Ramadhan kareem 2024

Ramadhan kareem 2024

Chumchang Changchum

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2013
Posts
5,988
Reaction score
6,226
Mwezi wa Ramadhan ni moja kati ya nguzo kuu za Uislamu. Kama ilivyo idhinishwa katika Kitabu kiukufu {QUR-AN 2 : 185}cha Waislamu. Siku za kufumga kati ya 29 mpaka 30 pia inategemea muandamo wa Mwezi.

AFYA NA FAIDA YA SWAUMU
1. Ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.

2. Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.

3. Faida nyingine ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya masikini na tajiri.

4. Pia funga hutusaidia kiafya kwani huifanya mifumo kadhaa ya mwili nayo kupata wasaa wa kupumzika kwa mda fulani.

NAWATAKIENI SWAUMU NJEMA YA MWEZI WA RAMADHAN
 

Attachments

  • instagram_20231202_110529.mp4
    1.9 MB
Muhimu..
Kwa wafungaji.. Moja kati Sunna tukufu {muhimu} kwa mfungaji ni kuharakisha kufungua.. Baadakya kuzama kwa jua {Magharibi}

Imepokelewa Hadith toka kwa Bin Tirmidhy, Ibnu Khuzayma na Ibnu Habban: “Hakika nimpendaye zaidi miongoni mwa waja wangu ni anayefanya haraka katika wao
 
Ya ayyuha lladhina amanu,qutiba alaykumu swiyamu kamaa kutiba ala ladhiina min qabliqum...laalakum taktakuun...

"Enyi watu/waumini mlioamini katika mungu,hakika mmefaradhishiwa kufunga mwezi wa ramadhani kama ambavyo walivyofunga waliokuepo kabla yenu..
Fungeni mwezi wa ramadhani ili mpate kuwa wachamungu"
 
Qur-an..
Mwezi wa Ramadhani ndio Mwezi ulio teremshwa Qur-an iwe uongofu kwa watu …………" Kwa sababu ndio Mwezi ulio teremshwa Qurani kwa Nabii Muhammad {S. A. W} ,
Inakulazimu, inatakiwa kwa Muislam kufanya bidii kuisoma Qur-an na ikiwezekana hata Juzuu zote 30 {Hii ni kwa faida ya Akhera yako} Tujitahidi basi hata Juzuu Moja au zaidi..
Umeshindwa umeshindwa basi tenga Muda sikiliza Qur-an. INSHA MWENYEZI MUNGU ATUWEZESHE...
Next... Swala ma Swaumu
 
Back
Top Bottom