Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Hizi wanapiga Bongo?

Jamaa mwingine huyo instagram anajiita regiment_builders ushindwe mwenyewe tu ila msisitize kwenye slab asiache kuweka wire mesh BRC maana naye nimeona anarahisisha sana ujenzi huyu😝
Nilichojifunza bongo tumenga'nga'nia ujenzi kwa kutumia namna material za zamani wakati kuna namna mpya kwa mfano nimeona kuna kuta wanaweka poystrene material hii yote ni kupunguza cost, kuna hollow blocks vilevile
Hizi namna za low cost housing utazikuta kwenye miradi mikubwa sanasana
 
Katika ujenzi wa majengo ya ghorofa, usukaji wa nondo katika slab, nguzo, ngazi ama mkanda (beam) n.k una kanuni zake hivyo ni muhimu sana katika hizi hatua ukamshirikisha mtaalam ahudhurie site ili kuhakikisha kanuni zote zinafuatwa

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Wakati mwingine mtu unaweza ukahadaika na picha za kazi wanazotumia mafundi kujitangazia mitandaoni, sasa changamoto inakuja pale unapowapa kazi hao mafundi. Unabaki unajiuliza mbona walichokifanya ni tofauti kabisa na jinsi wanavyojitangaza mitandaoni!!!?

Sasa nakuibia siri, mafundi wengine huwa wanaiba picha za watu na kuzitumia hizo picha kujitangazia huko mitandaoni.

Yupo jamaa yangu mmoja, alijengewa na mafundi aliowaamini sana uwezo wao kupitia picha zao za mitandaoni (kipindi hicho alikuwa anamtumia mdogo wake kuwasimamia hao mafundi) na sasa hivi anafikiria kulivunja boma lake aanze upya baada ya kufika site na kujionea yaliyofanyika

Mitaani kuna mafundi wazuri sana lakini ndio hivyo wako mbali sana na dunia, hawana hata habari na hii mitandao. Sasa mtu akipita site akaona kazi nzuri inavutia, ndio kama hivyo anapiga picha kiwizi wizi halafu anazitumia huko mitandaoni (Fundi aliyefanya hiyo kazi hana hata habari na hata hiyo simu kubwa hana, atajuaje kama kazi zake zinatumiwa na watu wengine kujitangaza?)

Point to Note:
Usihadaike na picha za mitandaoni, ni afadhali ukatembea tembea mwenyewe mitaani kutafuta mafundi wazuri ili usije ukaingia hasara, ujenzi ni mara moja tu, ukikosea maana yake ni aidha urudie au ukubaliane na uhalisia

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kama kiwanja chako kiko flat, makaro ya vyoo unaweza ukaweka popote kutegemeana na design ya nyumba yako unavyotaka iwe, lakini kama kiwanja chako kina mteremko (slope), basi hapo option iliyopo ni kujenga makaro yako sehemu ya kiwanja iliyo chini vinginevyo itabidi uingie gharama kuinua msingi uende juu zaidi ili kutengeneza mteremko (down slope) kati ya floor ya nyumba na mahali unapoenda kujenga hayo makaro

Hapo sasa itategemeana na umbali uliopo kati ya vyoo na mahali ambapo hayo makaro yamejengwa, kiujumla slab ya makaro ya choo inatakiwa iwe chini ukilinganisha na level ya jamvi (floor) ya nyumba vinginevyo uchafu wa kwenye makaro utakuwa unarudi ndani kwenye vyoo pindi makaro yatakapokuwa yamejaa

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Rekebisha hizo vent za huko kwenye paa, hazina kazi yoyote zaidi ya kuozesha ceiling board
Vent ni muhimu zikiwekwa vizuri zinapooza joto darini na kuzuia nyumba kupasuka, ila huwa sielewi pale wayu wanaweka vioo badala ya wavu
 
Point to Note:
Usihadaike na picha za mitandaoni, ni afadhali ukatembea tembea mwenyewe mitaani kutafuta mafundi wazuri ili usije ukaingia hasara, ujenzi ni mara moja tu, ukikosea maana yake ni aidha urudie au ukubaliane na uhalisia
Upo sahihi kabisa, majuzi nimemchukua fundi Dar baada ya kuona kazi zake mtandaoni akanifanyie kazi Mikumi, najuta nimepoteza frdha yangu, ila nadhani wengi wao wanapiga picha kazi za watu wengine na kujinasibu kuwa ni kazi zao
 
Umakini mkubwa unahitajika katika uchaguzi wa mafundi, maana wakiharibu unakuwa umepata hasara mara mbili (pesa uliyomlipa fundi wa awali, pesa ya kuja kurudia tena/kukarabati na pesa ya kununua material mengine)
 
Hivi kufunga mkanda kabla ya kuanza dirisha pale kati kati ina madhara gani? Msingi haujafungwa mkanda
 
Hivi kufunga mkanda kabla ya kuanza dirisha pale kati kati ina madhara gani? Msingi haujafungwa mkanda
Mkanda wa kati kazi yake ni kuzuia zile nyufa zinazojitokeza chini ya madirisha zisitokee kwa hivyo inaongeza uimara zaidi

Kama kwenye msingi hakukufungwa mkanda, basi ni afadhali huo mkanda wa kati ungefungwa kwenye msingi, kati kati ndio kukabaki bila mkanda
 
Umakini mkubwa unahitajika katika uchaguzi wa mafundi, maana wakiharibu unakuwa umepata hasara mara mbili (pesa uliyomlipa fundi wa awali, pesa ya kuja kurudia tena/kukarabati na pesa ya kununua material mengine)
Kwa sasa hao ndio wengi hasa wanapiga picha nyumba kazi z mafundi wengine wanasema ni wao. Kumbe ni takataka TU.
 
