Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #121
Mkuu inaonesha kabisa umekuja kwa lengo la kupinga/majibizano, hakuna mahali nimetaja oxygen hapo. Najua lengo lako ni kutaka uonekane mjuzi zaidi mbele ya kadamnasiBacteria wanaochakata uchafu hawahitaji oxygen ili kuishi au bacteria wa kwako ni special?
Sahihi, nyumba ikiwa na msingi mrefu inapendeza zaidiStd nyumba haipaswi kupungua ngazi 4 yaani msingi uinuke futi 2 au 60cm kutoka usawa wa ardhi
Na sio hizo tu, hata kokoto bapa (flaky aggregates), kokoto ndefu (elongated) hazifai hasa kwa high strength concrete. Kokoto ambazo unaweza kutumia kwa zege yoyote (low na high strength concrete) ni zile zenye thickness kubwa, fupi na zenye angle angleKokoto za duara hazifai kutumika kwenye ujenzi; au nasema uongo ndugu zangu?
Ahsante kwa ushauri.Jamiiforums ni msaada mkubwa sana kwenye ulimwengu wa leo unaohitaji akili na matumizi sahihi ya pesa,post za mdau Hechy Essy zimenifungua akili kama hivi alivyoandika ningevijua mapema vingenisaidia sana.
Kwenye ujenzi tusiogope kutumia washauri kisa kukimbia gharama mimi sikuwa na akili hii majibu yake nimeshayaona,kwa mnaoanza ujenzi tafadhalini watumieni watu kama hawa watawasaidia sana.
Inahitaji eneo lenye ukubwa wa mita ngapi?PLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Inatosha kwenye kiwanja cha mita 11m kwa mita 14...hiyo ni pamoja na eneo la kujenga karo la choo na njia za kupita pembeni kuzunguka nyumba kama utaweka uzioInahitaji eneo lenye ukubwa wa mita ngapi?
Hii idea ya tiles ni nzuriWakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa
Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama
Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)
Kwa majengo ya ghorofa ni muhimu kuyafanyia kitu kinachoitwa Structural Analysis kabla ya kuanza ujenzi ili kujua kama hilo jengo litaweza kuhimili mzigo utakaobeba. Lakini pia ujenzi wa majengo ya ghorofa ni tofauti na ujenzi wa jengo la kawaida (chini), katika ujenzi wa ghorofa (Load bearing structures) tofali huwa zinalazwa ambapo sehemu ya mzigo inabebwa na hizo kuta lakini kwa nyumba za chini, tofali zake huwa zinasimamishwa.mkuu nina swali langu naomba unijibu
Hii kuweka nguzo nyumba ambayo ishajengwa zamani, na upandishe gorofa moja .juu yake je inawezekana ?na je gharama za kuweka nguzo zipoje mpka kuweka zege la juu?
Je umazubuti utakuwepo?
Nyumba ya chini ina vyumba 4 sio master,,puplic toil mbili,kuna dining room,siting room,store
Na juu nataka kuweka vyumba viwili master tu ,dining room,siting room..je inaweza ikani cost kiasi gani?
Asante
Hujamsaidia bado ndugu yangu upeo ,Kwa majengo ya ghorofa ni muhimu kuyafanyia kitu kinachoitwa Structural Analysis kabla ya kuanza ujenzi ili kujua kama hilo jengo litaweza kuhimili mzigo utakaobeba. Lakini pia ujenzi wa majengo ya ghorofa ni tofauti na ujenzi wa jengo la kawaida (chini), katika ujenzi wa ghorofa (Load bearing structures) tofali huwa zinalazwa ambapo sehemu ya mzigo inabebwa na hizo kuta lakini kwa nyumba za chini, tofali zake huwa zinasimamishwa.
Lakini pia msingi wa jengo la ghorofa huwa unaenda chini zaidi tofauti na msingi wa majengo ya kawaida n.k
Kiujumla jengo la ghorofa ni vizuri design yake ikaanzia chini kabisa na kama ikitokea kuna kitu ulisahahu na unataka ukiongeze huko juu basi inatakiwa ufanye tena hiyo analysis ili ujue kama hicho utakachokiongeza hakitaleta madhara ya kuanguka kwa jengo
Sent using Jamii Forums mobile app
Majengo ya ghorofa yako ya aina mbili, aina ya kwanza kuna haya ambayo huwa zinajengwa nguzo, mkanda, slab mpaka mwisho (kuta zinakuja kuwekwa baadae, kwa hivyo kuta zake huwa hazibebi mzigo bali zinakaa tu kama uzio). Aina ya pili ni haya ambayo kuta,nguzo na mkanda vyote vinajengwa kwa pamoja kwa hivyo kuta zake pia zinashiriki katika ubebaji wa mzigo na ndio maana huwa tofali zake zinalazwa.Hujamsaidia bado ndugu yangu upeo ,
Mfano kwenye nyumba aliyokwishajenga akachafua angles zake nne za pembeni Kisha Kwa ndani akachagua sehemu hata tatu jumla 7 akatia nguzo za nguvu za hata mita 2 chini, hawezi kusimamisha ghorofa moja juu yake??
Sawa, awali tofali alisimamisha lakini si nguzo zipo kubeba hizo slab za juu?
View attachment 2789950
View attachment 2789951
Majengo kama haya hakuna tofali kabisa bali ni nguzo tu, kama zitawekwa baadae ni usalama tu sio kubeba slabs, na yanaenda juu floors kadhaa, hii moja tu ya ndugu yangu upeo itakua shida?