Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Katika ununuzi wa material ya mwanzo kabisa kwa ajili ya kuanza ujenzi, usisahau kupitia pharmacy kununua na kisanduku cha vifaa vya huduma ya kwanza (first aid kit).

Ni muhimu sana, kwa sababu mtu atakapopata tatizo mfano kukatwa na bati, kutobolewa na nondo au msumari n.k anaweza akapoteza maisha kwa kukosa huduma ya kwanza kutokana na kupoteza damu nyingi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Mkuu una madini
 
Aina ya mchanga utakaoutumia katika shughuli za ujenzi unaweza ukachangia kuongezesha kwa gharama za ujenzi, mchanga wenye vumbi jingi sio mzuri katika ujenzi, unafanya saruji itumike kwa kiasi kikubwa kutengeneza muunganikano mzuri. Mchanga mzuri ni ule mchanga wa mtoni, ambapo vumbi huzama chini ya maji na kuacha punje punje za mchanga zikae juu

Kuna mtu alinambia mchanga wa mtoni haufai kumbe ni vice versa
 
Kabla ya kuanza kupandisha tofali za boma, ni vizuri ukatandika nailoni maalum (Damp proof course ,DPC) juu ya tofali za msingi(au mkanda kama umeweka) ambapo itasaidia kuzuia unyevu nyevu usiweze kupanda juu na kuathiri kuta za boma.
DPC inauzwa bei gani mkuu
 
Kuna mtu alinambia mchanga wa mtoni haufai kumbe ni vice versa
Uwepo wa kemikali ama compounds zilizopo katika mchanga ndizo zinazofanya mchanga flani usifae katika matumizi ya ujenzi. Vitu kama chumvi n.k huathiri kwa kiasi kikubwa reaction kati ya cement na maji na kufanya udongo (mortar) usifikie kiwango cha ubora kilichokusudiwa.

Ukiona udongo wako umeacha rangi rangi kama chaki ama chokaa baada ya kukauka, basi ujue mchanga wako au maji uliyoyatumia kuchanganyia vilikuwa havifai
 
Mkuu shukrani sana kwa Elimu....
Nimesave namba.
 
Katika ujenzi, asilimia kubwa ya vifaa vya ujenzi vipo katika madaraja mfano kwenye bati kuna gauge 28, 30 na 32. Kwenye bomba kuna class A na class B, kwenye nondo pia kuna grade n.k

Usipokuwa makini, utauziwa kitu cha daraja la chini kwa bei ya kitu cha daraja la juu. Mshirikishe mtaalam katika hatua mbali mbali hasa hasa zile ambazo zinahitaji pesa nyingi ili usije ukaingia hasara

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Wauza viwanja wengi wanapenda kutumia kizio cha futi badala ya kizio cha mita ili kiwanja kionekane ni kikubwa

Mfano kiwanja cha futi 40 kwa futi 50 ambavyo ndio vingi sana huko wanapokata viwanja ni sawa na kiwanja cha mita 12 kwa mita 15.

Upande wa mita 12 ukitoa mita moja kulia na kushoto, unabaki na mita 10 (hapa itakulazimu nyumba uibane bane ili itoshee)

Kama utakuta viwanja vinauzwa kwa vipimo vya futi, basi nunua angalau kiwanja cha futi 50 kwa futi 60 na kuendelea ambacho ni sawa na mita 15 kwa mita 18 ili ubaki hata na eneo la parking/bustani mbele, ukishindwa kabisa nunua kiwanja cha futi 50 kwa futi 50 ambacho ni sawa na mita 15 kwa mita 15

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi, asilimia kubwa ya vifaa vya ujenzi vipo katika madaraja mfano kwenye bati kuna gauge 28, 30 na 32. Kwenye bomba kuna class A na class B, kwenye nondo pia kuna grade n.k

Usipokuwa makini, utauziwa kitu cha daraja la chini kwa bei ya kitu cha daraja la juu. Mshirikishe mtaalam katika hatua mbali mbali hasa hasa zile ambazo zinahitaji pesa nyingi ili usije ukaingia hasara

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Vp kwa GAUGE 32 kwa ubora wa bati?
Asante.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Gauge 32 sikushauri ndg, ukishindwa kununua bati za gauge 28, nunua za gauge 30

Hizi gauge 32 pamoja na bati za reject huwa zinatumika sana kujengea uzio katika site za ujenzi
Asante kwa ushauri mzuri!! Ila changamoto ni viwandani mteja kubambikiwa Gauge 32 baada ya 30 hapo kazi ipo kweli kweli mdau!!

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Asante kwa ushauri mzuri!! Ila changamoto ni viwandani mteja kubambikiwa Gauge 32 baada ya 30 hapo kazi ipo kweli kweli mdau!!

KAZI ni kipimo cha UTU
Kila bati huwa kuna maandishi yanaandikwa, ikiwemo na hiyo gauge...kagua bati zote moja baada ya lingine hata kama zipo pc 200, usije ukakagua tu bati mbili za juu ukaridhika
FB_IMG_1706864093518.jpg
 
Kila bati huwa kuna maandishi yanaandikwa, ikiwemo na hiyo gauge...kagua bati zote moja baada ya lingine hata kama zipo pc 200, usije ukakagua tu bati mbili za juu ukaridhikaView attachment 3012848
Mkuu una roho nyeupe! Hongera sana kwa kuwa mtu wa kushare information na wananzengo.
Nimejifunza mengi. Hakika huu ni uzi bora nimekutana nao JF.
Utabarikiwa na ubarikiwe Zaidi kwenye kazi zako.
 
Mkuu una roho nyeupe! Hongera sana kwa kuwa mtu wa kushare information na wananzengo.
Nimejifunza mengi. Hakika huu ni uzi bora nimekutana nao JF.
Utabarikiwa na ubarikiwe Zaidi kwenye kazi zako.
Amina amina nashukuru ndg kwa dua yako, tupo pamoja na ubarikiwe pia. Nyie ndio maboss zangu, nawategemea mniunge mkono kijana wenu
 
Je wajua ni kwanini vyoo vinatakiwa vikae upande wa kusini?

Upande wa kusini ndio upande ambao unapokea joto kwa kiasi kikubwa katika masaa yote 12, sasa kwa kuwa chooni ni mahali ambapo mtu hakai sana kama ilivyo sebleni, chumbani ama jikoni basi ndio maana vyoo vinatakiwa viwekwe upande huu.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom