Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Yan nyie watu ni watata in nature, kwani lile tangazo limesema mpate afya njema ya mwili? limesema tu mpate afya njema, sasa wewe kwanini uwaze tangazo limemaanisha afya ya mwili na si roho? acha kuwa mtu wa negativity, maisha yenyewe mafupi haya.
 
Basi lalamikia huo wimbo ufungwe kwa sababu upo na unapigwa sana tena kipindi hiki karibu kila nyumba na kwenye daladala huku Tanga utausikia, clouds wamechukua shairi moja tu.
Nakushauri lawama zako upeleke kwenye taasisi husika sijui BASATA kama wanahusika na qaswida ili kuuangalia huo wimbo na sio hilo tangazo.
 
Kuna jingle(wimbo umekaa kama tangazo hivi) unatangazwa sana na kituo kimoja maarufu cha redio cha hapa jijini Dar es salaam....wenyewe wanajiita redio ya watu.. Lile tangazo kwa upande wangu nadhani linapotosha maudhui na dhumuni kubwa la mfungo wetu mtakatifu wa Ramadhan.. Tangazo linasema hivi kwa kifupi "........waislamu fungeni mpate afya njema...." kwa upande wangu dhumuni kubwa la mfungo sio kupata afya njema ya mwili, nadhani bora ingekua "kupata afya njema ya Roho".. Na kama kuna mwislamu anafunga ili kupata afya njema ya mwili atakua kakose japo hilo laweza kua ni lengo moja wapo lakini dhumuni kubwa ni Afya ya Roho, kwa kutenda mema, kusali sana na kuomba toba kwa Allah..

In short tangazo hilo lina boa na kubadili dhumuni kwa watu wanao lisikia hasa wale wa madhehebu mengine na waislamu kwa ujumla... Wadau mnasemaje..

Na wengi huwa wanapotoka kwa jumbe tata kama hizi. Toka lini kufunga kunampa mtu afya ya mwili?
 
SHEIKH ALBAANIY ALIPOIPATA SANADI YA DHIKRI HII ALILETA SIJDA YA KUSHUKURU


عن أنس -رضي الله عنه- قال: جاء أعرابي إلىٰ النبي ﷺ، فقال:-

kutoka kwa anas Allah amridhie amesema:
Alikuja Bedui kwa Mtume wa Allah akasema :

يا رسول الله علمني خيراً، فأخذ النبيﷺ بيده فقال :
Ewe mtume wa Allah Nifundishe Kheri ,
Mtume akamshika Mkono na akasema :

﴿قل: سُبْحَـانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ للهِ،
وَلَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ، وَاللهُ أَكْبَرُ،﴾.

Sema :
Subhaanallaah, Alhamdulillaah
Walaa ilaaha illa Allaah, Wallaahu Akbar


فعقد الأعرابي علىٰ يده، ومضىٰ وتفكَّر ثم رجع،
Akakunja Bedui mkono wake , Na akaenda, akatafakari kisha Akarejea,

فتبسم النبي ﷺ قال:
Mtume akatabasamu akasema :

﴿تفكر البائسُ﴾.
Amefikiri mwenye Haja

• فجاء فقال: يا رسول الله.!
Akaja [yule bedui] akasema: ewe mtume wa Allah !

سُبْحَـانَ اللهِ… وَالْحَمْدُ للهِ…
وَلَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ… وَاللهُ أَكْبَرُ…

Subhaana Allaah , Alhamdulillaah na Laa ilaha Illa Allaah , na Allahu akbar

هٰذا لله، فما لي.؟!
Hizi ni za Allah, ni zipi zangu ?!


