Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kabla ya kumwaga zege, ni vizuri kupamwagia maji sehemu ambapo unataka kumwaga hiyo zege ili maji yaliyopo kwenye zege yasifyozwe na kusababisha kasi ya reaction kati ya cement na maji (hydration) kupungua na kufanya zege isifikie ule uwezo wake halisi wa kubeba mzigo
Naomba kuelimishwa! Nimeona ktk Ujenzi hususan majengo ya Serikali (madarasa) badala ya kufunga MKANDA niliona wamemwaga zege jengo Zima kisha wakaanza kunyanyua! Nini umuhimu zege kufunika jengo lote na sio mkanda wa msingi tu?
 
Unaweza ukaufikicha mchaichai lisha ukauweka chumbani usiku... unafukuza Mbu
Harufu ya mmea wa mchai chai hufukuza wanyama na wadudu hatarishi kama vile Nyoka, Kenge n.k. Ukiweza tafuta miche yake upande kuzunguka eneo lako, hao wanyama hawatosogea kabisa
 
naomba kujua... nini umuhimu wa Nguzo zinazowekwa ktk kona kuumgqnisha kuta za Boma?
Mahali ambapo kuta mbili zinakutana kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa nyufa, hii ni endapo ukuta mmoja wapo utashuka chini na ukuta mwingine ukabaki vile vile au kuta zote zikashuka chini lakini kwa viwango tofauti (unequal settlement) so mara nyingi huwa tunapendelea kuunganisha kuta kwa kutumia nguzo...mbali na hivyo, nguzo zinasaidia sana kuongeza uimara wa jengo kwa sababu uwezo wa tofali kuhimili mzigo ni tofauti na uwezo wa zege.
 
shukrani sana
 
Naomba kuelimishwa! Nimeona ktk Ujenzi hususan majengo ya Serikali (madarasa) badala ya kufunga MKANDA niliona wamemwaga zege jengo Zima kisha wakaanza kunyanyua! Nini umuhimu zege kufunika jengo lote na sio mkanda wa msingi tu?
Kitaalam inabidi iwe hivyo ila kutokana na hali ya kiuchumi watu wengi wamekuwa wakiskip kumwaga hiyo zege (oversite concrete), badala yake wanajaza kifusi mpaka juu kabisa kabiria na level ya mkanda halafu wanaweka rough floor nyembamba ili kupunguza gharama za ujenzi
 
Katika ununuzi wa bati, usiridhike kukagua bati za juu tu...kagua bati moja baada ya nyingine ili uone kama bati zote ni gauge ile ile uliyokusudia kulipia. Unaweza ukachanganyiwa bati za gauge 32 kati kati ya bando wakati umelipia bati za gauge 30 au gauge 28, mahali popote penye pesa ujanja ujanja huwa haukosekani
 
Je? Nitajuaje kua hii Gauge 28 na sio G30?
Asante
 
Kitaalam inabidi iwe hivyo ila kutokana na hali ya kiuchumi watu wengi wamekuwa wakiskip kumwaga hiyo zege (oversite concrete), badala yake wanajaza kifusi mpaka juu kabisa kabiria na level ya mkanda halafu wanaweka rough floor nyembamba ili kupunguza gharama za ujenzi
Hapa ndipo nataka kujua.
Kama nitamwaga zege nyumba nzima kabla ya kunyanyua boma, si maana yake hata ule mgawanyo wa vyumba nilioufanya kwenye msingi nitakua nimeufukia na zege?

Kama ni hivyo basi kuna ulazima gani wa kugawa vyumba wakati unachimba msingi ikiwa utakuja kufukia wote?
 
Hapa ndipo nataka kujua.
Kama nitamwaga zege nyumba nzima kabla ya kunyanyua boma, si maana yake hata ule mgawanyo wa vyumba nitakua nimeufukia na zege?

Kama ni hivyo basi kuna ulazima gani wa kugawa vyumba wakati unachimba msingi ikiwa utakuja kufukia wote?
Hili swali ni la msingi sana. Makini
 
Hapa ndipo nataka kujua.
Kama nitamwaga zege nyumba nzima kabla ya kunyanyua boma, si maana yake hata ule mgawanyo wa vyumba nilioufanya kwenye msingi nitakua nimeufukia na zege?

Kama ni hivyo basi kuna ulazima gani wa kugawa vyumba wakati unachimba msingi ikiwa utakuja kufukia wote?
Muingiliano wa kuta za ndani na kuta za nje katika msingi unafanya msingi uwe imara zaidi kwa maana kuta za ndani zinazoungana na kuta za nje zinakuwa kama support za ndani kuzuia kuta za nje zisisukumwe na kifusi utakachojaza ndani

Kama utaweka mawe na kumwaga zege, kuna kuta zingine unaweza ukaziskip kuziweka kwenye msingi, zikaja kuotea juu ya jamvi
 
Hii paragraph ya pili,

Sio kwamba Kuta zinazootea au anzia juu ya jamvi zinakua zina uimara hafifu kuliko zile zilizoanzia chini toka msingi unaanza??
 
Kitaalam ni vizuri kuta zote za juu zikalala juu ya mkanda, mkanda ni imara zaidi kubeba line load kuliko slab. Hiyo ya kuacha baadhi ya kuta watu wanafanya tu ili kupunguza gharama, kama mfuko uko vizuri weka tu kuta zote
 
Back
Top Bottom