Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 873
- 3,307
- Thread starter
-
- #521
1. Hapana, hapo kila kimoja kina kazi yake...ukiweka vyote inakuwa bora zaidi ila ukishindwa kuweka vyote kutokana na hali ya uchumi, weka mkandaMkuu naomba kufahamu yafatayo;
1. Unapoweka Jamvi unakuwa huna haja ya kuweka mkanda?
2. Kipi naweza kuskip katika namna ya kupunguza gharama lakini nikawa nimelinda ubora ktk haya;
a/kuweka Jamvi
b/ kuweka mkanda
c/ kuweka lenta 2, nikaweka moja tu ile ya juu.
Shukrani Sana mkuu Kwa Ushauri wako huu mzuri, vipi kwasisi tunaotumia msingi wa mawe kipi kitafaa zaidi? Hapa umeshauri zaidi Kwa wanaoutumia msingi wa tofali. Asante sana1. Hapana, hapo kila kimoja kina kazi yake...ukiweka vyote inakuwa bora zaidi ila ukishindwa kuweka vyote kutokana na hali ya uchumi, weka mkanda
2. Inategemea na uimara wa tofali pamoja na aina ya udongo. Kuna tofali flani zilikuaga zinatumika sana miaka ya nyuma (zilikuwa zinatengenezwa kwa kutumia saruji, mchanga na vikokoto vidogo vidogo).
Enzi hizo gari la tofali likifika site, tofali zilikuwa zinamwagwa tu kama mchanga na hazivunjiki (baada ya hapo ndio zinaanza kupangwa)
Hizi tofali zilikuwa imara sana tofauti na hizi za sasa ambazo zinatengenezwa kibiashara zaidi (cement kidogo, mchanga mwingi). Watu wengi wakitumia hizi tofali kwenye msingi, huwa wanaskip kuweka mkanda kwa sababu uimara wake unakaribiana na uimara wa zege yenyewe, kama utatumia hizi tofali za kileo nakushauri uweke mkanda hata wa nondo 3 ili kujiweka salama zaidi
Upande wa kuweka jamvi, kama udongo wako uko vizuri na uchumi wako hauruhusu unaweza ukajaza kifusi chenye mawe mawe na kukishindilia vizuri, baada ya hapo ukamwaga zege nyembamba
Kiufupi ni muhimu sana kuweka mikanda yote miwili katika aina yoyote ya msingi utakayotumia, lakini ikiwa mfuko hauruhusu weka mkanda wa juu (hapa pia uwe tayari kwa matokeo). Chini ni heri ukajipinda ukaweka hata mkanda wa nondo 2 kuliko kutoweka kabisaShukrani Sana mkuu Kwa Ushauri wako huu mzuri, vipi kwasisi tunaotumia msingi wa mawe kipi kitafaa zaidi? Hapa umeshauri zaidi Kwa wanaoutumia msingi wa tofali. Asante sana
Gharama za ufundi huwa ni around 20% mpaka 25% ya gharama za material katika hatua husika. Mfano kama material ya upauaji gharama yake ni milion 4, basi ufundi ni kati ya laki 8 mpaka milion 1.Mkuu vipi kuhusu namna ya kukadria gharama ya ufundi hasa Kwa ujenzi wa msingi, Boma n.k ni namna gani hasa ya ukadiriaji wa gharama sahihi ambao utasaidia kuepusha upigaji wa mafundi??
Muda gani?baada ya kuapply tabaka la kwanza (first coat) inatakiwa iachwe kwa muda kabla ya kufuta na ubao (rati)
Dakika 20 mpaka 30 kutegemeana na hali ya hewa, kama kuna joto/jua utaiacha kwa dakika 20 lakini kama kuna baridi (hakuna jua) utaiacha kwa dakika 30Muda gani?