Katiba sio lazima ipatikane sasa. Hata baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 Katiba inaweza kuandikwa. Uraisi ni Taasisi sio Jakaya Mrisho Kikwete. Baadhi ya watu humu ndani wanaibinafsisha Katiba Mpya kwa JK, sio kweli Katiba sio ya mtu kujipatia sifa.
Kwa kuwa tuna mambo mengi kwa kipindi kifupi ni bora tukaiahirisha mpaka hapo baadaye. Baada ya uchaguzi 2015, kutakuwa na sura mpya Bungeni hivyo kuleta mawazo mapya, wabunge wengine wenye misimamo ya UKAWA wanaweza kuwa wameshindwa uchaguzi, tutakuwa na rais mpya mwenye mawazo mapya pia. Watanzania pia watakuwa na mawazo mapya baada ya kuyatathimini ya sasa. 'Second thought is the best thought'. Subira yavuta kheri na harakaharak haina baraka. Ni bora kuyapima mawazo ya pande zote bila kuegemea upande mmoja na kufikiria kuafanyia kazi kwa pamoja bila ya kuathiri utaifa wetu kwa kuwa wote tu watanzania kuwa UKAWA au CCM hakutuondolei au kutuongezea hisa ya utaifa wetu. Sote ni watanzaia wenye mawazo tofauti juu ya Tanzania yetu iweje. Kuwa na mawazo tofauti ndiyo uhai wa Taifa lolote duniani, jambo lamsingi ni jinsi gani tuyaweke pamoja mawazo mazuri halafu tuendelee mbele. Kuzira mjadala ni ishara ya kutokomaa kimawazo lakini pia kulazimisha mawazo yako tu ni ishara ya ubabe au uwoga au kutojiamini au udikteta