Ramadhan Special Thread

[emoji617]HUKMU YA MWENYE KUOTA MCHANA WA RAMADHANI


حكم من احتلم في نهار صيامه لمعالي الشيخ صالح الفوزان حفظه الله ورعاه


[emoji441]Muulizaji anauliza: ni ipi hukmu ya mwenye kuota mchana wa ramadhani (na yakamteremka manii) je huhesabiwa yeye kusihi kwa funga yake au haihesabiwi?


[emoji2424]Jawabu kutoka kwa Al-allaamah swaaleh Al-fawzan (Allah amhifadhi)


Mwenye kuota mchana wa ramadhani basi hakika yake ni lazima aoge pindi akiota na manii yakateremka, na kuhusu funga yake ni sahihi kwani hakika ya kuota sio kwa khiyari yake na sio kwa makusudio yake, basi jambo hilo haliathiri funga yake, funga yake itakuwa ni sahihi hakuna madhara juu yake, lakini jambo la wajibu kwa muislam pindi akiota na manii yakateremka basi wajibu juu yake aoge kogo la janaba. Naam."


[emoji442]Sikiliza kwa faida clip ina sekunde 37 tu, ingia katika channel ya YouTube kuskiliza hii kisha subscriber channel yetu ili kupata faida za shekh fawzan kila zikitoka


••┈•✿•┈•••••°••○••°••••┈•✿•┈••

[emoji3578] Abou huda'a Al-jaziiriyyi حفظه الله


[emoji455]FAWA'AID SHEKH FAUZAN حفظه الله[emoji2391]


FAWA'AID SHEKH FAUZAN
 
Waalaykm Salam warahmatullah wabarakatuh.

Pole sana na matatizo ndugu. Allah Atakufanyia wepesi. Baada ya kila zito na wepesi upo....usijitie dhiki ya nafs...mitihani ndio tumeumbiwa binaadam, sio peke yako unae face challenges...Muombe Mungu Akufanyie wepesi mambo yako.

Nenda kaftari kwa rafki yako...nae usimkoseshe fadhila zake. Watu wanajua wapo kwenye mwezi wa kuchuma hawataki kupoteza fursa
 
Allah akulipe kheri.
 
Assalaam alaykum naomba kujua dodoma mda wa Kufuturu saa ngapi niliko hata msikiti hakuna Iko mbali
Kuswali maswali najua majira yameingia
 
Assalam aleykum ndugu zangu katika iman...

Ndugu yenu naomba kujuzwa maana sahihi ya hii swala ya Tar-weeh pamoja na faida zake.
01. Sunnah iliyokokotezwa
Mlango kuhusu Tarawiyh kutoka katika "al-Mulakhasw al-Fiqh"


Miongoni mwa mambo aliyoweka katika Shari´ah Mtume wa uongofu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mwezi wa Ramadhaan ni swalah ya Tarawiyh. Ni Sunnah iliyokokotezwa. Imeitwa Tarawiyh(mapumziko) kwa sababu watu walikuwa wakipumzika ndani yake kati ya kila Rak´ah nne[1]. Kwa sababu walikuwa wakirefusha swalah.

Bora iswaliwe na kikosi cha watu msikitini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha Maswahabah zake msikitini nyusiku kadhaa. Kisha akaacha kufanya hivo kwa kuchelea isije kufaradhishwa juu yao. Hayo yamethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku mmoja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali msikitini na watu kadhaa wakaswali pamoja naye. Kisha akaswali siku ya kufuata na watu wakawa wengi. Kisha wakakusanyika katika usiku wa tatu au wa nne na hakuwatokea. Kulipopambazuka akasema: “Nimeona mlichokifanya. Hakuna kilichonizuia kukutokeeni isipokuwa mimi nilichelea isije kufaradhishwa juu yenu.”[2]

Wakati huo ilikuwa katika Ramadhaan. Ikaswaliwa na Maswahabah baada yake na ummah wakaipokea kwa mikono miwili.

[1] Kati ya kila Tasliym mbili. Kwa sababu swalah ya Tarawiyh ni Rak´ah mbilimbili na vivyo hivyo juu ya swalah ya Tahajjud. Wakati mwingine hukosea baadhi ya maimamu wa misikiti ambao hawana uelewa. Utawaona hawatoi salamu baina ya kila Rak´ah mbili katika Tarawiyh na Tahajjud, kitu ambacho kinakwenda kinyume na Sunnah.

Wanazuoni wamesema kuwa ambaye atasimama kwenye Rak´ah ya tatu katika Tarawiyh au katika Tahajjud ni kama ambaye anasimama katika Rak´ah ya tatu kwenye Fajr. Kwa msemo mwingine ni kwamba swalah yake inabatilika. Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz analo jawabu ambalo amewaraddi watu hawa na kubainisha kosa lao.

[2] al-Bukhaariy (1129) na Muslim (1780).

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/167-168)
Imechapishwa: 05/05/2021









02. Fadhilah za Tarawiyh​

Mlango kuhusu Tarawiyh kutoka katika "al-Mulakhasw al-Fiqh"




Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika mtu anaposwali na imamu mpaka akamaliza basi anaandikiwa amesimama usiku mzima.”[1]
“Ambaye atasimama Ramadhaan kwa imani na kwa matarajio, basi atasamehewa dhambi zake zilizotangulia.”
Kwa hiyo ni Sunnah iliyothibiti. Haitakikani kwa muislamu kuiacha.
[1] Abu Daawuud (1375), at-Tirmidhiy (805), an-Nasaa´iy (1363) na Ibn Maajah (1327).
  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/168)
  • Imechapishwa: 06/05/2021
 

4. Sababu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoendelea kuswali mkusanyiko​

Qiyaam Ramadhwaan - al-Albaaniy




[5] Sababu iliyomfanya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoendelea kuswali na wao mkusanyiko mwezi uliobaki, ilikuwa ni kuchelea swalah za nyusiku zisije kufaradhishwa kwao katika Ramadhaan. Hiki ni kitu wasingekiweza, kama ilivyotajwa katika Hadiyth ya ´Aaishah katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na Muslim na vyenginevyo[1]. Wasiwasi huu uliondoka kwa kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya Allaah kukamilisha Shari´ah na kwa ajili hiyo mtu alikuwa anaweza kurudi kuswali nyusiku za Ramadhaan kwa mkusanyiko. Hukumu ya asili ikawa imebaki, ambayo ni kuswali kwa mkusanyiko, na kwa ajili hiyo ndio maana ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akaihuisha, kama ilivyotajwa katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na vyenginevyo[2].
[1] Tazama “at-Taraawiyh”, uk. 12-14.
[2] Tazama takhriyj ya Hadiyth hii na maneno ya Ibn ´Abdil-Barr na wengineo juu yake katika marejeo yaliyotangulia, uk. 49-52.
  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qiyaam Ramadhwaan, uk. 21
  • Imechapishwa: 07/05/2019
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…