Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
- #861
Tofali za siku hizi zina changamoto nyingi, utakuta tofali umenunua sehemu moja na machine ni moja lakini ukubwa unatofautiana. Tofali moja unakuta imezidi upana wa nchi 9, na nyingine haijafika hiyo nchi 9
Kuna tofali zingine unakuta upande mmoja umekaa tenge, hazijanyooka kutokana na allignment ya umbo (mould) katika machine
Kufuatia changamoto hizi, inabidi kabla ya kununua tofali uende na kobilo na tape ya kupimia ili kuhakikisha tofali utakazonunua ziko sawa kabla ya kuzipakia. Ukipima hata tofali 10 tu kutoka katika mafungu tofauti tofauti, utapata jibu kama tofali ni nzuri au lah
Changamoto ya tofali kukaa tenge ndio changamoto kubwa zaidi, ukitumia kobilo kuinyoosha, tofali inakuwa imeinama na ukitumia pima maji, tofali inakuwa imenyooka kwenye ulalo lakini kwenye wima inakuwa imepinda. Hapo kama fundi hajagundua tatizo, fundi atahangaika kutwa kunyoosha kuta
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane