Rais Wetu "Mchelea Mwana Kulia, Endelea Kuwachekea, Nyani "UKAWA!", Utayavuna Mabua

Rais Wetu "Mchelea Mwana Kulia, Endelea Kuwachekea, Nyani "UKAWA!", Utayavuna Mabua

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Wengine wetu huu mchakato wa Katiba, tangu ulipoanzishwa, tulisema humu, hauwezi kutupatia "Katiba Bora!" bali utatupatia "Bora Katiba!". Tuliowaaminia kule Bungeni tangu utungwaji wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, tuliwatahadharisha!, kuhusu "To fear the Greeks, especially when they brings gifts!". Japo mwanzo, walisua sua, wakasusa, baada ya kualikwa kufanya "rehearsals za kuikalia nyumba nyeupe", na zile chai na vitafunwa!, ni smiling faces na meno 32 nje!, wakasau yote!, wakarejea, wakabariki, wakakubali, hivyo hiki kinachoendelea sasa sio chanzo, ni matokeo tuu!, maadam haya ni maji na wameisha yavulia nguo hawana budi kuyaoga!, na kama wanatishia kutoendelea kuoga, tutawasokomezea huko bafuni na kuwamwagia maji waoge watake wasitake!.
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge Mbele Tupate Hiyo "Bora Katba!".

Sheria yenyewe ya Bunge Maalum, tumeitunga kwa haste haste, hivyo kuilipua lipua!, ikiwa na mapungufu kibao, na moja ya pungufu makubwa ni kwa sheria kumpa rais "appointments powers only" kwa mjumbe wa bunge hilo, baada tuu ya kuteuliwa, hakuna mamlaka yoyote ya kusitisha uteuzi wake!, hivyo kumpa mjumbe uhuru kamili wa kujiamulia lolote ikiwemo kutokuhudhuria vikao bila sababu yoyote ya msingi, kwa sababu hakuna kipengele chochote cha uwajibikaji kama kitu kinachofanywa na UKAWA kwa sasa, wamesusia kuendelea na mchakato na kutishia hata vikao vitakapoanza tena, wanadai hawatarejea!.

Kama hili ni kweli, na kama katika mahesabu ya akidi kupitishwa kwa hiyo "Bora Katiba" hakutawezekana kutimia mpaka UKAWA warudi Bungeni, japo naelewa wazi kipindi hiki cha mapumziko, "wale vijana wa kazi!", watasambazwa kote ndani UKAWA "man2mam!", kuhakikisha kila penye uzia!, watapenyeza rupia!, hadi akidi itimie!, lakini you can never tell with politics, jee wasipofanikiwa, itakuwaje?!. Imagine wajumbe wote wa UKAWA, wakiendelea kusimama imara na kushikilia msimamo wao wa kugomea BML, hali itakayopelekea kutukoseshea hiyo "Bora Katiba", mnaonaje tukimshauri Rais wetu JK, tuliomchagua wenyewe kwa ridhaa yetu, kuhakikisha mambo yafuatayo yanafanyika mapema na kwa haraka katika kikao kijacho cha Bunge la JMT.

