Mimi ni Simba ila nashangazwa na hizi shutuma kwa refa, Mimi nadhani refa na wasaidizi wake walikuwa na game nzuri tu. Ni lazima tuwe tunakubali matokeo na kama kuchambua basi tuangalie madhaifu ya team zetu. Mpira kipindi cha kwanza quality haikuwa nzuri mechi ya kawaida kipindi cha pili kilikuwa kizuri,
Simba alianza vizuri na chance mwanzoni tu tukapoteza ilikuwa goal wazi kabisa Yanga wamekuja kuamka kipindi cha pili kidogo kidogo wakawa hatari unaziona lakini tukija kwenye goal nikosa la goal keeper, makipa bora mipira kama ile wanaisukuma nje tu, Kamara kanikumbusha mipira ya miaka ya 90 kipa kama hujaruka kama nyani unaonekana sio kipa, ukitema sio kipa siku hizi kipa haruki hovyo na akiruka anasukuma mpira nje tu, Kamara ni kipa mzuri wajibu wa kocha wa makipa kuondoa udhaifu huo. Simba na Yanga wamepambana na goal kosa moja tu ila tusikimbilie refa huko hapana, waamuzi wamejitahidi sana ukichukua hakuna VAR.