Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Mkuu kuna slab siku hizi zipo namna hiyo hapo chini naomba nijuze unayofahamu kuhusu slab hizi maana wanadai zinapunguza sana gharama but nina mashaka kuhusu ubora in the long run.
View attachment 3075165View attachment 3075166View attachment 3075168View attachment 3075169
Binafsi sijawahi kutumia aina hii ya slab lakini lengo hasa la kuweka hizo tofali ni kupunguza kiasi cha material yatakayohitajika kwenye zege ambapo inapunguza hizo gharama na pili ni kupunguza uzito wa slab yani self weight (hizo tofali huwaga ni hollow blocks, ni tofali ambazo kati kati zinakuwa na matundu)
 
Ok Engineer ujenzi wa aina hii nimekuwa nikiuona Nigeria, Uganda, Kenya na bongo nimeona napo umeanza hivi karibuni, kwa Kenya nafahamu kampuni inayouza hizi slab imekuwa ikizingatia sana viwango kwa maana ya kufanya materia testing n.k.
Nafikiri soon utaanza kutumiwa na kushauriwa na wataalam wengi wa ujenzi kwa kadiri utaalam utakavyoruhusu.
 
Kawaida teknolojia mpya inapoanza kutumika mahali, huwa inasubiriwa muda flani upite (let say miaka 10, 20 n.k) ndipo watu wanakuja na conclusion kwamba teknolojia hii itatufaa au lah vinginevyo mtu akubali kuwa chambo/tester (watu wapate majibu kupitia yeye)

Kuna teknolojia zingine huwa zinafanyiwa mahesabu kabisa na kupitia hayo mahesabu, majibu yanapatikana muda huo huo kwamba itafaa au haifai.

Binafsi aina hii ya slab sijawahi kukutana nayo live kwa huku kwetu zaidi ya kuona tu kwenye video na picha
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Nimeipenda elimu yako.
 
Wakati mwingine chemba za vyoo huwa zinajaa kwa sababu bomba zinazosafirisha uchafu zinakuwa zimepasuka chini kwa chini na kufanya mchanga/udongo uingie kwenye bomba na kuziba njia kwa hivyo uchafu unakuwa haufiki kwenye karo (unapotelea sehemu zenye leakage katika bomba)

Hapa solution ya kudumu ni kubadilisha bomba in case kama zitakuwa zimepasuka lakini pia ni vizuri ukatumia bomba ambazo kuta zake ni nene (hakikisha kabla hujanunua, unaminya kule mwisho wa bomba uone kama inabonyea au lah)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Fundi nina swali kidogo. Ninategemea kujenga nyumba ya mfumo huu hapa chini... Sasa nilitaka kufahamu, je kutakuwa na shida kwenye upauaji/bati
IMG_6973.jpeg
kulingana na hizo kona zilizopo kwenye jengo?
 
Attachments

  • IMG_6960.jpeg
    IMG_6960.jpeg
    739.3 KB · Views: 24
Kama wiring yako ni ya mfumo wa kuingiza nyaya kwenye bomba (conduit pipes), tumia single wire

Twin wire matumizi yake ni kwa wiring ya nje (surface wiring) mfano kwenye kuta n.k ambapo utabana waya zako na saddle clip. Mfumo huu wa surface wiring ulikuwa ukitumika zaidi miaka ya nyuma, ambapo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na mfumo wa kuchimbia bomba katika kuta

Wapo wanaonunua twin wire na kuzichuna ili wapate single wire mbili, kitu ambacho ni hatari kwa maana ile plastic ya waya inaweza ikachunika mahali wakati wa kuchuna na wewe ukaitumia bila kujua, baadae ikaleta madhara kutokana na mgusano wa live na neutral

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ngazi zote zinatakiwa zilingane kimo, mfano kama kimo ni nchi 5 basi weka nchi 5 ngazi zote, kama ni nchi 6, weka nchi 6 ngazi zote

Hii ni kwa sababu, mtu anapopanda ngazi ya kwanza, ya pili n.k tayari miguu inakuwa imeshakariri kile kina ambacho miguu imeanza nacho katika ngazi za awali kwa hivyo hata miguu itakuwa inajikunja kwa namna ile ile na ndio maana wakati mwingine mtu anaweza akawa anapanda/shuka ngazi huku anachezea simu na bado asijikwae

Itakapotokea ngazi moja wapo ipo tofauti na ngazi zingine, uwezekano wa kujikwaa katika hiyo ngazi ni mkubwa sana

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukijaza kifusi katika msingi bila kukimwagia maji, kuna uwezekano wa jamvi yako kushuka baada ya muda
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Attachments

  • 20240901_111251.jpg
    20240901_111251.jpg
    37.5 KB · Views: 22
Wakati wa kuset jengo, sio lazima kutumia mbao (profile) kusetia...unaweza ukatumia tofali hizo hizo ulizoleta site kusetia ambapo utakuwa umepunguza gharama zisizo na ulazima

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuna mfumo flani wa ngazi ambao chini ya ngazi kunakuwa na uwazi (bahati mbaya sina picha yangu mwenyewe), nahofia mambo ya copyright

Ule mfumo kiusalama sio mzuri vinginevyo itabidi utafute namna itakayofanya huo mfumo uwe salama

Kwenye huo uwazi ambao upo kati ya ngazi moja na ngazi nyingine, anaweza kukaa mnyama/mdudu hatari yoyote kama Nyoka, Kenge, Tandu, Nge n.k hasa kipindi cha mvua ambapo wadudu hawa hutafuta hifadhi kutokana na mashimo yao kujaa maji

Design yoyote inabidi pia izingatie na mambo ya usalama watakaokuwa wanaishi humo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi wa kuta, ni vizuri level za kuta zote zikawa zinachukuliwa sehemu moja ili kuepuka kuta kupishana

Kila fundi ana namna yake ya kujenga, mwingine anaweka udongo kidogo, mwingine anaweka udongo wa wastani na mwingine anaweka udongo mwingi

Sasa huyu fundi anayetumia udongo kidogo, ndiye anatakiwa ajenge ukuta ambao utakuwa kama gauge kwa kuta zingine zote (mafundi wote wachukulie level kutoka kwake, hapa itawalazimisha hata mafundi waliozoea kutumia udongo mwingi watumie udongo kidogo kutokana na kufuata level ya huyo fundi)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom