Ramadhan Special Thread

Allah twakuomba utufikishe Ramadhan
Aamin ,huu mwezi una Rehema , Maghfira na baraka tele niliweka nia ya kuswali Seriazi karibu na mwezi huu miaka ya nyuma na mwezi ulipoingia nikakithirisha dua na Mwenyezi Mungu akajaalia tokea hapo nina miaka kibao nimefanikiwa kudumishwa swala yangu na kuiboresha

Na kila mwezi unapoisha najiona kama kuna upya fulani Ktk dini(chanya) umeongozeka kama siyo Ktk kuacha mazoea au kuongezea na kuboresha 'amali zangu njema

Nb:Tufunge kikweli kweli na tutumie fursa hii vizuri Ktk kuzidisha dua , kutubu , kuomba Maghfira na ibada mbalimbali kikubwa zaidi na dua na uhakika mabadiliko makubwa(chanya)yatajitokeza na kupanda daraja za kiimani inshaAllah.
 
Kabisa na hii inasadifu hikma ya swaumu kama alivyobainisha Allah subhaanahu wataa'la aliposema (لعلكم تتقون) - ili mpate kuwa wachamungu.

Kwa hakika swaumu ni katika sababu kuu za uchamungu, kwa sababu ndani yake kuna kufuata maamrisho ya Allah subhaanahu wataa'la, na kujiepusha na makatazo yake.
 
Aaante sana mpendwa, mfungo kwa mwaka huu unaanza lini na mimi nijiandae
 
Ramadhani iko njiani inakuja wakurungwa tujiandae kwa kununua mabox ya tambi na sukari
Pia tuziandae nafsi zetu, kwa kudhamiria kukithirisha kufanya ibada na kukithirisha kuomba maghfira(msamaha).
Katika mwezi huu uliojaa fadhila tele.

Kwani amesema mtume wa Allah (rehma na amani ziwe juuyake), katika mafhuumu ya hadhithi.

" Amekula hasara yule ambaye ataidiriki ramadhani kisha asisamehewe madhambi yake"
 
Leo Ijumaa ya mwisho ndani ya mwezi wa Sha'ban Mwenyezi akijaalia ijumaa ijayo itakuwa ndani ya Ramadan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…