Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Somo zuri sana la elimu ya fedha na matumizi.
 
Nami ningependa kujua haya mawe yanaongeza nini maana naona si kila project inatandika mawe kabla ya kumwaga zege. Labda mwenye uzoefu wa miradi ya serikali anaweza kutujuza. Mawe ni lazima au hapana?
Mawe yanatumika kwa ajili ya kuongeza uimara wa msingi/floor katika jengo. Wengi huwa wanakwepa kwa sababu ya gharama, lakini ukiweka inakuwa vizuri zaidi. Kama uchumi hauruhusu weka tu kifusi lakini ukishindilie vizuri kwa matabaka kuanzia chini mpaka kufikia level inayohitajika.

Kwa majengo kama mashule, mahospitali n.k mawe ni lazima na ni muhimu sana kwa sababu ni majengo ambayo yana muingiliano wa watu wengi na pia yanatumika kwa muda mrefu (yapo majengo yana miaka zaidi ya 50 na bado yanaendelea kutumika kwa sababu ya msingi imara)
 
Vipi nimije ga kozi hiyo ya mwisho ya msingi na tofali hizo za mchnaga na kokoto...hapo sii msingi u akjwa ngangari kama nondo tuu
 
Safi sana kiongozi , nikiwa Moshi ufundi nilisoma Plumbing , nilifundishwa kuwa hata system ya choo na bafu havitakiwi kuwa na same path(destination) sababu , ya hao bacteria (anaerobes bacteria) ambao ndio huvunja vunja uchafu.
👍
 
Baada ya kupiga plaster msingi wako, paka black bitumen (changanya na solvent)
Kopo la 4Lts linauzwa kwenye 18,000 mpaka 20,000
Vipi nikijenga tiles?
Je hiyo bitumen i asaidia nini as opposed to kupaka rangi ya kawaida
 
Kwenye nguzo za vibaraza sio lazima uweke nguzo za zege, unaweza ukaweka nguzo ya shape ya "L" kwa kutumia tofali na bado nyumba yako ikavutia lakini pia ikakupunguzia gharama za nondo na ufundi
Tofali unalaza?
 
Bati lina upande dume na upande jike, katika upigiliaji upande jike unatakiwa uwe juu ya upande dume

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
Jike anakuwaje juu ya duume...this goes against nature bro
 
Hili ebu fafanua vizhri na sie back bencher tuelewe vizuri.
Sasa kwa mfano kiwanja kipo kinafa e barabara kuu north wards na kimebanwa between other two plots. Slope yake ni towards the south na mie nataka kuweka mjengo hapo hiyo sebule nataka ipate madirisha on atleast two walls naiweka kwa wapi maana lazima ukuta mmoja utakuwa east au west. Nipe utaalam hapo mwanawane
 
🤣🤣🤣 Aise kumbe site kuna kuliana timing eeh 🤣🤣🤣🤣
 
Uzi mzuri sana kwa wanaohitaji kujenga mambo ya kujifunza hapa ni mengi sana.
 
Ok...je nini tofauti ya single na 3 phase? Mbona sijawahi sikia 2 phase au 4 phase?
Kwa makadieio ya haraka haraka ya wiring ya nyumba ya vymba vitatu; ac kila chumba socket 2 kila chumba heater 3 vyooni yenye muundo wa corridor, chumba kulia chumba kushoto materials inaweza fika kiasi gani?
 
Hii bonge la elimu leo nimesoma page 10 tuu tayari munkari wakujenga nimepata.

Anyways great job sasa mie suggestion yangu tuu ni moja.
Unatupa nondo nzuri sana hapa mwanawane na katika kuborasha basi tutengeneze kipamflet ambacho kitakuwa na jshauri wote huu katika mpangilio mzuri i.e process yote kutoka kusaka plot mpaka finishing.

Kuwe na chapters mahusisi so mtu akifika stage flani anafungua tuu chapter flani.

So unakuwa na chapters kama hivi

Ununuzi wa kiwanja
Maandalizi ya site
Ujenzi wa msingi
Uje zi wa boma
Kupaua etc.

So hapo mtu anaenda direct kwa chapter husika.

Sasa najua wabongo tulivyo wangese nikisema hapa tuchangishe buku 2 kila mdau tupate hii ili tuwe tunatembea nayo au kuwa nayo nda i ya nyumba watapita kushoto.

But anyways unaweza tengeneza hicho kipamflet ukawa unauza mwanawane itasaidia wengi sana
 
Ili upate madirisha pande mbili katika sebule, inatakiwa sebule ikae ubavuni/pembeni mwa nyumba (ambapo mbele kutakuwa na dirisha na mlango wa kuingilia, na ubavuni pia kutakuwa na madirisha mengine mawili). Ramani nyingi ukiziangalia utaona sebule ipo kati na hivyo kufanya sebule iwe na dirisha upande wa mbele pekee huku ikitegemea mwanga na hewa zaidi kutoka madirisha ya Dinning room.
 
Na hili unalosema mie naonaga sana kwenye ramani which i feel inanyima nyuma mzunguko mzuri wa hewa maana inatokea upande mmoja tuu.

Sasa kwa mantiki hiyo, dirisha na mlango vinatakiwa kutazama north alafu madirisha mawili mingine yatizame east au west? Which is better? East au west?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Aise kumbe site kuna kuliana timing eeh [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yah, hizi scenario zipo nyingi sana..mfano mwingine unaweza ukakubaliana na mafundi kujenga msingi wote mpaka jamvi, sasa wakishamaliza kujenga kuta za msingi usishangae fundi akakuambia utafute watu wa kujaza kifusi ili baadae waje wamalizie kazi ya kumwaga jamvi (wakati huo wewe unajua pesa mliyokubaliana na fundi inajumuisha kila kitu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…