Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh,

Ndugu zangu zimebaki siku chache kabla ya ya kuudiriki mwezi wa Ramadhan In Shaa Allah.

Katika mwezi huu tunatambua fika ujira wa mwezi huu ni mkubwa kuliko katika miezi mingine, hivyo ni wajibu kwetu sisi kukumbushana katika kukimbilia kheri hizi kwani hakuna kitakachotufaa pindi tukiondoka kwenye dunia hii.

Naomba kukumbushia haya machache na mengine ndugu zangu hawa Kazakh destroyer ETUGRUL BEY Nurain Msonjo reymage watakazia name kuongeza mengi zaidi In Shaa Allah.

Swaum
Ni wajibu kwetu kufunga, na kufunga huku kusiwe ni kujizuia kula na kunywa tuu, laa, ila tujizuie kula na kunywa na kuacha yale yote tupaswayo kuyaacha kwa vile ambavyo Mwenyezi Mungu ametuamrisha mfano kusengenya, uzinzi, kuiba, dhana mbaya kwa wenzetu nk, na kufanya yale yote yenye kupelekea kuongezeka kwa ahmali zetu njema.

Swala

Tukumbuke pia kusimamisha swala tano tena kwa nyakati zake, ibada yoyote ni kulazumiana nayo ndipo allah anapoweka wepesi, wewe wa kuswali ramadhan mpaka ramadhan weka nia kabisa kuwa utaendelea na swala hata baada ya Ramadhani na Allah atafanya wepesi na malipo yatakuwa maradufu.

Taraweh
Tukumbuke kusimama kwa ajili ya swala ya Tarawee.

Quran
Tukithirishe kusoma Quran kwa wingi, mwenye juzuu moja alazimiane nayo hiyo hiyo na mwenye 30 naweza kusema kila siku juzuu moja na kidogo mpaka mwezi unaisha na msahafu unakuwa umeumaliza kwa idhini ya Allah.

Wanawake
Hapa nitoe nasaha kwa sisi wanawake, Ramadhani si mwezi wa kushinda jikoni kutwa nzima kupika hiki na kile, kwanza muda wa futari watu hawana hamu ya kula sana hivyo tujitahidi kuweka muda wa ibada uwe mrefu kuliko tunavoweka muda wa jikoni.

Wanaume
Nanyi mna jukumu kubwa kwa wake zenu, dada zenu na watoto wenu, waimize kufanya ibada na sio kukalia majiko, mpaka vipindi vya swala vinawapita na ibada zingine. Mtu hushindwa kusimama hata kwa ibada za usiku kwa kuwa siku nzima alikuwa busy na jiko (sikatai kuandaa lakini tujitahidi kupata wasaa wa ibada kwani ni neema kuwa miongoni mwa watakaoipata Ramadhani na bado hatujui kama neema hii itakuwa nasi katika mwaka mwingine).

Kufuturisha
Hili nalo kinapendeza, hata tende moja tayari unachuma thawabu za mwezi huu.

Allah atujaalie tuwe miongoni mwa wataka udiriki mwezi wa Ramadhani na atujaalie tuwe ni wenye kunufaika na ujira wa Ramadhani.
 
Back
Top Bottom