Wanabodi,
Wengine wetu huu mchakato wa Katiba, tangu ulipoanzishwa, tulisema humu, hauwezi kutupatia "Katiba Bora!" bali utatupatia "Bora Katiba!". Tuliowaaminia kule bungeni tangu utungwaji wa sheria tuliwatahadharisha!, mwanzo wakasusa, baada ya chai na vitafunwa wakarejea, wakabariki, wakakubali, hivyo haya ni maji wameisha yavulia nguo hawana budi kuyaoga!.
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge Mbele Tupate Hiyo "Bora Katba!".
Sheria yenyewe ya Bunge Maalum, tumeitunga kwa kuilipua lipua, ikiwa na mapungufu kibao, na moja ya pungufu kubwa ni kwa mjumbe baada ya kuteuliwa, kuwa na mamlaka ya kujiamulia lolote, bila sheria hiyo kumbana kwa uwajibikaji kama kitu kinachofanywa na UKAWA kwa sasa, wamesusia kuendelea na mchakato na kutishia hata vikao vitakapoanza tenza, hawatarejea!. Kama hili ni kweli, na kama katika mahesabu ya kupitishwa kwa hiyo "Bora Katiba" hakutawezekana kwa akidi kutimia mpaka UKAWA warudi Bungeni, then mnaonaje kama mambo yafuatayo yangefanyika.
Lengo la Mabadiliko haya ya seria ya Bunge Maalum ni kwa lengo la kuwaadabisha waasi wa UKAWA, ambao sio tuu wanatishia hatari ya kutopatikana kwa "Bora Katiba", sasa UKAWA inazidi kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa!, wameunganisha nguvu kwa wapinzani wote kuwa kitu kimoja, na mwaka 2015, wakisimamisha mgombea mmoja, kuna hatari kubwa ya CCM kushindwa (Zanzibar ni hata kwa dawa CCM haiwezi tena kushinda), hivyo kuhatarisha hali ya usalama na amani ya taifa hili kwa sababu CCM ndicho chama pekee nchini Tanzania chenye uzoefu wa kutawala na kuendesha nchi, hivyo Tanzania bila CCM haiwezekani!.
- Sheria ya Bunge la Katiba ifanyiwe marekebisho, serikali ipeleke muswada wa marekebisho, kumpa rais Kikwete mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe wa BMK kama wajumbe hao, hawatahudhuria baadhi ya vikao, vikiwemo vile vikao vya kufanya maamuzi.
- Marekebisho mengine ni ya kuwalazimisha wajumbe wa BMK walioteuliwa, kuwajibika kwa kuhudhuria vikao vya BMK kwa lazima, kwa mujibu wa sheria na sio kwa hiyari kama ilivyo sasa!.
- Baada ya rais kupewa mamlaka ya kutengua uteuzi wa wajumbe waasi, pia apewe mamlaka ya kuteua wajumbe wengine kutoka majina yale yale yaliyopendekezwa mwanzo, ila hakupata nafasi za uteuzi, hivyo mjumbe yoyote wa BMK akipoteza sifa za kuwa mjumbe wa Bunge hilo kwa sababu zozote zile, Rais ateue Replacement.
- Yaletwe marekebisho ya "Simbiyosis Relationship" kati ya Wajumbe wa Bunge la Katiba Ambao ni Wabunge wa la JMT na BLW, wakipoteza sifa zao za kuwa Wajumbe wa BMK, automatically wapoteze na soifa zao za ubunge wa JMT na BLW automatically na pia wazuiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10!, ili kuwashikisha adabu na kuwatia nidhamu!.
- Bunge lifanye marekebisho ya sheria ya uchaguzi, kuwa Mbunge yoyote au Mjumbe wa BLW atakapoteza sifa za Ubunge au Ujumbe wa BLW, the 1st Runner Up kwenye uchaguzi wa mwisho, ateuliwe mbunge au mjumbe wa BLW na hapo hapo ateuliwe mjumbe wa BMK, akidi itimie tujipatie hiyo "Bora Katiba" wanamchi wanaoisubiria kwa hamu!.
Na kwa vile CCM haijawahi hata kuwaza uwezekano wa kushindwa, hivyo hakuna maandalizi yoyote kwa mihimili mikuu ya dola, kupewa hata orientation ya kukitumikia chama kingine chochote, likiwemo jeshi letu ambalo tumelishuhudia juzi kwenye maonyesho jinsi lilivyo imara, sijawahi kusikia warsha, semina sau kongamano lolote la "Change of Arms" kwa Jeshi kuwa tayari kumtumia Amiri Jeshi Mkuu mwingine yoyote nje ya CCM, hivyo ikitokea CCM imeanguka!, Tanzania haitatawalika!, tutaingia katika machafuko makubwa ya ajabu!, hata huu umoja na ushirikiano wa UKAWA, ni ushirikiano wa "convenience tuu!", hiyo convenience ikiiisha, patazuka patashika ya ajabu ya mashati kuchanika!, nchi haitatawalika kabisa!.
Sisi wengine kazi yetu ni kusema tuu, hapa namwambia rafiki yetu JK, endelea kuwachekea tuu hawa UKAWA kwa kujiaminisha wako likizo!, huku ukiendelea kuwaacha wakudekee!, nakukumbusha tuu ule msemo wa Kiswahili usemao.
"Mchelea Mwana Kulia!.....
NB. Kwa wale ambao ni wavivu wa kusoma bandiko refu, nilichouliza hapa ni Jee Hawa UKAWA, wanaotaka kutuharibia nchi, watimuliwe kwa "insubordination?!, au tuendelee kuwachekea nyani, tukijiandaa kuvuna mabua?!. Swali la kujiuliza, ni Jee Wanachokifanya UKAWA ni kwa Maslahi ya Taifa?!.
Jumapili Njema!.
Wasalaam.
Pasco.
una minyoo ya kike wewe gamba!wewe serukamba nini?
