Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #541
Mkuu una madiniPLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Aina ya mchanga utakaoutumia katika shughuli za ujenzi unaweza ukachangia kuongezesha kwa gharama za ujenzi, mchanga wenye vumbi jingi sio mzuri katika ujenzi, unafanya saruji itumike kwa kiasi kikubwa kutengeneza muunganikano mzuri. Mchanga mzuri ni ule mchanga wa mtoni, ambapo vumbi huzama chini ya maji na kuacha punje punje za mchanga zikae juu
DPC inauzwa bei gani mkuuKabla ya kuanza kupandisha tofali za boma, ni vizuri ukatandika nailoni maalum (Damp proof course ,DPC) juu ya tofali za msingi(au mkanda kama umeweka) ambapo itasaidia kuzuia unyevu nyevu usiweze kupanda juu na kuathiri kuta za boma.
Roller nzima ni tsh 80,000/=DPC inauzwa bei gani mkuu
ShukraniRoller nzima ni tsh 80,000/=
Mita moja ni Tsh 2,500
Roller nzima inakuwa na urefu wa mita 50
Uwepo wa kemikali ama compounds zilizopo katika mchanga ndizo zinazofanya mchanga flani usifae katika matumizi ya ujenzi. Vitu kama chumvi n.k huathiri kwa kiasi kikubwa reaction kati ya cement na maji na kufanya udongo (mortar) usifikie kiwango cha ubora kilichokusudiwa.Kuna mtu alinambia mchanga wa mtoni haufai kumbe ni vice versa
Mkuu shukrani sana kwa Elimu....Uwepo wa kemikali ama compounds zilizopo katika mchanga ndizo zinazofanya mchanga flani usifae katika matumizi ya ujenzi. Vitu kama chumvi n.k huathiri kwa kiasi kikubwa reaction kati ya cement na maji na kufanya udongo (mortar) usifikie kiwango cha ubora kilichokusudiwa.
Ukiona udongo wako umeacha rangi rangi kama chaki ama chokaa baada ya kukauka, basi ujue mchanga wako au maji uliyoyatumia kuchanganyia vilikuwa havifai
Sawa ndg, tupo pamojaMkuu shukrani sana kwa Elimu....
Nimesave namba.
Vp kwa GAUGE 32 kwa ubora wa bati?Katika ujenzi, asilimia kubwa ya vifaa vya ujenzi vipo katika madaraja mfano kwenye bati kuna gauge 28, 30 na 32. Kwenye bomba kuna class A na class B, kwenye nondo pia kuna grade n.k
Usipokuwa makini, utauziwa kitu cha daraja la chini kwa bei ya kitu cha daraja la juu. Mshirikishe mtaalam katika hatua mbali mbali hasa hasa zile ambazo zinahitaji pesa nyingi ili usije ukaingia hasara
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Gauge 32 sikushauri ndg, ukishindwa kununua bati za gauge 28, nunua za gauge 30Vp kwa GAUGE 32 kwa ubora wa bati?
Asante.
KAZI ni kipimo cha UTU
Asante kwa ushauri mzuri!! Ila changamoto ni viwandani mteja kubambikiwa Gauge 32 baada ya 30 hapo kazi ipo kweli kweli mdau!!Gauge 32 sikushauri ndg, ukishindwa kununua bati za gauge 28, nunua za gauge 30
Hizi gauge 32 pamoja na bati za reject huwa zinatumika sana kujengea uzio katika site za ujenzi
Kila bati huwa kuna maandishi yanaandikwa, ikiwemo na hiyo gauge...kagua bati zote moja baada ya lingine hata kama zipo pc 200, usije ukakagua tu bati mbili za juu ukaridhikaAsante kwa ushauri mzuri!! Ila changamoto ni viwandani mteja kubambikiwa Gauge 32 baada ya 30 hapo kazi ipo kweli kweli mdau!!
KAZI ni kipimo cha UTU
Mkuu una roho nyeupe! Hongera sana kwa kuwa mtu wa kushare information na wananzengo.Kila bati huwa kuna maandishi yanaandikwa, ikiwemo na hiyo gauge...kagua bati zote moja baada ya lingine hata kama zipo pc 200, usije ukakagua tu bati mbili za juu ukaridhikaView attachment 3012848
Amina amina nashukuru ndg kwa dua yako, tupo pamoja na ubarikiwe pia. Nyie ndio maboss zangu, nawategemea mniunge mkono kijana wenuMkuu una roho nyeupe! Hongera sana kwa kuwa mtu wa kushare information na wananzengo.
Nimejifunza mengi. Hakika huu ni uzi bora nimekutana nao JF.
Utabarikiwa na ubarikiwe Zaidi kwenye kazi zako.