• فقال له النبي ﷺ:
Mtume akamwambia:

﴿يا أعرابي إذا قلت:-
Ewe bedui utakaposema :-

سُبْحَـانَ اللهِ
قال الله: صدقت.
Subhaana Allah
Allaah husema : umesema kweli

وإذا قلت: وَالْحَمْدُ للهِ،
Na utakaposema : Alhamdulillah

قال الله: صدقت.
Allah husema umesema kweli

وإذا قلت: لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ،
Na utakaposema : Laa ilaha illah Allah
قال الله: صدقت،
Allah husema Umesema Kweli

وإذا قلت: الله أكبر،
Na utakaposema :Allahu akbaar

قال الله: صدقت،
Allah husema : Umesema kweli

وإذا قلت: «اللهم اغفر لي»،
Na Ukisema : Allahumma Ighfirliy ( ewe Allah nisamehe )

قال الله: قد فعلت،
Allah husema : Hakika nimefanya

وإذا قلت: «اللهم ارحمني»،
Na pindi unaposema : Allahumma irhamniy : ( Ewe Allah nirehem mimi )

قال الله: [قد] فعلت،
Allah husema : hakika Nimefanya

وإذا قلت: «اللهم ارزقني»،
Na unaposema : Allahumma Urzuqniy (ewe Allah nipe Rizki mimi )

قال الله: قد فعلت.﴾
Allah husema: hakika Nimefanya


⏮• فعقد الأعرابي علىٰ سبع في يده، ثم ولىٰ».
⏭ Akafumba bedui vidole vyake saba kisha akaondoka




قال العلامة المحدث/ محمد ناصر الدين الألباني -رحمه الله تعالىٰ-:
«أخرجه البيهقي في -شعب الإيمان-

Amesema Sheikh Albaaniy - Allah amrehem - imepokewa na imaam Al-Bayhaqiy katika Shuabul Iymaan

المصدر :
[سلسلة اﻷحديث الصحيحة
رقم: (3336)].
Silsilatul ahaadiythi Asw-Swahiyhah: nambari 3336.

_________________

NENO LANGU:

Ihifadhi Dhikri hii kwa ufupisho baada ya kuikusanya:


سُبْحَـانَ اللهِ وَالْحَمْدُ للهِ وَلَا إِلٰهَ إِلَّا اللهُ وَاللهُ أَكْبَر ُ اللهم اغفر لي اللهم ارحمني اللهم ارزقني.

Subhaana Allah wal-hamdulillah walaa ilaha illa Allah wallahu akbar Allahumma Ighfirliy warhamniy warzuqniy



Ni miongoni mwa Dhikri muhimu saana hio, Sheikh alivyoipata Hadith alileta Sijda ya kushukuru.
 
Kwa hakika masiku yaliyobaki ni machache. Kwa Jicho yakinifu watu wengi wamechoka, na hata idadi ya waswaliji imeanza kupungua. Basi Fahamuni kuwa huenda katika kumi hili na siku hizi zilizobaki mwisho wako ukawa mwema kwa kuupata ule Usiku wenye cheo. Hivyo jihimize umalize kwa nguvu kama ulivyoanza kwa nguvu. Ubora wa A'amal tunaungalia mwisho wake upoje. Ndio maana tunaambiwa kuna wale ambao huweza kufanya maovu maisha yao yote lakini Qadar ikamtangulia na akarejea kwa mola wake kwa matendo machache ya mwisho yenye ikhlaas na akawa ni katika watu wa peponi. Siku zilizobaki si haba, juzuu kumi unaweza kumaliza, Laylatul Qadr unaweza kuidiriki, Swadaka unaweza kuendelea kutoa. Jiombee zaidi dua na maghfira huku ukiuombea umma zaidi na zaidi upate kuongoka. Tushikane mkono kwa mkono kuitafuta pepo. Pepo ambayo jicho la bin-Adam na Majini hayajapatapo kuiona wala akili kufikiria uhalisia wake haijawahi kamwe. Pepo ambayo Jibreel alipooneshwa aliapa kwa Allaah kumuambia kuwa, hakuna yoyote atakaehadithiwa kuhusu mfanano wa pepo na mtu huyo akaacha kuingia Peponi. Pepo ipo chini ya utiifu, uchaMungu, kujitakasa na Rehma ya Allaah. Ewe Mola wetu, kwa Rehma yako tunakuomba pepo yako tukufu na utuepushe na adhabu ya moto.
 
Back
Top Bottom