Rais Zelensky utawalipa nini NATO?

Wewe inaonekana siyo mfuatiliaji.

Hayo mataifa ya Magharibi, hayawezi kukubali kushindwa. Ukraine itaathirika sana, hasa kwenye kupoteza uhai wa watu wake, lakini ni lazima Russia itashindwa hata kama itakuwa ni baadabya muda.

Hivi unajua kuwa hata uwepo wa hiyo nchi ya Ukraine ni matokeo ya Urusi kushindwa dhidi ya mataifa ya Magharibi? Hiyo Ukraine ilikuwa ni sehemu ya USSR. Unafahamu ni kwa nini USSR ilikufa? Unafahamu kuwa Russia baada ya wananchi wake kuishi kwa mateso makubwa kwa miaka mingi, huku wananchi wake wengi wakitorokea mataifa ya Magharibi, ikawa haina namna zaidi ya kuyapigia magoti mataifa ya Magharibi, nayo yakampa masharti, na baada ya kuyatekeleza ndipo akaondolewa vikwazo, akamwagiwa misaada ya pesa iliyomsaidia kuanza kuujenga uchumi wake uliokuwa umedorora sana?

Nchi za Magharibi zimepata mahali pa kuidhoofisha sana Urusi. Na haya mataifa ya Magharibi hayatatulia mpaka yahakikishe Urusi imetokomea. Kumbuka Urusi ndiyo inayowapa tekinolojia ya nuklia North Korea na Iran. Na mataifa ya Magharibi yanahofu kuwa huenda baadaye ikaipa tekinolojia hiyo Syria na mataifa mengine yenye tawala za kidikteta, zikiwemo za Afrika. Hivyo hawatamwacha ashinde, kwa sababu licha ya kuisaidia Ujraine, nyuma yake ni kutafuta uhakikisho kuwa Russia haiwi hatari kwa usalama wao kupitia tekinolojia ya nuklia inayoisambaza kwa tawala za kidikteta.

Kushindwa kwa Urusi hakutakuwa kwenye battlefield, bali itakuwa mchanganyiko wa mbinu. Hakuna uwekezaji, mapato yanashuka, skilled labor inakimbia, mapato yaliyobakia kidogo yanagharamia vita, watu wanaishi maisha magumu, etc. Kwa upande mwingine, haya mataifa mengine kwa umoja wao wana uwezo wa kuitegemeza Ukraine kwa kipindi kirefu kadiri watakavyo.
 
Mkuu kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa mataifa washirika wa Nato kwa sasa wanachopigania ni kuhakikisha wanamuangusha Putin.

Hawana ubaya na wananchi wa Urus hata kidogo hivyo basi siku Putin akitoka madarakani tu basi na vita ya Nato na Rusia inasimama hapo hapo.

Kumbuka kuwa rais ni taasisi na akitoka Putin atakuja mrusi mwingine ataendeleza hiyo teknolojia ya nyuklia.
 
Moja ya vijitu vijinga kabisa duniani ni hako ka Zelensky. Kangeifahamu kwa kina Marekani na washirika wake, kasingekubali kuingia kwenye huu mtego.
Alafu kanajiona ni bonge la mjanja wakati kila kitu kanapiga magoti kuomba.
 
Nyiny watanganyika mliwalipa nini waliowasaidia kumkabili Idd Amin ?
 
Kinachoniacha hoi ni mtu hambaye nilimuona kuwa role model wangu,akiwemo Salary Slip pamoja na wengine waliokuwa wakiungana kwa pamoja kupinga mauji ya wasio na hatia, udhalimu,roho mbaya,ufedhuli ,kiburi na kila aina ya tabia mbaya alizokuwanazo jiwe..,eti Leo hii mtu huyohuyo anaungana na wengine kushangilia mauaji yanayofanywa na dikiteta Putin kwa watu hambao hawakuwai kumrushia hata punje ya Mchele kwenye mipaka yake..mtu huyohuyo anamshangilia kiongozi anayefanya kila njia kuwanyamazisha wakosoaji wake ikiwemo kuwapa sumu

Kweli ukijaribu kumsoma mwanadamu unaweza kupata stroke kwenye ubongo,ni vema mambo mengine ukarelax na kujifanya kama huyaoni!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Kajamaa kanatia kichefuchefu kwa kuwauza wananchi wake.
Kwan huyo ndo alienda Urusi kuwaomba waivamie Ukraine ? au Urusi alipoipora Crime Zele ndo alikuwa rais kipind hicho ? au Urus alipokuwa anasaidia waas kujitenga mwaka 2014 hadi 2019 Zele ndo alichochea ? Hii vichaa mpo wengi sema mkinunua smart mnaanza ambukiza wengine ukichaa , huo mgogoro mchoche ni urusi na ndio maana majiran wengine wa Urusi wameanza jihami mapema sana mf Moldova katuma barua kujiunga na EU pia Georgia anapambania kujiunga na NATO huku Finland akiwa tyr kajiunga na NATO , sasa mmatumbi uliyeferi hesab za kuchagua ndo unajua zaid ya majiran wa urusi ?
 
Kwan sijaelewa Ukraine imeivamia Urusi au Urusi kaivamia Ukraine , je uhusika wa Zele ni upi ? Kumkabili Putin au ulitaka aache nchi iwe kolon la urusi kama alivyofanya kwa majimbo ya donetsk na luhansk alisema anayasaidia kuwa huru ila akaja yaingiza Urusi , kwako hii ni sawa ?
 
Kwani ukionyesha kutofautiana na mchango wa mtu kwa busara utakosa nini ndugu?

Staarabika maana wenzako tulishatoka huko kwenye kutumia matusi.
 
Inawezekana kabisa mkuu maana kuna binadamu wanaomba kabisa matatizo
Ww mchambia majan na hao wazungu wa mashariki ya ulaya ( jiran zake Putin ) nan anajua hasa hiyo migogoro na njia ipi hasa ya kujikwamua kutoka kwa russia domination ?
 
Korea awe tajiri kuliko urusi Amkaa mkuu
 
Ww mchambia majan na hao wazungu wa mashariki ya ulaya ( jiran zake Putin ) nan anajua hasa hiyo migogoro na njia ipi hasa ya kujikwamua kutoka kwa russia domination ?
Afadhali nikupige block maana akili huna.
 
Rais Zelensky nikimuokoa ninamkumbuka JK wa TZ
 
Ukisoma koment za waswahili kama nyiny unaifunza kuwa waafrika bado mpo karne ya 15 , ndio maana mlitawaliwa , mnaamin kila ugomv unalenga kushinda kwa kumtoa mwenzio damu ? Urusi anapotezewa muda hapo ili awe dhohofi kiuchumi , warusi wanalalamika sana , na kibaya China kateka uchumi wa Urusi sasa hv kila kitu ndan ya Urusi kimekuwa made in china , baada ya vita kama Urus akishinda bas anaenda kuwa kolon la china indirectly , na kama Urusi akishindwa bas ndan ya Urusi kuna jamii zinakandamizwa miaka na miaka hasa zile zenye asili ya kichina /asia na weng wenu mnaamin warusi wana asili ya kizungu tu , sio kwel bali upande wa East ya Urusi imetawaliwa na waasia na wamenyimwa fursa kila kona ya nchi yao ya Urusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…