Nzagambaaa
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 1,135
- 1,826
Achana nae, Mwenye kipato hanaga zarau za kishamba hizi....hii kenge Moja tu inasubili ugari kwa Shemeji yake.Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
Inasaidia ardhi kupumua kutokana na joto kali lililopo chini, usipoweka hayo matundu ardhi itashindwa kupumua na kufanya ukuta usukumwe na udongo ambapo itasababisha nyufa katika kuta za msingi.Mtaalamu hayo matundu yanasaidia nini?
Yasipowekwa itatokea shida gani ktk msingi au nyumba
Nashukuru ndugu kwa appreciation, ujenzi sio mgumu kama utaamua kujenga kwa awamu tofauti na kusubiri mpaka pesa yote itimie.Jamiiforums ni msaada mkubwa sana kwenye ulimwengu wa leo unaohitaji akili na matumizi sahihi ya pesa,post za mdau Hechy Essy zimenifungua akili kama hivi alivyoandika ningevijua mapema vingenisaidia sana.
Kwenye ujenzi tusiogope kutumia washauri kisa kukimbia gharama mimi sikuwa na akili hii majibu yake nimeshayaona,kwa mnaoanza ujenzi tafadhalini watumieni watu kama hawa watawasaidia sana.
Shukrani sana kwa ufafanuzi mkuu.Nashukuru ndugu kwa appreciation, ujenzi sio mgumu kama utaamua kujenga kwa awamu tofauti na kusubiri mpaka pesa yote itimie.
Unaweza ukaweka malengo ya miezi miwili miwili, mitatu mitatu n.k mfano mwezi januari mpaka machi ukajiwekea malengo ya kujenga msingi, mwezi april mpaka june ukainua boma, mwezi july mpaka septemba ukapaua n.k. ndani ya miaka miwili au mitatu unakuwa tayari umeshamaliza na kuhamia.
Katika hizo intervals za muda unakuwa na kazi ya kukusanya pesa kwa ajili ya hatua/malengo yanayofuata
Kama hutojali, unijibu maswali yafuatayo:PLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Samahani ndg kwa kuchelewa kujibu, shida ipo kwenye app ya JF upande wa notification hivyo inanifanya niwe nakuja kuchungulia comment kila mudaKama hutojali, unijibu maswali yafuatayo:
1. Unapatikana wapi?
2. Unaweza kwenda mikoani? Kama jibu ni ndiyo, gharama yake ni sh ngapi nje na malipo ya kazi? Site ipo Arusha.
3. Ikiwa mtu anataka kuiboresha nyumba iliyokamilika kwa kubadili muundo wake, unaweza kuifanya hiyo kazi kwa kusaidia katika ushauri na pia kuichora ramani yake upya? Itakuchukua siku ngapi kukamilisha mchoro wake?
Asante.
Safi sana kiongozi , nikiwa Moshi ufundi nilisoma Plumbing , nilifundishwa kuwa hata system ya choo na bafu havitakiwi kuwa na same path(destination) sababu , ya hao bacteria (anaerobes bacteria) ambao ndio huvunja vunja uchafu.Kitaalam haishauriwi maji ya jikoni (kuoshea vyombo n.k) kwenda ktk shimo la choo kwa sababu maji ya jikoni yana mafuta ambayo hutengeneza tabaka juu ya maji na kuzuia hewa isiingie chini. Umeng'enyaji wa uchafu uliopo ktk shimo la choo hufanywa na bacteria ambao hao bacteria wanahitaji hewa ili waendelee kuishi.
Utakapomwaga maji ya jikoni kwenye karo la choo, lile tabaka la mafuta litafanya bacteria wakose hewa na kupelekea kufa hivyo karo litakuwa linajaa haraka (mara kwa mara) kutokana na kwamba umeng'enyaji wa uchafu haufanyiki au unafanyika kwa kiasi kidogo kutokana na uchache wa hewa na bacteria uliopo chini.
Vinginevyo itabidi ujenzi wa septic tank (lile shimo la pembe nne) uweke buffer wall kati kati (Mechanism ya Buffer wall nitaielezea siku nyingine, subscribe huu uzi uendelee kupata dondoo mbali mbali kuhusu ujenzi)
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali +255(0)624068809
Kabisa kabisa, hiyo ni kwa sababu ya zile kemikali za sabuni, body wash n.k....maji ya bafuni inatakiwa yaelekezwe moja kwa moja ktk shimo la duara (soak way pit) bila kupitia ktk shimo la mstatili (septic tank)Safi sana kiongozi , nikiwa Moshi ufundi nilisoma Plumbing , nilifundishwa kuwa hata system ya choo na bafu havitakiwi kuwa na same path(destination) sababu , ya hao bacteria (anaerobes bacteria) ambao ndio huvunja vunja uchafu.
Aiseee vzr sana, leo umenipa elim7 nyingine.... Mimi ni mechanical engineer, huwa nafanya plumbing(sewage and clean water) , lakin majengo mengi ambayo nimefanya design, nilikuwa naweka maji ya jikon direct kwenye septic, although nilikuwa najenga septic and soak away kwa pamojaa...Kitaalam haishauriwi maji ya jikoni (kuoshea vyombo n.k) kwenda ktk shimo la choo kwa sababu maji ya jikoni yana mafuta ambayo hutengeneza tabaka juu ya maji na kuzuia hewa isiingie chini. Umeng'enyaji wa uchafu uliopo ktk shimo la choo hufanywa na bacteria ambao hao bacteria wanahitaji hewa ili waendelee kuishi.
Utakapomwaga maji ya jikoni kwenye karo la choo, lile tabaka la mafuta litafanya bacteria wakose hewa na kupelekea kufa hivyo karo litakuwa linajaa haraka (mara kwa mara) kutokana na kwamba umeng'enyaji wa uchafu haufanyiki au unafanyika kwa kiasi kidogo kutokana na uchache wa hewa na bacteria uliopo chini.
Vinginevyo itabidi ujenzi wa septic tank (lile shimo la pembe nne) uweke buffer wall kati kati (Mechanism ya Buffer wall nitaielezea siku nyingine, subscribe huu uzi uendelee kupata dondoo mbali mbali kuhusu ujenzi)
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali +255(0)624068809
Sabbu hapo wanaogopa back pressure inaweza kurudi kwenye pipe za maji ya kuogea na kuanza kutoa harafuSafi sana kiongozi , nikiwa Moshi ufundi nilisoma Plumbing , nilifundishwa kuwa hata system ya choo na bafu havitakiwi kuwa na same path(destination) sababu , ya hao bacteria (anaerobes bacteria) ambao ndio huvunja vunja uchafu.
Umemjibu vema.Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
Tupo pamoja ndg yanguUmemjibu vema.
Asante sana kwa elimu unayoitoa na kwa uungwana wako.
Tukitoka ya hii ya vyumba viwili tuone na ya vyumba vitatuPLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
I appreciate what you are giving. It is beneficial and eye opener. Mimi nina opinion na pia nina swali if you won't mind. Opinion yangu ni kuhusu utoaji wako wa elimu. Elimu ni nzuri sana, kama itawezekana uongezee hata na simple sketch (illustrations) kutoa mwanga zaidi kwa point husika.Ni ngumu sana kuviunganisha pamoja vitu viwili vyenye tabia tofauti mfano katika ule mfereji wa maji katika nyumba za paa la kuficha mafundi wengi wanamwaga zege kwenye ile slab ya mtaro, halafu kuta za mfereji wanazijenga kwa tofali.
Ikumbukwe kuwa kila material ina thermal expansitivity value yake, hivyo joto linapoongezeka au kupungua kila material itatanuka/kusinyaa kwa kiasi chake kutokana mabadiliko ya hilo joto. Kiasi cha utanukaji/kusinyaa itategemea na hiyo value yake ya thermal coefficient
Utofauti wa hizi values ndio unaofanya materials zilizounganishwa pamoja kuachana na kuleta nyufa ktk maungio kwa sababu kila kimoja kitatanuka/kusinyaa kwa namna yake
Ni vizuri ukatumia material ya aina moja au materials ambazo values zake angalau zinakaribiana sana ili kufanya huo muunganiko wa vitu viwili kutanuka na kusinyaa kwa pamoja pale kunapotokea mabadiliko ya joto.
Kwenye ule mfereji, ni vizuri ukatumia zege pote (yaani ile slab na kuta zake za pembeni) lakini kama ukishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ya kiuchumi basi unashauriwa baada ya kumwaga ile slab ya mfereji, pandisha ukuta mfupi wa zege hata wa sentimita 15 mpaka 20 halafu juu ndipo ulaze tofali , lengo ni kuepuka nyufa zinazojitokeza kwenye zile kona za mfereji (pale kwenye maungio ya slab na kuta za mfereji) kutokana na utofauti wa hizo thermal coefficient values.
Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali
Huu mfumo unahitaji umakini sana, mimi binafsi napembelea mfumo wa contemporary ambao mfereji wake unazungukia nje kama ilivyo pvc gutter. Upauaji unakuwa wa kawaida (angle ndogo) ila bati linakuwa halionekani na mzunguko wa bati wote unadondoshea maji kwenye huo mfereji (hakuna kuchimbia bati kwenye ukuta)I appreciate what you are giving. It is beneficial and eye opener. Mimi nina opinion na pia nina swali if you won't mind. Opinion yangu ni kuhusu utoaji wako wa elimu. Elimu ni nzuri sana, kama itawezekana uongezee hata na simple sketch (illustrations) kutoa mwanga zaidi kwa point husika.
Swali langu ni kuhusu hii style mpya ya kuweka paa. Nimesikia mara nyingi sana kuna tatizo la maji kuvuja. Nawaza ni namna gani in a nutshell kuavoid hii changamoto?
Asante