  1. Sheria ya Bunge la Katiba ifanyiwe marekebisho, serikali ipeleke muswada wa marekebisho, kumpa rais Kikwete mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe wa BMK kama wajumbe hao watakosa sifa za kuendelea kuwa wajumbe wa BMK, na miongoni mwa sifa hizo, ni kutohudhuria idadi ya vikao fulani bila sababu za msingi, ikiwemo ulazima wa kuhudhuria vikao vya kufanya maamuzi!.
  2. Marekebisho mengine ni kuongezwa kipengele cha uwajibikaji kwa kuwalazimisha wajumbe wa BMK walioteuliwa, kuwajibika kwa kuhudhuria vikao vya BMK kwa lazima, kwa mujibu wa sheria na sio kwa hiyari kama ilivyo sasa!.
  3. Baada ya rais kupewa mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe watakaopoteza sifa, pia apewe mamlaka ya kuteua wajumbe wengine kutoka majina yale yale yaliyopendekezwa mwanzo, ila hakupata nafasi za uteuzi, hivyo mjumbe yoyote wa BMK akipoteza sifa za kuwa mjumbe wa Bunge hilo kwa sababu zozote zile, Rais ateue Replacement.
  4. Kwenye Bunge la JMT na kule BLW, yaletwe marekebisho ya "Simbiosis Relationship" kati ya Wajumbe wa Bunge la Katiba ambao ni Wabunge wa Bunge la JMT na BLW, wakipoteza sifa za kuwa Wajumbe wa BMK, automatically wapoteze na sifa za ubunge wa JMT na ule wa BLW automatically na pia wazuiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10!, ili kuwashikisha adabu na kuwatia nidhamu wajumbe wanaoleta uasi na kutaka kutukoseshea hiyo "Bora Katiba" tuijarajiao!.
  5. Bunge la JMT na BLW, wafanye marekebisho ya sheria za uchaguzi za NEC na ZEC, kuwa Mbunge yoyote au Mjumbe wa BLW atakaepoteza sifa za Ubunge au Ujumbe wa BLW, the 1st Runner Up kwenye uchaguzi wa mwisho, ateuliwe kuwa Mbunge au mjumbe wa BLW na hapo hapo ateuliwe mjumbe wa BMK, sio tuu ili akidi itimie tujipatie hiyo "Bora Katiba" wananchi wanaoisubiria kwa hamu ipatikane, bali pia kuokoa mabilioni ya fedha zinazotumika kuendesha chaguzi ndogo
Lengo la Mabadiliko haya ya sheria ya Bunge Maalum ni kuwaadabisha hawa waasi wa sio tuu wa UKAWA, bali kuzuia kabisa jaribio jingine lolote la uasi!, hivyo kuwafanya wajumbe wote wa BMK kuwa na nidhamu ya hali ya juu na utii wa kondoo!, ili mchakato uliobakia, uendeshwe fasta, tujipatie "Bora Katiba" tunayiosubiria kwa hamu, tuipigie kura ya ndio katika umoja wetu kama Watanzania!.

Ushauri wangu huu, unafutia kitendo cha UKAWA, ambao sio tuu wanatishia hatari ya kutopatikana kwa "Bora Katiba", sasa hawa UKAWA inazidi kuwa ni tishio kwa "usalama wa taifa!", baada ya hawa UKAWA kufanya kitendo cha "hatari sana", kwa kuunganisha nguvu kwa wapinzani wote kuwa "kitu kimoja!", katika umoja ambao ni nguvu ya hatari sana kwa mustakabili wa taifa letu, mwaka 2015!, endapo zile juhudi za "vijana kuwafarakanisha wapinzani kuhakikisha wapinzania wanaendelea kuwa fragmented" zinaendelea kushtukiwa, hivyo kuna hatari kwa wapinzani, kuungana na wakisimamisha mgombea mmoja, wa urais, ubunge na madiwani, mwaka 2015, then kuna hatari kubwa ya CCM kuanguka!, (Zanzibar ni given!, hata kwa dawa CCM haiwezi tena kushinda!), hivyo kuhatarisha hali ya usalama na amani ya taifa hili kwa sababu CCM pekee, ndicho chama pekee nchini Tanzania chenye uzoefu wa long experience ya uzoefu wa muda mrefu wa kutawala nchi, kuendesha nchi, na kuunda serikali!, hivyo Tanzania bila CCM haiwezekani!.

