Kwa majengo ya ghorofa ni muhimu kuyafanyia kitu kinachoitwa Structural Analysis kabla ya kuanza ujenzi ili kujua kama hilo jengo litaweza kuhimili mzigo utakaobeba. Lakini pia ujenzi wa majengo ya ghorofa ni tofauti na ujenzi wa jengo la kawaida (chini), katika ujenzi wa ghorofa (Load bearing structures) tofali huwa zinalazwa ambapo sehemu ya mzigo inabebwa na hizo kuta lakini kwa nyumba za chini, tofali zake huwa zinasimamishwa.
Lakini pia msingi wa jengo la ghorofa huwa unaenda chini zaidi tofauti na msingi wa majengo ya kawaida n.k
Kiujumla jengo la ghorofa ni vizuri design yake ikaanzia chini kabisa na kama ikitokea kuna kitu ulisahahu na unataka ukiongeze huko juu basi inatakiwa ufanye tena hiyo analysis ili ujue kama hicho utakachokiongeza hakitaleta madhara ya kuanguka kwa jengo
Sent using
Jamii Forums mobile app