mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
- Thread starter
- #21
Ni kweli Urusi haiwezi kupigana na nchi zote za NATO na ikabaki salama, lakini pia ni kweli kuwa nchi zote za NATO haziwezi kuipiga Urusi na zikabaki salama!!Acha kujitoa ufahamu urusi hawezi kupigana na nchi Zote za NATO Na akabaki salama ni vile tu bado zina maslahi yao nchini urusi
Ngoja nikupe hii: Amerika imekuwa ikiishawishi poland itoe ndege zake za vita (Mig 29) kwa Ukraine halafu yenyewe itaipa Poland ndege zingine kufidia zile zilizotolewa na Poland. Poland ikakubali, lakini ikasema sisi tutawapa Marekani, kisha Marekani ndio wawajibike kuzipeleka Ukrane!! Mchezo ukawa umeishia hapo!! Marekani ikalalamika kuwa hayo hayakuwa mapatano!! Hakuna anayethubutu kufanya chochote kitakachohalalisha Urusi iishambulie!! Marekani keshaingia baridi tayari, na hakuwa na jibu lolote zaidi ya kulalamika kuwa hamkutujulisha hivyo kabla. Poland imeshashtuka kungali mapema kuingizwa choo cha kike na Marekani kama yule Zelensky wa Ukraine alivyojikuta kwenye choo cha kike!!