Na kwa vile CCM haijawahi hata mara moja, sio tuu kufikiria , bali hata kuwaza uwezekano wa kuwezekanika kushindwa, hivyo hakuna maandalizi yoyote kwa mihimili mikuu ya dola, kupewa hata japo ka orientation ya probability ya yumkini ya kuyumkinika ya kukitumikia chama kingine chochote, zaidi ya chama dola CCM walichokizoea, ambao waserikali wote ni wanachama wake!, likiwemo jeshi letu la Wananchi wa CCM, Watanzania, ambalo tumelishuhudia juzi kwenye maonyesho jinsi lilivyo shupavu na imara, sijawahi kusikia warsha, semina au kongamano lolote la aina yoyote ya "Change of Arms" kwa Jeshi kuwa tayari kumtumikia Amiri Jeshi Mkuu mwingine yoyote nje ya CCM!, hivyo ikitokea CCM imeanguka!, Nchi itayumba!, Tanzania haitatawalika!, tutaingia katika machafuko makubwa ya ajabu!, hata huu umoja na ushirikiano wa UKAWA, ni ushirikiano wa "convenience tuu!", hiyo convenience ikiiisha, patazuka patashika kubwa ya ya ajabu ya nguo na mashati kuchanika!, nchi inawezekana isitawalike kabisa!, hivyo itakuwaje?!.

Sisi wengine kazi yetu ni kusema tuu, hapa tunamshauri, rais wetu, mwenzetu, na rafiki yetu JK, endelea kuwachekea tuu hawa UKAWA kwa kujiaminisha kuwa wako likizo!, huku ukiendelea kuwaacha wakizidi kukudekea huku wakipita huku na kule kuwaamsha waliolala!, haswa kwa kuzingatia kwa sasa UKAWA ndio wana "call the shots" na CCM inafutia nyuma kuziba mashimo, kama walivyofanya majuzi kwa kutangulia, Kiwani Pemba, ndipo leo CCM ikafuatia!, nakukumbushia tuu ule msemo wa Kiswahili usemao.

"Mchelea Mwana Kulia!"..... na "Ukiwachekea Nyani.....!", Jee Mpendwa wetu uko tayari "kulia wewe", na kipindi cha mavuno ya 2015, uvune mabua?!.

NB. Kwa wale ambao ni wavivu wa kusoma bandiko refu, nilichouliza hapa in short ni Jee hawa UKAWA, wanaotaka kutuharibia nchi yetu, kwa kutaka kutukwamishia hili zoezi la kujipatia "Bora Katiba" ya muungano wa serikali mbili, unaopendwa na Watanzania wote kabisa!, watimuliwe kwa "insubordination?!, au tuendelee kuwachekea tuu kama mtu awachekeaye nyani, tukijiandaa kuvuna mabua?!.

Swali la kujiuliza, ni Jee Wanachokifanya UKAWA ni kwa Maslahi ya Taifa?!.

Jumapili Njema!.

Wasalaam.

Paskali

Note:
Kwa wasionifahamu: Paskali japobana chama, hana kambi, na hana mtu wa 2015, bali ana watu anao waaminia!.
Kwa upande wa CV yangu, Paskali ni Mhitimu wa Darasa la Saba la UPE, alipasi shule ya msingi ila hakuchaguliwa, nafasi zilijaa, hivyo ameishia darasa hilo la Saba yaani ni Standard Seven Leaver!.

Msimamo wangu kwenye hoja ya serikali ngapi ni huu Kama Kweli Nia ya Dhati ni Kuimarisha Muungano, Then...

Uzuri wa Msimamo wa CCM kutetea Serikali Mbili, nimeueleza Hapa Topic: Chonde Chonde Rais JK: Msimamo wa CCM wa Serikali Mbili, Ndio Utakauvunja Muungano!.

Uhalali wa Bunge la Katiba nimeuleza hapa!
Katiba: Nashauri Bunge Lililopo Livunjwe!, Liundwe Bunge...

Na kwa Wale Vimbelembele Kwenye BMK Wanaojidai eti wametumwa na Wananchi, pia nao niliwapatia ujumbe wao hapa
Wito kwa Bunge la Katiba: Kura iwe ya Siri kwasababu Hakuna Yeyote Aliyetumwa na Wananchi!.
 
