Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kama eneo lako lina mchanga, anza kwanza kuchimba na kujenga makaro ya choo ili upate mchanga wa kujengea

Kama utachimba shimo la futi 6 upana, futi 8 urefu na kina cha futi 12 utapata mchanga wenye ujazo wa cubic meter 15 sawa na gari kubwa moja la 15m³ ambao unatosha kujengea tofali za msingi

Na pia mchanga utakaokuwa umechimba kwenye msingi utaweza kupata zaidi ya cubic meter 30 kwa nyumba yenye line meter ya 100m+ sawa na trip mbili za gari kubwa (huu utajengea boma)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kama unajenga sehemu yenye asili ya maji maji, tandika chini nailoni kabla hujamwaga zege ya chini kwenye msingi (blinding) ili kuzuia maji yasipande juu kuanzia chini kabisa. Wakati unasimamisha tofali za boma, weka tena nailoni (Damp proof course, DPC) na pia kati kati ya vyumba utandike nailoni (Damp proof memberane, DPM)


Kutakuwa na offer ya punguzo la bei (8% Discount) kufuatia sikukuu ya nane nane mpaka Jumapili tarehe 11/08/2024 saa kumi na mbili jioni

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane.
 
Jitahidi sana mkanda wa juu, kina chake kisipungue nchi 6 sawa na sentimita 15...Ukiweza weka hata nchi 8 itakuwa bora zaidi maana juu ya sehemu ambazo zina madirisha na milango kuna mzigo mkubwa unabebwa na huu mkanda.

Huduma ya kutembelea site (Site Visit) ipo, ni kila jumamosi na jumapili

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Jitahidi sana mkanda wa juu, kina chake kisipungue nchi 6 sawa na sentimita 15...Ukiweza weka hata nchi 8 itakuwa bora zaidi maana juu ya sehemu ambazo zina madirisha na milango kuna mzigo mkubwa unabebwa na huu mkanda.

Huduma ya kutembelea site (Site Visit) ipo, ni kila jumamosi na jumapili

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane

Mkanda wa Inch 8 lazima uwe na nondo nne mraba zilizosukwa au hata tatu kwa pembetatu tu..
 
Mkanda wa Inch 8 lazima uwe na nondo nne mraba zilizosukwa au hata tatu kwa pembetatu tu..
Kwa mkanda wa juu, ni vyema ukatumia nondo nne nne, ila kwa mkanda wa chini ukitumia nondo tatu tatu haina shida.

Kama utatumia nondo tatu tatu mkanda wa juu, basi ni vizuri sehemu zote zenye uwazi (milando na madirisha) ukaongeza kipande cha nondo upande wa chini, yani ikawa ni nondo 3 chini, nondo moja juu kwa ajili ya kushikilia ringi
 
Kwa mkanda wa juu, ni vyema ukatumia nondo nne nne, ila kwa mkanda wa chini ukitumia nondo tatu tatu haina shida.

Kama utatumia nondo tatu tatu mkanda wa juu, basi ni vizuri sehemu zote zenye uwazi (milando na madirisha) ukaongeza kipande cha nondo upande wa chini, yani ikawa ni nondo 3 chini, nondo moja juu kwa ajili ya kushikilia ringi
Thanks nilitumia nne mikanda yote ila kuna sehemu nondo zilikua zimetokeza zinaonekana sijui walipunja mchanga kwenye zege au ni lile Box lilikosewa. Kuna fundi akawa ananiambia sijui mpiga box hakutumia pipe level. Pipe level ni nini😥
 
Thanks nilitumia nne mikanda yote ila kuna sehemu nondo zilikua zimetokeza zinaonekana sijui walipunja mchanga kwenye zege au ni lile Box lilikosewa. Kuna fundi akawa ananiambia sijui mpiga box hakutumia pipe level. Pipe level ni nini[emoji26]
Hapo kuna mawili
1. Fundi hakuweka spacer kati ya nondo na box
2. Size ya ringi alizotumia haikuwa sahihi, kwa hivyo fundi alikosa hata hiyo nafasi ya kuweka hizo spacer

Kitaalam nondo inatakiwa ifunikwe na zege kwa angalau nyama ya nchi moja, kama mkanda wako una upana wa nchi 9 basi unatakiwa utumie ringi yenye upana wa nchi 7 (nchi moja cover ya kulia, na nchi moja cover ya kushoto)

Nondo ikiwa wazi kama hivyo ni rahisi kupata kutu kutokana na unyevu nyevu, inatakiwa upige plaster mapema.

Kuna uwezekano pia nyufa zikatokea kwenye plaster pale nondo itakapotanuka kutokana na joto kali. Utanukaji wa plaster ni tofauti na utanukaji wa nondo pale kunapotokea ongezeko la joto, lakini kwa zege na nondo utanukaji wake unakaribiana kwa hivyo ilibidi nondo ifunikwe na zege then plaster ndio iwe juu ya zege
 
Katika suala la ushauri, mafundi wapo wa aina mbili

1. Fundi wa kwanza
Huyu anakupa ushauri wa kitaalam bila kujali kwamba kutakuwa na ongezeko la kazi mbali na vile mlivyokubaliana (ambapo anaweza akakuomba nyongeza ya malipo au akaamua tu kukufanyia fair licha ya kuwa na ongezeko la kazi)

2. Fundi wa pili
Huyu anakupa ushauri ambao utakuwa unampa unafuu katika kazi yake ili amalize kazi haraka mfano kwenye ramani inaweza ikawa inaonesha mkanda uwe na kina cha nchi 6 lakini yeye akakushauri kwamba hata ukiweka kina cha nchi 4 haina shida au katika kuchimba msingi, anaweza akachimba tu kidogo halafu akakuambia kwamba hii haina shida, hata mahali flani tulijenga hivi hivi na hakukuwa na tatizo (hapo ujue anajitengenezea urahisi ili apunguze ukubwa wa kazi)

NB: Usifuate kila ushauri unaopewa na fundi, pima na wewe mwenyewe katika hali ya kawaida kabla ya kukubali ushauri wake. Wakati mwingine anaweza akakushawishi ununue bidhaa kampuni/duka flani sio kwa sababu ya ubora, ni kwa sababu ameahidiwa mgao (commission) kila anapoenda kununua bidhaa mahali hapo


Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
Mkuu unajua sana….Unajua mno
 
Katika ujenzi wa ghorofa, ni muhimu sana ukafuata maelekezo yote ya michoro kama inavyoonekana mfano
1. Kama document zako zinaonesha zege ya nguzo iwe ni grade 25, basi inabidi utumie grade 25 kweli

2. Kama document zako zinaonesha nguzo ziwe na nondo nne nne za milimita 16, basi inabidi ufanye kama maelekezo yanavyotaka

3. Kama slab yako inataka nondo zipishane kwa spacing ya sentimita 20, weka hivyo hivyo...usije ukaongeza spacing ili utumie nondo chache n.k

Ni bora ukaongeza kuliko kupunguza ili kujiweka salama zaidi, majengo ya ghorofa yana mahesabu makali hivyo katika ujenzi wake inahitaji umakini wa hali ya juu kwa kufuata maelekezo yote ya michoro


Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Shida yangu Ni Ramani huo mchoro mkubwa tayari nyumba ya L na huo mdogo Ni kisima hivyo vipimo nataka ra amani ya nyumba mkuu na makadilio ya gharama hata kujenga ukuta was nje was fensi
 
Hivi zile bati za steps (muundo kigae) mbao zake zinapigwa karib karibu sana hua wanaweka centimetres (cm) ngap kuachan baina ya mbao na mbao
Screenshot_20240813-070137_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom