Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Two Way Switch
Hizi ni switch ambazo unaweza ukazitumia kuwasha ama kuzima kifaa cha umeme (taa,feni n.k) ukiwa sehemu tofauti tofauti (zaidi ya moja)

Mfano katika chumba unaweza ukaweka switch moja ya kuwashia taa pembeni ya mlango, na switch nyingine ukaiweka pembeni ya kitanda.
Hii itakusaidia kuweza kuwasha ama kuzima taa, feni n.k ukiwa hapo hapo kitandani bila kupata shida ya kuinuka kwenda kuzima/kuwasha kifaa katika switch ya mlangoni.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ni vizuri zoezi la kufix milango kwenye frem zake ukalifanya baada ya kumaliza kutengeneza sakafu yako (mfano tiles, terazzo n.k kiujumla ni baada ya floor finish) ambapo chini ya mlango utaacha uwazi mdogo ambao hata Panya mdogo hawezi kupita (japo uwazi wa robo nchi)

Hii itakusaidia milango yako kufunguka vizuri hata kama kuna punje punje za mchanga kwenye sakafu.

Kuna milango mingine unakuta mpaka imechora alama ya robo duara kwenye sakafu kutokana na milango kugusana kabisa na floor, ikitokea hata kuna michanga chini, mlango unashindwa kufunguka mpaka michanga ifagiwe kwanza.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kama eneo lako lina mteremko mkali, ni vizuri nyumba yako ukaijenga kwa level tofauti tofauti kama ngazi ambapo katika kila sehemu ambayo kunakuwa na step, utaweka nguzo kuongeza uimara wa jengo.

Kujenga msingi wa kozi 10+ kutokea usawa wa ardhi ni very risk na wakati mwingine utalazimika kufanga mkanda (beam) zaidi ya mmoja kutokana na msingi kuwa mrefu, achilia mbali idadi ya tofali kuwa kubwa.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Tani moja ya nondo za milimita 12, zinaingia nondo 94.
Kama unajenga ghorofa na nondo zako unanunua kwa tani (uzito), ni vyema ukajua mapema katika kila size flani ya nondo, zinaingia pc ngapi kwa tani moja ili usije ukapunjwa

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Upande wa madirisha ya aluminium, jitahidi ununue madirisha ambayo yana upper transform.

Upper transform ni ile sehemu ndogo ya juu ambayo inagawa urefu wa dirisha katika sehemu mbili.

Ukiachana na uimara wa dirisha, pia upper transform inaongeza mvuto na muonekano wa nyumba tofauti na madirisha ambayo vioo vyake vinaanzia chini mpaka juu bila ya kuwa na transform

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kama nyumba yako bado hujapaka rangi, usibandue zile sticker za kwenye madirisha ya aluminium maana ukizibandua, baadae ukitaka kupaka rangi utapata shida ya kufunika na magazeti.
Bandua sticker baada ya zoezi la kupaka rangi kuisha

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuna baadhi ya profile za aluminium mifereji yake (njia za vioo) ipo mbali mbali, hii inaongeza upenyo (gap) kati ya kioo kimoja na kioo kingine hata kama vioo vyote vitakuwa vimefungwa.

Mijusi, Mbu na wadudu wengine huingia ndani kupitia huo uwazi. Kwa hivyo ukienda kununua madirisha au fundi akija site kupima madirisha inabidi uangalie sample zote za profile na uchague ambazo mifereji yake imekaribiana ili kupunguza huo uwazi wa kioo na kioo au kioo na wavu wa Mbu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
vip

vip kuusu UPVC window
 
Nimepita mahali nimekuta mafundi wamelaza nondo moja moja tu kwenye mkanda (beam). Sasa wanaweza wakawa wana nia nzuri ya kubana matumizi lakini je boss anafahamu kwamba imetumika nondo moja moja?!!

Au boss ndio kapigiwa hesabu ya nondo nne nne then kwenye usukaji wa nondo kafungiwa nondo moja moja, kwa kuwa yeye hayupo, mimi sijui.

Kuna ule mfumo wa watu (maboss) kuwa wanalipia pesa hard ware then wanakuwa wanamuagiza fundi akachukue material dukani wakidhani kwamba wamewakomoa mafundi kuiba.

Kwenye suala la pesa, hata maadui wanaweza wakaungana kuipambania hiyo pesa ili wakipata wagawane, baada ya mgao uadui unaendelea kama kawaida.

Risiti sio ishu, unaweza ukaandikiwa risiti ya mifuko 20 ya cement kumbe umeuziwa mifuko 15, kinachofanyika na hawa wauzaji nikikielezea hapa itakuwa ni mbinu hata kwa wengine ambao hawana hiyo tabia wakajifunza. Kiufupi ni kwamba usiziamini risiti unazopewa ukajua kilichoandikwa pale ni kweli 100%

Haki mimi nitashinda site na mafundi mguu wangu mguu wake 😂
 
Na ndio inavyotakiwa hawa mafundi wetu wanaangalia kumaliza kazi na sio kufanya kazi iwe ya kiwango cha juu
tena mm fundi akintajia bei sipunguzi ata mia ila atafata maelekezo yangu mpaka achoke. siwezi vumilia upuuzi kwenye ujenzi wa nyumba

kilichonikuta nyumba ya kwanza sitakaa nirudie nyumba miaka 6 ni nyufa kila siku unaziba mpaka gharama za kuziba zishafikia gharama za room mbili fill finished
 
Pole sana mwanawane. Unachosema ni kweli wee akisema bei yake usipinge ila sasa nikuwa nae benet mpaka mjengo wakamilika.

Che ngine hawa wapuuzi wavi u wakufikiri. Inabidi kabla ya kuanza ujenzi wa kitu chochote basi wee unaze kufikiria kutakuwa na changamoto gani na uwe na suluhisho maana wao ilimradi iende.

Tena fundi tiles wanakera kweli. Yeye akiona mzigo wa tiles upo basi anahitaji kipande kidogo yeye anachukua nzima anakatalata tuu bila kufikiri
 
Unajua huu uzi inafaa kusoma comments zote za Hechy Essy ukiwa na note book. Fundi akifanya kazi unaangalia na desa lako linasemaje
Mimi nina kinote book changu nimejaza comments zote za Hechy Essy ..hizi nondo zake najiona kabisa na mimi ni nusu Injinia, nikiwa tayar nitamtafuta aniandalie ramani na ushauri wa ziada
 
Ukishinda site kinachofata ni kukukomoa, mahali ambapo panahitajika mifuko mitatu ya cement, wenyewe watachanganya mifuko mitano. Lengo lao hasa ni kukutia hasara zaidi baada ya wewe kuamua kuwabana kupita kiasi
Labda kama hujui ratios zinavyoenda
 
Back
Top Bottom