Unataka JK awafanye nini UKAWA? Hivi na wewe umo miongoni mwa wahafidhina wanaoamini kuwa CCM imeumbwa kutawala milele na hakuna chama kingine chochote kinachoweza kutawala zaidi ya CCM?

Nadhani kama unawaza haya, na kama vijana wengi wa umri wako wanawaza kama wewe, basi tuna safari ndefu sana katika kuikomboa Tanganyika na Tanzania yetu!
 
Watu tuanalalamikia nguvu ya kufanya maamuzi we unaongezea hapo hapo!!!!!!
 
Unataka JK awafanye nini UKAWA? Hivi na wewe umo miongoni mwa wahafidhina wanaoamini kuwa CCM imeumbwa kutawala milele na hakuna chama kingine chochote kinachoweza kutawala zaidi ya CCM?

Nadhani kama unawaza haya, na kama vijana wengi wa umri wako wanawaza kama wewe, basi tuna safari ndefu sana katika kuikomboa Tanganyika na Tanzania yetu!

Ana ndoto yake huyo ambayo kwa harakati hizi za ukawa inakufa hukua anaiona!!!!!!
Hataki ukawa wawe active ili kundi lake lipate hiyo ndoto yao!!!!!

Pasco kwa nini haja binafsi izidi mahitaji ya wengi????!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mie ndiyo sijamuelewa kabisa, usitutishe na andiko refu,wala JK hakuchelea,wakati ulimtaka akatenda,halii mtu hapa, rasimu iko mezani, s3.
 
Ana ndoto yake huyo ambayo kwa harakati hizi za ukawa inakufa hukua anaiona!!!!!!
Hataki ukawa wawe active ili kundi lake lipate hiyo ndoto yao!!!!!

Pasco kwa nini haja binafsi izidi mahitaji ya wengi????!!!!!

kwakweli sijamuelewa Pasco anachotaka ni nini zaidi na kukua kwa UKAWA kunamuumiza nini! najua Pasco yuko TeamLowassa na huenda kukomaa kwa upinzani ni kuona kama ndoto zake zinafifia.

Lakini ngoja nisubiri jibu lake labda anweza kuni-prove wrong!
 
Pasco,kwanza ukumbuke zile zama za Chama kushika UTAMU zimeisha,na hapa hakuna sheria yoyote itakayotungwa ambayo itakinzana na sheria mama ya Nchi ya haki na uhuru wa kufanya maamuzi.

Pili tumeshatoka kwenye serikali ya chama kimoja,cha msingi JK aamue either avunje Bunge la katiba na kuitikia katiba kwenye dustbin tuendelee na maisha yetu. Au aamue kuwapa uhuru wanachama wa chama cheke watoe mawazo na maamuzi yatokanayo na imani ya kila mmoja na kufanya maamuzi kutokana na hali halisi ya ulimwengu wa leo.
 
Wanabodi,

Wengine wetu huu mchakato wa Katiba, tangu ulipoanzishwa, tulisema humu, hauwezi kutupatia "Katiba Bora!" bali utatupatia "Bora Katiba!". Tuliowaaminia kule bungeni tangu utungwaji wa sheria tuliwatahadharisha!, mwanzo wakasusa, baada ya chai na vitafunwa wakarejea, wakabariki, wakakubali, hivyo haya ni maji wameisha yavulia nguo hawana budi kuyaoga!.
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge Mbele Tupate Hiyo "Bora Katba!".

Sheria yenyewe ya Bunge Maalum, tumeitunga kwa kuilipua lipua, ikiwa na mapungufu kibao, na moja ya pungufu kubwa ni kwa mjumbe baada ya kuteuliwa, kuwa na mamlaka ya kujiamulia lolote, bila sheria hiyo kumbana kwa uwajibikaji kama kitu kinachofanywa na UKAWA kwa sasa, wamesusia kuendelea na mchakato na kutishia hata vikao vitakapoanza tenza, hawatarejea!. Kama hili ni kweli, na kama katika mahesabu ya kupitishwa kwa hiyo "Bora Katiba" hakutawezekana kwa akidi kutimia mpaka UKAWA warudi Bungeni, then mnaonaje kama mambo yafuatayo yangefanyika.