Wakati mwingine mtu unaweza ukahadaika na picha za kazi wanazotumia mafundi kujitangazia mitandaoni, sasa changamoto inakuja pale unapowapa kazi hao mafundi. Unabaki unajiuliza mbona walichokifanya ni tofauti kabisa na jinsi wanavyojitangaza mitandaoni!!!?

Sasa nakuibia siri, mafundi wengine huwa wanaiba picha za watu na kuzitumia hizo picha kujitangazia huko mitandaoni.

Yupo jamaa yangu mmoja, alijengewa na mafundi aliowaamini sana uwezo wao kupitia picha zao za mitandaoni (kipindi hicho alikuwa anamtumia mdogo wake kuwasimamia hao mafundi) na sasa hivi anafikiria kulivunja boma lake aanze upya baada ya kufika site na kujionea yaliyofanyika

Mitaani kuna mafundi wazuri sana lakini ndio hivyo wako mbali sana na dunia, hawana hata habari na hii mitandao. Sasa mtu akipita site akaona kazi nzuri inavutia, ndio kama hivyo anapiga picha kiwizi wizi halafu anazitumia huko mitandaoni (Fundi aliyefanya hiyo kazi hana hata habari na hata hiyo simu kubwa hana, atajuaje kama kazi zake zinatumiwa na watu wengine kujitangaza?)

Point to Note:
Usihadaike na picha za mitandaoni, ni afadhali ukatembea tembea mwenyewe mitaani kutafuta mafundi wazuri ili usije ukaingia hasara, ujenzi ni mara moja tu, ukikosea maana yake ni aidha urudie au ukubaliane na uhalisia

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Mkuu Henchy Essy nikupe pongezi kwa elimu unayoitoa humu ndani.

Katika pita zangu mtandaoni nilikutana na nyumba hiyo hapo, kwa ujuzi na uzoefu wako ninaomba unitoe tongo tongo juu ya haya maswali yangu.

1, Je hizo nguzo mbili (Upande wa kushoto), zilizojengwa kwa tofali bila nondo wala zege ni imara na madhubuti kweli?

2. Kama hizo nguzo mbili ni imara na madhubuti, ikiwa nitajenga nguzo nne (Mbili kushoto na mbili kulia), na kila nguzo moja nikajenga kwa kutumia vipande vya nusu tofali (Kwenye picha zimetumika tofali nzima) na juu ya hizo nguzo nikamwaga zege la lenta, je nguzo hizo zitakuwa na uimara na uthabiti wa kuweza kubeba Gable la nyumba?.

Naomba nitangulize shukrani.
1723898063104.jpg
 
Naomba nitangulize shukrani.View attachment 3095509
1. Ndio, hapo haina shida. Ukitumia nguzo za tofali inabidi tofali zake uzilaze lakini pia usijenge tofali nzima nzima tupu, inatakiwa zifatane tofali nzima, then tofali za vipande mpaka juu

2. Nguzo za tofali hutakiwi kujenga kwa nusu tofali, ukijenga kwa nusu tofali maana yake kozi inayofata inabidi iwe na vipande vya robo tofali. Hapo huwa tunatumia tofali nzima, ambapo kozi ya nusu tofali na tofali nzima zinakuwa zinafatana
 
Ulishawahi kuchimba shimo kwa lengo la kuweka karo la choo lakini ukakutana na maji kabla hata ya kufikia kina cha futi 10?

Ikitokea hivyo, inatakiwa uongeze mapana/marefu ya shimo ili kupata shimo la ujazo ule ule uliokuwa umekusudia

Lakini pia inabidi utandike nailoni, Damp proof membrane (DPM) kabla ya kumwaga zege na kuanza ujenzi wa tofali

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Mara nyingi wezi majumbani huwa wanalenga zaidi kuiba vitu vya sebuleni kama TV, redio na vitu vingine vingine vya thamani kwa sababu wanajua sebuleni ndio sehemu ambayo panakuwa hakuna watu usiku

Hivyo basi, kiusalama design yako ya ramani inatakiwa angalau dirisha moja la chumba chohote cha kulala liwe linaangalia upande wa mbele wa nyumba ili kama kuna lolote linafanyika mtu aweze kuona

Lakini pia kama utaweka uzio (fence), upande wa nyuma usiweke louvers (yale madirisha ya urembo ili kuongeza usalama zaidi)

