hali ingekuwa tofauti Rais wangu. Lakini ulipuuzia na kutoa kejeli zilizovuka mpaka juu ya ugonjwa huu. Sasa tunalia watu wako.

Ninalia nikishuhudia misafara ya ambulance kama daladala ndani ya jiji la Dar. Ninalia nikiona leo wenzetu wa mikoani wanatukimbia. Wanatukimbia kwa sababu yako Rais wangu. Wanatukimbia kwakuwa jemedari ulifanya mzaha uliopindukia ukauacha ugonjwa ukolee. Ona leo tumebaki wakiwa tukilia na kuomboleza, kukata tamaa na kumuachia Mungu!

Lakini Rais wangu, wewe uliondoka Dar mapema sana , nachelea kusema uliijua hali halisi. Mbona hukutuambia ukweli? Mbona hukutuweka huru? Umeondoka umetuacha na sasa tunatengwa na ndugu zetu na kuteseka kwa ugonjwa. Ukirudi utatueleza nini hasa? Tutakuamini tena kwa lipi zaidi?

Ninalia baada ya kushuhudia nilichokiona Mloganzila, hospitali imejaa na sasa tunatafuta nyingine! Sijui nayo itajaa? Ninalia maana siijui kesho yangu mimi binafsi hasa ninaposhuhudia watu wakitolewa ndani ya nyumba zao hoi kwa Corona. Kilio changu kinakuwa kizito kwakuwa uzembe uliofanya mwanzoni umeendelea kuufanya hata juzi.

Eti hufungi mipaka kwakuwa unategemewa na nchi zingine! Watu wako waliokupa ajira wana thamani kuliko kitu chochote kile. Chonde chonde, ndiyo waliokufanya sasa unaongea ukiwa na mamlaka. Umeshindwa kutumia mamlaka kutoa amri zitakazookoa walau kwa kiasi fulani watu wako.

Swali langu kwako, mwezi huu utapokea mshahara kama watumishi wengine?
 
Wageni wametuletea Corona, ni wakati wetu sasa kupambana na hali zetu. Hakuna namna.
 
Hili ni shairi hadthi ngonjera au? Kama kulia wee lia tu usisahau kufanya kazi raisi hawezi kugawana mshahara wake na wewe! Corona ipo nawa mikono kwa sabuni na maji yanayo tiririka usisaha kuvaa barakoa popote uendapo.
 
Hapa kuna makundi mawili, wale waliokuja Duniani kulinda Dunia na wale waliokuja Duniani kutalii.
Waliokuja kutalii hawana wasi wasi maana kwao, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.. Wale walinzi wamejawa na hofu kuu iwapo 'wataamriwa kuondoka' Duniani itakuwajee?
Tusitishane!
Kwa maana maandiko yanasema, mwenye haki wangu, ataishi kwa imani.
Watu tume survive ugonjwa wa ndui, Rift valley fever, swine flu etc na hili la Corona tuta survive tu kwa msaada wa Bwana!
 
Hafai kupgia kura huyu asee yani kura yng huna. Kwani tulivyo pambana vita vya kuikomboa Kagera nchi zingine zilitusaidia nn? Baada tu ya kuona janga la korona kwann hukufunga mipaka yote nakuzuia wageni kuingia isipokuwa wanatanzania na wageni wenye vibali vya kuishi na kufanya kazi. Kwaajili yako ww sasa watanzania wakosa kazi, kupatiwa likizo zisizo na malipo je sasa unalionaje hilo maisha yanazidi kuporomoka watu saivi wanakaa na kuzungumza na wenye nyumba kutokulipa mpaka janga lipite na je wao kama wa nategemea izo nyumba je huona chain nzma ya economy ulishaivuruga huku chini unabaki kuangalia ndege zimige kazi ndani yani bado unatoa watu Dar unapeleka mikoa mingine bado kwako ni sawa. Think twice tendea haki kura zetu, Kenya tayari wanaanza kutoa stimulus package ww umejipanga vp??
Rais wangu salamu kwako.

Rais wangu, kusema kweli umeniangusha sana na umezidi kuondoa imani yangu kwako. Swali ninalokuuliza, je na mwezi huu wa nne utapokea mshahara kama watumishi wengine?

Nimeuliza swali hilo kwakuwa bila ya kuhadaa wala kubwabwaja umenifanya mimi pamoja na watanzania wengi kukumbwa na majonzi kwa tunayoyaona na kuyashuhudia. Nalia kwa huzuni kubwa na nina mashaka makuu na kesho yangu pamoja na ya wenzangu.

Nakumbuka siku unaondoka Dar kwenda mkoani ukiwa Dodoma ulituambia tusitishane, tuchape kazi, tena ukasema kaugonjwa haka wala siyo tunavyokachukulia. Ni mwepesi kuliko malaria na UKIMWI. Baada ya kauli yako hiyo unajua ni nini kilitokea? Wasaidizi wako walianza kuyaishi yale uliyosema, hawakujiandaa kuchukua hatua. Wakatuzodoa kuwa Corona si chochote wala lolote. Sasa tunalia!