  1. Sheria ya Bunge la Katiba ifanyiwe marekebisho, serikali ipeleke muswada wa marekebisho, kumpa rais Kikwete mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe wa BMK kama wajumbe hao, hawatahudhuria baadhi ya vikao, vikiwemo vile vikao vya kufanya maamuzi.
  2. Marekebisho mengine ni ya kuwalazimisha wajumbe wa BMK walioteuliwa, kuwajibika kwa kuhudhuria vikao vya BMK kwa lazima, kwa mujibu wa sheria na sio kwa hiyari kama ilivyo sasa!.
  3. Baada ya rais kupewa mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe waasi, pia apewe mamlaka ya kuteua wajumbe wengine kutoka majina yale yale yaliyopendekezwa mwanzo, ila hakupata nafasi za uteuzi, hivyo mjumbe yoyote wa BMK akipoteza sifa za kuwa mjumbe wa Bunge hilo kwa sababu zozote zile, Rais ateue Replacement.
  4. Yaletwe marekebisho ya "Simbiyosis Relationship" kati ya Wajumbe wa Bunge la Katiba Ambao ni Wabunge wa la JMT na BLW, wakipoteza sifa zao za kuwa Wajumbe wa BMK, automatically wapoteze na soifa zao za ubunge wa JMT na BLW automatically na pia wazuiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10!, ili kuwashikisha adabu na kuwatia nidhamu!.
  5. Bunge lifanye marekebisho ya sheria ya uchaguzi, kuwa Mbunge yoyote au Mjumbe wa BLW atakapoteza sifa za Ubunge au Ujumbe wa BLW, the 1st Runner Up kwenye uchaguzi wa mwisho, ateuliwe mbunge au mjumbe wa BLW na hapo hapo ateuliwe mjumbe wa BMK, akidi itimie tujipatie hiyo "Bora Katiba" wanamchi wanaoisubiria kwa hamu!.
Lengo la Mabadiliko haya ya seria ya Bunge Maalum ni kwa lengo la kuwaadabisha waasi wa UKAWA, ambao sio tuu wanatishia hatari ya kutopatikana kwa "Bora Katiba", sasa UKAWA inazidi kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa!, wameunganisha nguvu kwa wapinzani wote kuwa kitu kimoja, na mwaka 2015, wakisimamisha mgombea mmoja, kuna hatari kubwa ya CCM kushindwa (Zanzibar ni hata kwa dawa CCM haiwezi tena kushinda), hivyo kuhatarisha hali ya usalama na amani ya taifa hili kwa sababu CCM ndicho chama pekee nchini Tanzania chenye uzoefu wa kutawala na kuendesha nchi, hivyo Tanzania bila CCM haiwezekani!.

Na kwa vile CCM haijawahi hata kuwaza uwezekano wa kushindwa, hivyo hakuna maandalizi yoyote kwa mihimili mikuu ya dola, kupewa hata orientation ya kukitumikia chama kingine chochote, likiwemo jeshi letu ambalo tumelishuhudia juzi kwenye maonyesho jinsi lilivyo imara, sijawahi kusikia warsha, semina sau kongamano lolote la "Change of Arms" kwa Jeshi kuwa tayari kumtumia Amiri Jeshi Mkuu mwingine yoyote nje ya CCM, hivyo ikitokea CCM imeanguka!, Tanzania haitatawalika!, tutaingia katika machafuko makubwa ya ajabu!, hata huu umoja na ushirikiano wa UKAWA, ni ushirikiano wa "convenience tuu!", hiyo convenience ikiiisha, patazuka patashika ya ajabu ya mashati kuchanika!, nchi haitatawalika kabisa!.

Sisi wengine kazi yetu ni kusema tuu, hapa namwambia rafiki yetu JK, endelea kuwachekea tuu hawa UKAWA kwa kujiaminisha wako likizo!, huku ukiendelea kuwaacha wakudekee!, nakukumbusha tuu ule msemo wa Kiswahili usemao.

"Mchelea Mwana Kulia!.....

NB. Kwa wale ambao ni wavivu wa kusoma bandiko refu, nilichouliza hapa ni Jee Hawa UKAWA, wanaotaka kutuharibia nchi, watimuliwe kwa "insubordination?!, au tuendelee kuwachekea nyani, tukijiandaa kuvuna mabua?!. Swali la kujiuliza, ni Jee Wanachokifanya UKAWA ni kwa Maslahi ya Taifa?!.

Jumapili Njema!.

Wasalaam.

Pasco.
intarahamwe@work
 
hii nayo ni kama tamthilia nyingine kwa mtazamo wangu lakini
 
Pasco,kwanza ukumbuke zile zama za Chama kushika UTAMU zimeisha,na hapa hakuna sheria yoyote itakayotungwa ambayo itakinzana na sheria mama ya Nchi ya haki na uhuru wa kufanya maamuzi.

Pili tumeshatoka kwenye serikali ya chama kimoja,cha msingi JK aamue either avunje Bunge la katiba na kuitikia katiba kwenye dustbin tuendelee na maisha yetu. Au aamue kuwapa uhuru wanachama wa chama cheke watoe mawazo na maamuzi yatokanayo na imani ya kila mmoja na kufanya maamuzi kutokana na hali halisi ya ulimwengu wa leo.

kabla ya ukawa wangeanza na ccm ambao wajadili katiba yao badala ya tume kwakulazima hoja zao
 
Wanabodi,

Wengine wetu huu mchakato wa Katiba, tangu ulipoanzishwa, tulisema humu, hauwezi kutupatia "Katiba Bora!" bali utatupatia "Bora Katiba!". Tuliowaaminia kule bungeni tangu utungwaji wa sheria tuliwatahadharisha!, mwanzo wakasusa, baada ya chai na vitafunwa wakarejea, wakabariki, wakakubali, hivyo haya ni maji wameisha yavulia nguo hawana budi kuyaoga!.
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge Mbele Tupate Hiyo "Bora Katba!".

Sheria yenyewe ya Bunge Maalum, tumeitunga kwa kuilipua lipua, ikiwa na mapungufu kibao, na moja ya pungufu kubwa ni kwa mjumbe baada ya kuteuliwa, kuwa na mamlaka ya kujiamulia lolote, bila sheria hiyo kumbana kwa uwajibikaji kama kitu kinachofanywa na UKAWA kwa sasa, wamesusia kuendelea na mchakato na kutishia hata vikao vitakapoanza tenza, hawatarejea!. Kama hili ni kweli, na kama katika mahesabu ya kupitishwa kwa hiyo "Bora Katiba" hakutawezekana kwa akidi kutimia mpaka UKAWA warudi Bungeni, then mnaonaje kama mambo yafuatayo yangefanyika.

