Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

b238cd95a65a7e8f908ca315c54ce6c8.jpg
c4269dc73a74a751eb26ceab3384e2cb.jpg
 
Fanyeni yale mazuri yote tuliyoelekezana kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan
 
Akina dada ambao mmekengeuka kwa kuvaa mavazi yanayoacha wazi sehemu kubwa ya maumbile yenu embu oneni aibu mnayoyafanya sio kitu kizuri kabisa ,jistirini kama mlivyokuwa mnajistiri kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadan
 
Asalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,

Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote nawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.

Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.

Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu

Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.

Kwa haya machache napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.

Karibuni.

Mwezi mtukufu umepita sasa umerudi kwa kasi kwnye threads za kusifia uzinzi wa tunda, diamond na mobeto innalillah wa inna illaih rajiun
 
Back
Top Bottom