Maelezo mazuri sana mkuu ila labda namimi nitie neno kwanza..
Bwana
Zurri hakutoa maana ya neno karimu كريم bali alitia hili na lile hakutoa maana.
Ila ndugu umefafanua vizuri lakini niseme kwamba kukataza jambo ambayo ni mubaha tu wala haliingii katika ibada basi inakuwa haifai kwa sababu ni kuharamisha aliyohalalisha Allah.
Neno karimu كريم ni kweli ni waznu wa فعيل kwa maana inakuwa kama ni kitenda hivi.
Lakini wakati huo huo neno hilo linaweza likawa na maana ya مفعول به (mtendwa).
Hasa pale ambapo neno hilo limetanguliwa na jina ambalo kiuhalisia HALITENDI BALI HUTENDWA.
Hivyo neno hili kulichambua peke yake kwa maana hiyo alafu ukasema haifai sio sawa sawa kwa sababu inakuja katika hali nyingi lakini kwa muktadha ule ule wa صيغة المبالغة ila inaweza kuja katika maana ya kuwa ni kilichoTENDWA.
Mfano wa maana ambazo zinaonyeshwa kwamba neno kariym كريم linaweza kuwa na maana ya مفعول (mtendwa,mfanyiwa)angalia aya za Allah...
قالت يا أيها الملأ إني ألقي إلي كتاب كريم
[ AN-NAML - 29 ]
(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.
Ukiangalia mwisho wa aya hapo neno KARIYM limetanguliwa na neno KITABU(jina)kwa maana ya hapo utafasiri kwamba kitabu ni MTENDA (فاعل)?
Hapo kitabu kinageuka kinakuwa ni mtendwa na kariym inageuka inakuwa ni mtendwa kwa maana ya hicho kitabu KIMEFANYWA KUWA KITUKUFU kwa msingi ule ule wa صيغة المبالغة (yaani kama kukitukuza kitu na kukipa ukubwa zaidi)
Aya nyingine...
أولم يروا إلى الأرض كم أنبتنا فيها من كل زوج كريم
[ ASH-SHUA'RAA - 7 ]
Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri?
Umeona neno kariym lina maana ipi hapo?
Wamefasiri maana ya uzuri yaani imefanywa kuwa nzurii.
وزروع ومقام كريم
[ ADDUKHAN - 26 ]
Na mimea na mahali pazuri
Hapo kariym inamfasiri huyo maqaam(mahali)kwa maana ya hapo neno KARIYM ni mtendwa ambaye anamuwakilisha SEHEMU kwa hvyo tafsiri ya neno kariym hapo ni kwamba SEHEMU ILIYOFANYWA KUWA NZURI na sehemu wala haiwezi kujifanya kuwa nzuri bali hufanywa.
Na aya nyingi zinaomyesha kwamba kariym anaweza akawa mtendwa..
إنه لقرآن كريم
[ AL -WAAQIA'H - 77 ]
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,
Hapo neno kariym limetanguliwa na neno QURANI kwa maana tafsiri yake ni "QURANI ILIYOFANYWA TUKUFU"
Kwa maana hiyo tunaweza kufupisha kwa kusema hivi.
"KARIYM IKITANGULIWA NA KITU AMBACHO HAKINA SIFA YA KUTENDA BASI NENO KARIYM LINAGEUKA LINAKUWA NI MTENDWA NA SIO MTENDA TENA".... Ndo mana hata aya zimetumia neno kariym kwa namna hiyo.
Hivyo mtu akisema "RAMADHAN KARIYM" maana yake ni ramadhani(mwezi)uliofanywa kuwa mtukufu" na wala haina maana ya kuwa eti huo mwezi ndo umetenda na kuwa mtenda.ukitafsiri hvyo maana yake mpaka aya tulizotoa zitatafsiriwa kwa makosa pia.
Na kiarabu ujanja wake wooooteee basi ikiwa kinaenda kinyume na Qurani twatakiwa tuifate Qurani imeweka msingi gani kwa sababu ndo marejeo.
Na hiyo Qurani ndo imetuonyesha kwamba neno KARIYM likitanguliwa na jina ambalo halitendi basi hilo jina hugeuka kuwa MTENDWAA..
Ramadhani kariym maana yake ni ramadhani iliyofanywa kuwa tukufu.
Zurri maana ya kariym usikariri kwa namna moja tu,huwa inakuwa na maana mbalimbali kwa mujibu wa kilichotangulia.
Neno Kareem كريم
limekuja katika uzani wa فعيل ambayo ina maana ya صيغة المبالغة na inaweza ikawa na maana ya صفة مشبهة
ama neno مبارك MUBAARAK
Limekuja katika uzani wa اسم المفعول
kwamaana ya Mtendwa( Iliyobarikiwa)
Kwamaana imefanyiwa kitendo cha Baraka
Allah anajua zaidi