  1. Sheria ya Bunge la Katiba ifanyiwe marekebisho, serikali ipeleke muswada wa marekebisho, kumpa rais Kikwete mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe wa BMK kama wajumbe hao, hawatahudhuria baadhi ya vikao, vikiwemo vile vikao vya kufanya maamuzi.
  2. Marekebisho mengine ni ya kuwalazimisha wajumbe wa BMK walioteuliwa, kuwajibika kwa kuhudhuria vikao vya BMK kwa lazima, kwa mujibu wa sheria na sio kwa hiyari kama ilivyo sasa!.
  3. Baada ya rais kupewa mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe waasi, pia apewe mamlaka ya kuteua wajumbe wengine kutoka majina yale yale yaliyopendekezwa mwanzo, ila hakupata nafasi za uteuzi, hivyo mjumbe yoyote wa BMK akipoteza sifa za kuwa mjumbe wa Bunge hilo kwa sababu zozote zile, Rais ateue Replacement.
  4. Yaletwe marekebisho ya "Simbiyosis Relationship" kati ya Wajumbe wa Bunge la Katiba Ambao ni Wabunge wa la JMT na BLW, wakipoteza sifa zao za kuwa Wajumbe wa BMK, automatically wapoteze na soifa zao za ubunge wa JMT na BLW automatically na pia wazuiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10!, ili kuwashikisha adabu na kuwatia nidhamu!.
  5. Bunge lifanye marekebisho ya sheria ya uchaguzi, kuwa Mbunge yoyote au Mjumbe wa BLW atakapoteza sifa za Ubunge au Ujumbe wa BLW, the 1st Runner Up kwenye uchaguzi wa mwisho, ateuliwe mbunge au mjumbe wa BLW na hapo hapo ateuliwe mjumbe wa BMK, akidi itimie tujipatie hiyo "Bora Katiba" wanamchi wanaoisubiria kwa hamu!.
Lengo la Mabadiliko haya ya seria ya Bunge Maalum ni kwa lengo la kuwaadabisha waasi wa UKAWA, ambao sio tuu wanatishia hatari ya kutopatikana kwa "Bora Katiba", sasa UKAWA inazidi kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa!, wameunganisha nguvu kwa wapinzani wote kuwa kitu kimoja, na mwaka 2015, wakisimamisha mgombea mmoja, kuna hatari kubwa ya CCM kushindwa (Zanzibar ni hata kwa dawa CCM haiwezi tena kushinda), hivyo kuhatarisha hali ya usalama na amani ya taifa hili kwa sababu CCM ndicho chama pekee nchini Tanzania chenye uzoefu wa kutawala na kuendesha nchi, hivyo Tanzania bila CCM haiwezekani!.

Na kwa vile CCM haijawahi hata kuwaza uwezekano wa kushindwa, hivyo hakuna maandalizi yoyote kwa mihimili mikuu ya dola, kupewa hata orientation ya kukitumikia chama kingine chochote, likiwemo jeshi letu ambalo tumelishuhudia juzi kwenye maonyesho jinsi lilivyo imara, sijawahi kusikia warsha, semina sau kongamano lolote la "Change of Arms" kwa Jeshi kuwa tayari kumtumia Amiri Jeshi Mkuu mwingine yoyote nje ya CCM, hivyo ikitokea CCM imeanguka!, Tanzania haitatawalika!, tutaingia katika machafuko makubwa ya ajabu!, hata huu umoja na ushirikiano wa UKAWA, ni ushirikiano wa "convenience tuu!", hiyo convenience ikiiisha, patazuka patashika ya ajabu ya mashati kuchanika!, nchi haitatawalika kabisa!.

Sisi wengine kazi yetu ni kusema tuu, hapa namwambia rafiki yetu JK, endelea kuwachekea tuu hawa UKAWA kwa kujiaminisha wako likizo!, huku ukiendelea kuwaacha wakudekee!, nakukumbusha tuu ule msemo wa Kiswahili usemao.

"Mchelea Mwana Kulia!.....

NB. Kwa wale ambao ni wavivu wa kusoma bandiko refu, nilichouliza hapa ni Jee Hawa UKAWA, wanaotaka kutuharibia nchi, watimuliwe kwa "insubordination?!, au tuendelee kuwachekea nyani, tukijiandaa kuvuna mabua?!. Swali la kujiuliza, ni Jee Wanachokifanya UKAWA ni kwa Maslahi ya Taifa?!.

Jumapili Njema!.

Wasalaam.

Pasco.

Unadhani nchi inaweza kuongozwa kama famlya ya kwenu? kana kwamba babako ama mamako akiamua hakuna mjadala.
 
Sijui kama pasco yuko serious,???? kwake maslahi ya chama kwanza nchi badae!!!!!!!! Katiba bora??? sasa ameona bora katiba!!!! Njoo huku Pasco weka mambo sawa
 
Back
Top Bottom