Elon Mzebuluni
JF-Expert Member
- Jan 22, 2016
- 226
- 146
Mkuu generally roof inakuwa rated kwenye area, sasa ukitaka kujua ni bati ngapi au vigae vingapi utatumia inategemea na dimensions za bati utakazo chagua kutoka kwa manufacturer. kwa mfano kwenye picha hapo chini ukichagua bati la picha namba:Nimeona kiongozi na ramanj ya roof iko hivyo hivyo . Nilichokuwa naomba ni idadi ya bati zinazotosha kufunika hilo Banda. Na nashukuru kwa ushauri wa kuweka kozi nne baada ya Renta
Ubarikiwe sana kiongozi picha namba nne ni nzuri zaidi.umekata kiu yangu Mungu akutangulie katika majukumu yako.Mkuu generally roof inakuwa rated kwenye area, sasa ukitaka kujua ni bati ngapi au vigae vingapi utatumia inategemea na dimensions za bati utakazo chagua kutoka kwa manufacturer. kwa mfano kwenye picha hapo chini ukichagua bati la picha namba:
Picha namba moja
Chukua Upana wa bati baada ya kuezeka = 0.762m
Mfano Urefu wa bati = 3m
Area ya bati = 0.762x3= 2.286m²
Idadi ya bati = Area ya roof ÷ Area ya bati
= 165.2÷2.286
= 72.3 ~ 73
Bati 73
Ukienda kwa hesabu hiyo juu utapata
Picha namba mbili = bati 68
Picha namba tatu = bati 55
Picha namba nne= bati 61
View attachment 3019898
Barikiwa sana kakaMkuu generally roof inakuwa rated kwenye area, sasa ukitaka kujua ni bati ngapi au vigae vingapi utatumia inategemea na dimensions za bati utakazo chagua kutoka kwa manufacturer. kwa mfano kwenye picha hapo chini ukichagua bati la picha namba:
Picha namba moja
Chukua Upana wa bati baada ya kuezeka = 0.762m
Mfano Urefu wa bati = 3m
Area ya bati = 0.762x3= 2.286m²
Idadi ya bati = Area ya roof ÷ Area ya bati
= 165.2÷2.286
= 72.3 ~ 73
Bati 73
Ukienda kwa hesabu hiyo juu utapata
Picha namba mbili = bati 68
Picha namba tatu = bati 55
Picha namba nne= bati 61
View attachment 3019898
Aiseee vzr sana, leo umenipa elim7 nyingine.... Mimi ni mechanical engineer, huwa nafanya plumbing(sewage and clean water) , lakin majengo mengi ambayo nimefanya design, nilikuwa naweka maji ya jikon direct kwenye septic, although nilikuwa najenga septic and soak
Mkuu acha uongo mechanical eng.hafanyi hizo kazi labda wewe ni environmental eng.Aiseee vzr sana, leo umenipa elim7 nyingine.... Mimi ni mechanical engineer, huwa nafanya plumbing(sewage and clean water) , lakin majengo mengi ambayo nimefanya design, nilikuwa naweka maji ya jikon direct kwenye septic, although nilikuwa najenga septic and soak away kwa pamojaa...
away kwa pamojaa...
hizi dawa wanasema hamna kituIli kuepuka mbao zako kuliwa na wadudu wa mbao, hakikisha mbao zote utakazotumia katika upigiliaji wa dari, upauaji n.k ziwe ni mbao za dawa, kama utakuwa na mashaka na dawa iliyotumika unaweza ukanunua dudu killer ukapaka kwenye mbao zako
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Ni kweli, siku hizi biashara nyingi zimekuwa na usanii mwingi, yote hayo ni katika tamaa ya kumaximize profit.hizi dawa wanasema hamna kitu
Mkuu heshima kwako.Kubali kuingia gharama zaidi ili kupata msingi imara. Msingi ukiwa imara, jengo litadumu muda mrefu bila kuleta shida yoyote.
(i) Tumia tofali imara, ukipata tofali zilizowekwa vikokoto itakuwa bora zaidi
(ii) Usiunge kuta mbili ambazo zinatofautiana vina (depth), tumia nguzo za zege na ringi zake weka karibu karibu kuongeza uimara
(iii) Jaza kifusi chenye mawe mawe, usitumie kifusi cha udongo wa mfinyazi
(iv) Hakikisha visiki vyote unavitoa kwa kuving'oa na sio kuvikata
(v) Usitumie maji ya chumvi katika ujenzi, maji utakayotumia katika ujenzi yawe ni maji ambayo mtu anaweza kuyanywa
(vi) Itaendelea....
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
1. Kwa upande wa nguzo, nondo za milimita 16 ndio minimum size (kima cha chini)...inatakiwa utumie nondo za milimita 16 na kuendelea, nguzo ndio kama miguu ya jengo lenyeweMkuu heshima kwako.
1. Slab ya 31.5msq kuna haja ya kuweka nguzo za nondo ya 16mm? Inabeba chumba kimoja kikubwa cha kulala tu
2. Naomba kujua idadi ya nondo na saruji kuweka slab ya 31.5msq (4.5X7)
Asante sana mtalaamu1. Kwa upande wa nguzo, nondo za milimita 16 ndio minimum size (kima cha chini)...inatakiwa utumie nondo za milimita 16 na kuendelea, nguzo ndio kama miguu ya jengo lenyewe
Mfano tukipiga hesabu ya uzito wa hiyo slab pekee, uzito wake ni 7mX4.5mX0.125mX2400Kg/m³ = 9450Kg sawa na tani 9.45 (na hii ni uzito wa zege tu peke yake, hatujapigia hesabu uzito wa nondo zake)
Huo uzito sasa ndio unajigawa katika nguzo zote (japo asilimia chache ya uzito utabebwa na kuta)
Daaah, safi sanaUkichukua marine board moja ukaichana vipande vya 20cm, utapata vipande 6 vya futi nane nane.
Marine board moja ya milimita 12, bei yake ni kati ya 40,000 mpaka 45,000. Mashineni kuchana njia moja ni Tsh 200/=, Tsh 200 x njia 5 = Tsh 1,000 (Jumla 46,000/=)
(Unaweza ukanunua na mbao 2 za 2x2 ukapigilia vipande sehemu ambazo utakuwa unafunga kabali zako)
Mbao moja ya upana unaofanana na hivyo vipande vya marine board ulivyovikata (20cm sawa na 1x8 ya futi 12) inauzwa +/-13,000/= kwa hivyo 13,000x6 jumla ni sawa na 78,000/=
Tofauti 78,000 - 46,000 = 32,000/= (Saved)
Kama ni kwa matumizi ya mkanda (beam), mbao sita zitacover mita 10.8, marine moja itacover mita 7.2
Mbali na hizo njia mbili hapo juu, option nyingine ambayo ni nafuu ni kukodi mbao zilizotumika ambapo kukodi mbao moja ni kati ya 1,500 mpaka 2,000 (2000x6=12,000/=). Kawaida muda wa matumizi huwa wanatoa siku 3, kwahivyo mfano ukikodi jumamosi, jumanne asubuhi inatakiwa urudishe
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Nina ujenzi kijijini, nikanunua vigae mjini kama km 300 hivi bila kufanya utafiti wa nauli. Kuja kusafirisha najikuta naingia gharama kubwa na muda bora ningenunua kulekule tu.Kabla ya kufanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi, pendelea kuulizia bei ya vitu tofauti tofauti sehemu mbali mbali
Wakati mwingine unakuta kuna utofauti wa bei kwa zaidi ya Tsh 1000 na zaidi kwa kila bidhaa, ambapo kama idadi ya bidhaa utakazonunua itakuwa kubwa utajikuta umepoteza elfu moja nyingi ambazo ungeweza kufanyia manunuzi ya vifaa vingine na kupunguza gharama za ujenzi.
Ukishafanya hili zoezi utakuwa unajua duka no 1 utakuwa unanunua bidhaa flani mfano misumari na mbao, duka no 2 utakuwa unanunua labda tofali na cement, duka no 3 utakuwa unanunua nondo n.k kutokana na bei ulizozifanyia utafiti hapo kabla
Mfano unaweza ukakuta duka moja wanauza misumari Tsh 3000/kg lakini duka lingine wanauza Tsh 4000/kg.
Kama hukufanya research ya bei za vitu, huu utofauti wa bei utakuja kuugundua siku ambayo umeenda duka ulilozoea kununua lakini ukakuta wamefunga au wamechelewa kufungua na kuamua kwenda kununua bidhaa duka lingine (kama ndio unamalizia ujenzi, utajilaumu sana kwa kutogundua hili suala mapema)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
300Km ni nyingi mkuu, hata kama kungekuwa na upungufu wa Tsh 100,000/= ni bora tu ungenunulia huko huko ulipo maana kusafirisha hivyo vigae kwa huo umbali unaweza ukafika site ukakuta vigae vilivyovunjika hasara yake inazidi hiyo pesa uliyoisave, ukajikuta unaingia hasara zaidiNina ujenzi kijijini, nikanunua vigae mjini kama km 300 hivi bila kufanya utafiti wa nauli. Kuja kusafirisha najikuta naingia gharama kubwa na muda bora ningenunua kulekule tu.
Utafiti wa bei na associated costs ni muhimu