Kuna louvers ambazo zinaruhusu hewa kupita lakini haziruhusu mtu kuona ndani (hizi kiusalama ndio nzuri kutumia, zinakuwa zinaongeza privacy pia)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika upachikaji wa fremu za milango katika kuta, fremu zinatakiwa ziflash na ukuta upande wa ndani wa chumba na sio upande wa nje. Hii inasaidia mlango wako uweze kuzunguka nyuzi 180 bila kukwama

Kama fremu zako zitaflash na ukuta upande wa nje, na milango yako ikawa inafungukia kwa ndani, maana yake ile sehemu ya unene wa ukuta iliyobaki ndani itakuwa inazuia milango yako isiweze kufunguka kwa nyuzi 180, milango itakuwa inafunguka kwa nyuzi 90 pekee

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika zoezi la upigiliaji wa mbao za dari, usinunue mbao ndefu zote. Ili kuokoa gharama inabidi uchanganye mbao ndefu na mbao fupi kulingana na mahitaji

Bei ya mbao fupi (12ft/pc) kwa Dsm ni Tsh 2,800/=
Bei ya mbao ndefu (20ft/pc) ni Tsh 6,500/=

Mpaka hapo kimahesabu utaona kwamba bei ya mbao ndefu na bei ya mbao fupi kwa futi moja hazilingani, itakuwa haina maana kama utanunua mbao ndefu halafu ukaitumia sehemu ambayo urefu wake hauzidi futi 12 (ni afadhali ungenunua mbao fupi mbili ambapo ungetumia Tsh 5,600/= ukaokoa Tsh 900 kwa kila mbao ndefu moja)

Hiyo Tsh 900/= unaweza ukaiona ni ndogo lakini ukizidisha mara 100 unapata Tsh 90,000/= (hii saving ungeweza kununua kiroba cha kg 25 za misumari kwa ajili ya hilo zoezi la upigiliaji wa mbao za dari au ungepata mbao zingine 32 za futi 12)

Kama chumba chako upana wake hauzidi futi 12, basi unaweza ukatumia mbao fupi tupu lakini kama upana wake unazidi futi 12, basi itabidi ununue mbao fupi na mbao ndefu

Mbao nzima (ambazo hazikatwi) inabidi ziwe sambamba (parallel) na mapana ya chumba, na mbao za kukatwa inabidi ziwe sambamba na marefu ya chumba

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Baada ya floor yako kukamilika, maji yakimwagwa kwenye hiyo sakafu inabidi maji yakimbilie mlangoni

Hii inasaidia hata wakati wa kupiga deki chumba, maji yasituame sehemu nyingine yoyote (mfano chini ya kitanda, kabati n.k). Lakini pia hata ikitokea maji ya mvua yameingia ndani kupitia madirishani, we unayasubiri tu pale mlangoni na ndoo yako na sio kuhangaika kuyakusanya chumba kizima

Slope inayowekwa hapo inakua ni ndogo sana kiasi kwamba mtu hawezi kuiona kwa macho na wakati mwingine hata ukitumia pima maji ile bubble inakuwa bado ipo kati kati isipokuwa edge moja ya bubble inakuwa inagusa au kukaribiana na mstari wa kile kipande cha kati

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kwa ardhi kama hii inachanika wakati wa jua na kukaza wakati wa mvua unafanyaje kujiepusha na nyufa

Rafki yangu kajenga ila nyumba inapiga nyufa vibaya mno kaziba mpaka kachoka

20240923_163659.jpg
 
Kwa ardhi kama hii inachanika wakati wa jua na kukaza wakati wa mvua unafanyaje kujiepusha na nyufa

Rafki yangu kajenga ila nyumba inapiga nyufa vibaya mno kaziba mpaka kachoka

View attachment 3104381
Hapo kwanza inatakiwa umwagwe mchanga wa kutosha baada ya kuchimba msingi, lakini pia wakati wa kujaza kifusi usiurudishie ule udongo uliochimba kwenye msingi (tafuta udongo mwingine wenye asili ya kichanga uutumie kama kifusi na umwagie maji ya kutosha ili udongo ujishindilie chini)

Pia kama bajeti yako iko vizuri, unaweza ukamwaga na zege yenye BRC au ule wavu wa madirisha (wire mesh, wengine wanasuka nondo kabisa hata za milimita 10 au 8) kuzunguka msingi mzima. Baada ya hapo ndio wanaanza kujenga kuta za msingi
 
Weka chemba katika kila sehemu ambapo bomba zako za mfumo wa maji taka zinabadili uelekeo ili iwe rahisi kufanya uchunguzi pale inapotokea tatizo la kuziba kwa chemba, usitumie Elbows za nyuzi 90 kuunga bomba moja na nyingine

Bomba moja lina urefu wa futi 20 sawa na mita 6, kama umbali kutoka chemba moja na chemba nyingine ni zaidi ya mita 6, basi ni bora ukaweka chemba nyingine kati kati ya hizo chemba mbili kuliko kuunga bomba inapoishia hiyo mita 6

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom