Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Wewe ni mwanadamu wa jinsia ya kike. Kila mtu anafahamu juu ya matatizo ya jinsia katika dunia hii na kila nchi inajitahidi kuondoa matatizo hayo. Njia mojawapo ni kuachana na hali ya kulinganisha jinsia hizi ktk kazi, ili tuzifunike tofauti hizo.

Tangu Samia uliposhika nafasi ya urais, kila hotuba yake imekuwa ni kama nafasi ya kujitetea kwamba unaweza nafasi hiyo, na kuwatetea wanawake wenzako. Ombi langu kwako, achana na kujitetea.

Angalia unavyoshangiliwa na wanawake wenzako, wakiona kama ni mafanikio yao kumbe wengine hawawezi kama wanaume wengine wasivyoweza.

Mfano mzuri dunia hii ni Margret Thatcher na sasa ni yule ‘binti’ mdogo anayeiongoza serikali ya Finland, Sanna Marin kama alivyokuwa Thatcher hataki kabisa kukaribisha jambo hilo la kuonesha wanawake wanaweza au hawawezi. Kwake yeye ni kiongozi na siyo kiongozi mwanamke.
 
Mimi naona apate ziara moja aende Ughaibuni (official visit) akapigiwe mizinga 21 na heshima zote ili aongeze kujiamini na ajue kabisa ndani ya dunia hii yeye siyo wa Rais kwanza mwanamke.

Kina Queen Elizabeth wametawala dunia miaka na miaka. Majukumu mazito kuliko aliyonayo.
 
Mkuu Zygot kuna tofauti kati ya jinsi na jinsia miongoni mwa watu. Jinsia ama "gender" kwa lugha ya Kingereza ni mahusiano ya kijamii na kiutamaduni yenye kuhusisha mgawanyo wa majukumu muhimu kwa kuangilia jinsi ya mtu, yaani Mume (Me[emoji124]) au Kike (Ke[emoji126]). Kwa hiyo basi jinsi ya Rais wetu au "sex category" kwa lugha ya kigeni ni ya Kike (Ke) [emoji126].
 
Mimi naona apate ziara moja aende Ughaibuni ( official visit ) akapigiwe mizinga 21 na heshima zote ili aongeze kujiamini na ajue kabisa ndani ya dunia hii yeye siyo wa kwanza.
Tatizo, huko pia atakwenda kupewa support kama mwanamke. Nchi kama US siyo mfano mzuri maana nao bado wanaona ni ajabu m'ke kuwa kiongozi wa nchi. Ndo maana hata makamu wao alituma salamu maalumu, 'za kike.'
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa.
 
Tatizo, huko pia atakwenda kupewa support kama mwanamke. Nchi kama US siyo mfano mzuri maana nao bado wanaona ni ajabu m'ke kuwa kiongozi wa nchi. Ndo maana hata makamu wao alituma salamu maalumu, 'za kike.'
Rais kupewa support na mwanamke mwenzake siyo jambo baya maana kumbuka tupo kwenye mission ya Beijing.

Muhimu ni kuprove kuwa anaweza kufanya vizuri zaidi.
 
Hata mimi hili jambo jana lilinifikirisha, nikajisemea moyoni inawezekana ndani ya Chama chake au watu walio karibu naye wanazungusha maneno kwamba hataweza kuongoza hii Nchi, nionavyo ndani ya chama kuna kila zana inainuliwa kumponda Mh. Rais, watu wa Jiwe wapo vitani muda wote, hawataki kuamini kwamba sasa keki imevunda wakae kwa kutulia.

Mama akae kwa kujiamini, aunde timu anayoiamini bila shaka yoyote, atoe takataka na chawa wote wa aliyepita, tayari anaye Mabeyo wasiwasi wa nini?
 
Back
Top Bottom