Pengine ungekuwa na kauli tofauti na ile hali ingekuwa tofauti Rais wangu. Pengine ungechukua tahadhari za kimamlaka kama mkuu wa nchi hali ingekuwa tofauti Rais wangu. Lakini ulipuuzia na kutoa kejeli zilizovuka mpaka juu ya ugonjwa huu. Sasa tunalia watu wako.

Ninalia nikishuhudia misafara ya ambulance kama daladala ndani ya jiji la Dar. Ninalia nikiona leo wenzetu wa mikoani wanatukimbia. Wanatukimbia kwa sababu yako Rais wangu. Wanatukimbia kwakuwa jemedari ulifanya mzaha uliopindukia ukauacha ugonjwa ukolee. Ona leo tumebaki wakiwa tukilia na kuomboleza, kukata tamaa na kumuachia Mungu!

Lakini Rais wangu, wewe uliondoka Dar mapema sana , nachelea kusema uliijua hali halisi. Mbona hukutuambia ukweli? Mbona hukutuweka huru? Umeondoka umetuacha na sasa tunatengwa na ndugu zetu na kuteseka kwa ugonjwa. Ukirudi utatueleza nini hasa? Tutakuamini tena kwa lipi zaidi?

Ninalia baada ya kushuhudia nilichokiona Mloganzila, hospitali imejaa na sasa tunatafuta nyingine! Sijui nayo itajaa? Ninalia maana siijui kesho yangu mimi binafsi hasa ninaposhuhudia watu wakitolewa ndani ya nyumba zao hoi kwa Corona. Kilio changu kinakuwa kizito kwakuwa uzembe uliofanya mwanzoni umeendelea kuufanya hata juzi. Eti hufungi mipaka kwakuwa unategemewa na nchi zingine! Watu wako waliokupa ajira wana thamani kuliko kitu chochote kile. Chonde chonde, ndiyo waliokufanya sasa unaongea ukiwa na mamlaka. Umeshindwa kutumia mamlaka kutoa amri zitakazookoa walau kwa kiasi fulani watu wako.

Swali langu kwako, mwezi huu utapokea mshahara kama watumishi wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah! hili janga ni sisi wote hata kama asipodhibiti kwa sasa basi ugonjwa utaenea na kumfikia hata yeye mwenyewe, cha msingi ni kushirikiana kwa pamoja namna ya kuuangamiza(kujikinga) huu ugonjwa.

anahitaji ushauri wa kitaalamu zaidi ikiwemo wa kitabibu na kiuchumi pia, maana nafikiri huku hana utalamu napo kama ilivyokuwa mimi. ila naimani anao wasaidizi wenye utaalamu na mambo haya
 
Hapa kuna makundi mawili, wale waliokuja Duniani kulinda Dunia na wale waliokuja Duniani kutalii.
Waliokuja kutalii hawana wasi wasi maana kwao, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.. Wale walinzi wamejawa na hofu kuu iwapo 'wataamriwa kuondoka' Duniani.
Tusitishane!
Kwa maana maandiko yanasema, mwenye haki wangu, ataishi kwa imani.
Watu tume survive rift valley fever, swine flu etc na hili la Corona tuta survive tu kwa msaada wa Bwana!
Maandiko pia yanasema "usimjaribu Bwana Mungu wako" Ndiyo maana akatuumba tofauti na viumbe wengine. Ametupa akili na uwezo wa kujua mema na mabaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu haambiliki wala hashauriki na hana huruma na mtz yeyote zaidi ya Bashite na chato
 
Hapa kuna makundi mawili, wale waliokuja Duniani kulinda Dunia na wale waliokuja Duniani kutalii.
Waliokuja kutalii hawana wasi wasi maana kwao, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.. Wale walinzi wamejawa na hofu kuu iwapo 'wataamriwa kuondoka' Duniani.
Tusitishane!
Kwa maana maandiko yanasema, mwenye haki wangu, ataishi kwa imani.
Watu tume survive rift valley fever, swine flu etc na hili la Corona tuta survive tu kwa msaada wa Bwana!

Asante boss👏👏👏
 
..nashauri asipokee mshahara wa mwezi huu.

..hakutimiza wajibu wake hivyo hastahili kupokea mshahara wa mwezi aprili.
 
Hili ni shairi hadthi ngonjera au? Kama kulia wee lia tu usisahau kufanya kazi raisi hawezi kugawana mshahara wake na wewe! Corona ipo nawa mikono kwa sabuni na maji yanayo tiririka usisaha kuvaa barakoa popote uendapo.
Sasa mwezi huu alipwe mshahara kwa kazi gani aliyofanya? Labda hela ya likizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom