Hizi wanapiga Bongo?
PLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Vent ni muhimu zikiwekwa vizuri zinapooza joto darini na kuzuia nyumba kupasuka, ila huwa sielewi pale wayu wanaweka vioo badala ya wavuRekebisha hizo vent za huko kwenye paa, hazina kazi yoyote zaidi ya kuozesha ceiling board
Upo sahihi kabisa, majuzi nimemchukua fundi Dar baada ya kuona kazi zake mtandaoni akanifanyie kazi Mikumi, najuta nimepoteza frdha yangu, ila nadhani wengi wao wanapiga picha kazi za watu wengine na kujinasibu kuwa ni kazi zaoPoint to Note:
Usihadaike na picha za mitandaoni, ni afadhali ukatembea tembea mwenyewe mitaani kutafuta mafundi wazuri ili usije ukaingia hasara, ujenzi ni mara moja tu, ukikosea maana yake ni aidha urudie au ukubaliane na uhalisia
Umakini mkubwa unahitajika katika uchaguzi wa mafundi, maana wakiharibu unakuwa umepata hasara mara mbili (pesa uliyomlipa fundi wa awali, pesa ya kuja kurudia tena/kukarabati na pesa ya kununua material mengine)Upo sahihi kabisa, majuzi nimemchukua fundi Dar baada ya kuona kazi zake mtandaoni akanifanyie kazi Mikumi, najuta nimepoteza frdha yangu, ila nadhani wengi wao wanapiga picha kazi za watu wengine na kujinasibu kuwa ni kazi zao
Hivi kufunga mkanda kabla ya kuanza dirisha pale kati kati ina madhara gani? Msingi haujafungwa mkandaUmakini mkubwa unahitajika katika uchaguzi wa mafundi, maana wakiharibu unakuwa umepata hasara mara mbili (pesa uliyomlipa fundi wa awali, pesa ya kuja kurudia tena/kukarabati na pesa ya kununua material mengine)
Mkanda wa kati kazi yake ni kuzuia zile nyufa zinazojitokeza chini ya madirisha zisitokee kwa hivyo inaongeza uimara zaidiHivi kufunga mkanda kabla ya kuanza dirisha pale kati kati ina madhara gani? Msingi haujafungwa mkanda
Kwa sasa hao ndio wengi hasa wanapiga picha nyumba kazi z mafundi wengine wanasema ni wao. Kumbe ni takataka TU.Umakini mkubwa unahitajika katika uchaguzi wa mafundi, maana wakiharibu unakuwa umepata hasara mara mbili (pesa uliyomlipa fundi wa awali, pesa ya kuja kurudia tena/kukarabati na pesa ya kununua material mengine)
Mkuu Henchy Essy nikupe pongezi kwa elimu unayoitoa humu ndani.Wakati mwingine mtu unaweza ukahadaika na picha za kazi wanazotumia mafundi kujitangazia mitandaoni, sasa changamoto inakuja pale unapowapa kazi hao mafundi. Unabaki unajiuliza mbona walichokifanya ni tofauti kabisa na jinsi wanavyojitangaza mitandaoni!!!?
Sasa nakuibia siri, mafundi wengine huwa wanaiba picha za watu na kuzitumia hizo picha kujitangazia huko mitandaoni.
Yupo jamaa yangu mmoja, alijengewa na mafundi aliowaamini sana uwezo wao kupitia picha zao za mitandaoni (kipindi hicho alikuwa anamtumia mdogo wake kuwasimamia hao mafundi) na sasa hivi anafikiria kulivunja boma lake aanze upya baada ya kufika site na kujionea yaliyofanyika
Mitaani kuna mafundi wazuri sana lakini ndio hivyo wako mbali sana na dunia, hawana hata habari na hii mitandao. Sasa mtu akipita site akaona kazi nzuri inavutia, ndio kama hivyo anapiga picha kiwizi wizi halafu anazitumia huko mitandaoni (Fundi aliyefanya hiyo kazi hana hata habari na hata hiyo simu kubwa hana, atajuaje kama kazi zake zinatumiwa na watu wengine kujitangaza?)
Point to Note:
Usihadaike na picha za mitandaoni, ni afadhali ukatembea tembea mwenyewe mitaani kutafuta mafundi wazuri ili usije ukaingia hasara, ujenzi ni mara moja tu, ukikosea maana yake ni aidha urudie au ukubaliane na uhalisia
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
1. Ndio, hapo haina shida. Ukitumia nguzo za tofali inabidi tofali zake uzilaze lakini pia usijenge tofali nzima nzima tupu, inatakiwa zifatane tofali nzima, then tofali za vipande mpaka juuMkuu Henchy Essy nikupe pongezi kwa elimu unayoitoa humu ndani.
Katika pita zangu mtandaoni nilikutana na nyumba hiyo hapo, kwa ujuzi na uzoefu wako ninaomba unitoe tongo tongo juu ya haya maswali yangu.
1, Je hizo nguzo mbili (Upande wa kushoto), zilizojengwa kwa tofali bila nondo wala zege ni imara na madhubuti kweli?
2. Kama hizo nguzo mbili ni imara na madhubuti, ikiwa nitajenga nguzo nne (Mbili kushoto na mbili kulia), na kila nguzo moja nikajenga kwa kutumia vipande vya nusu tofali (Kwenye picha zimetumika tofali nzima) na juu ya hizo nguzo nikamwaga zege la lenta, je nguzo hizo zitakuwa na uimara na uthabiti wa kuweza kubeba Gable la nyumba?.
Naomba nitangulize shukrani.View attachment 3095509
Hapo kwanza inatakiwa umwagwe mchanga wa kutosha baada ya kuchimba msingi, lakini pia wakati wa kujaza kifusi usiurudishie ule udongo uliochimba kwenye msingi (tafuta udongo mwingine wenye asili ya kichanga uutumie kama kifusi na umwagie maji ya kutosha ili udongo ujishindilie chini)Kwa ardhi kama hii inachanika wakati wa jua na kukaza wakati wa mvua unafanyaje kujiepusha na nyufa
Rafki yangu kajenga ila nyumba inapiga nyufa vibaya mno kaziba mpaka kachoka
View attachment 3104381