Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Tofali za siku hizi zina changamoto nyingi, utakuta tofali umenunua sehemu moja na machine ni moja lakini ukubwa unatofautiana. Tofali moja unakuta imezidi upana wa nchi 9, na nyingine haijafika hiyo nchi 9

Kuna tofali zingine unakuta upande mmoja umekaa tenge, hazijanyooka kutokana na allignment ya umbo (mould) katika machine

Kufuatia changamoto hizi, inabidi kabla ya kununua tofali uende na kobilo na tape ya kupimia ili kuhakikisha tofali utakazonunua ziko sawa kabla ya kuzipakia. Ukipima hata tofali 10 tu kutoka katika mafungu tofauti tofauti, utapata jibu kama tofali ni nzuri au lah

Changamoto ya tofali kukaa tenge ndio changamoto kubwa zaidi, ukitumia kobilo kuinyoosha, tofali inakuwa imeinama na ukitumia pima maji, tofali inakuwa imenyooka kwenye ulalo lakini kwenye wima inakuwa imepinda. Hapo kama fundi hajagundua tatizo, fundi atahangaika kutwa kunyoosha kuta

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Uwiano wa mchanga na saruji katika udongo wa kujengea (mortar) unategemea pia na hali ya mchanga jinsi ulivyo, kuna mchanga mwingine una vumbi jingi hivyo ukitumia ratio ile ile uliyozoea kutumia siku zote, udongo utakosa nguvu iliyokusudiwa ya kuunga hizo tofali

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Wakuu Nina kiwanja cha 50ft*40ft ramani hapo chini tafadhar naomba makadirio ya mahitaji .
Natanguliza shukuran
 
Attachments

  • house.jpg
    house.jpg
    309.2 KB · Views: 16
Wakuu Nina kiwanja cha 50ft*40ft ramani hapo chini tafadhar naomba makadirio ya mahitaji .
Natanguliza shukuran
Hapo ulipoandika CH kama ndio nafasi ya karo la choo, nafasi haitatosha
Tuwasiliane upate ramani na makadirio kwa bei ya offer, zimebaki siku 19 muda wa ofa kuisha
 
Ukienda kununua misumari ya bati, tafuta misumari ambayo shina zake zina mistari mistari kama mistari ya screw. Hii ni mizuri zaidi hata ukija upepo mkali, inakuwa ngumu bati kuezuliwa tofauti na misumari ambayo iko plain

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ili nyumba ifanane kabisa na ramani husika, ni lazima vipimo viwe na uhalisia katika ujengaji wake, vinginevyo ramani lazima itafanyiwa editing

Mfano unakutana na ukuta una distance ya sentimita 55 wakati huo tofali zima lina urefu wa sentimita 45. Ili itimie sentimita 55, inabidi fundi akate kipande cha sentimita 7.5 aunge na udongo wa nchi 1 kitu ambacho ni kigumu sana ndio maana wakati mwingine unakuta fundi haweki udongo kati ya tofali na tofali kwa sababu nafasi ya kuweka udongo inakosekana, kitu ambacho ni makosa katika ujenzi

Lakini kingine, unaweza pia ukakuta ukuta una distance chini ya sentimita 45 na umesimama wenyewe (free standing) kutokea usawa wa dirisha. Hapa pia ujenzi wake unakuwa mgumu kwa sababu haitakiwi tofali ziwe zinajengwa nzima nzima kwa kufatana. Kama chini ilikuwa ni tofali zima, basi juu yake inabidi ijengwe vipande vya nusu tofali

Editing katika ramani huathiri zaidi ukubwa wa madirisha na milango lakini pia hata position zake, ambapo inalazimika kupunguza ama kuongeza ukubwa ili kupata urahisi katika ujengaji wake.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ili dari lako liwe imara, marefu ya gympsum board yanatakiwa yagawanywe kwa 3. Urefu wa gympsum board ni sentimita 244, ukigawanya kwa 3 unapata 81cm kwahivyo utakuwa unapigilia mbao kila baada ya sentimita 81 kutokea ukutani.

Wengine wanaganywa marefu kwa 2 ili kuokoa idadi ya mbao lakini kutokana na uzito wa gympsum board yenyewe huwa inafika mahala screw zinaanza kuashia kidogo kidogo na hivyo kusababisha hata mipasuko katika maungio ya gympsum board moja na nyingine, na kwenye mikanda ya pembeni

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika upande wa madirisha ya aluminium, kama unategemea kuweka dirisha la urefu wa futi 6 basi ongezea futi 1 ili iwe futi 7.

Hii ni kwa sababu, katika dirisha la aluminium kuna ile sehemu ya juu ya dirisha (transom) ambayo mara nyingi ni kama haitumiki kwa hivyo ukiweka dirisha la futi 6, vioo vikubwa vya chini havitakuwa na huo urefu wa futi 6, vitakuwa na urefu wa futi 5 au chini ya hapo kutegemea na urefu wa hiyo upper transom.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kwa jengo la ghorofa moja, minimum diameter ya nondo kwa nguzo inayotakiwa kutumika ni milimita 16, hiyo ya milimita 12 watu wanaforce tu kupunguza gharama.

Kwenye jengo la ghorofa, nondo za milimita 12 huwa zinatumika kwenye slab na ngazi
Asante mkuu kwa maelezo mazuri. Je kama nimetumia mm16 kwenye column ni lazima msingi uwe na 16mm? Au naweza kutumia 12mm kwenye msingi?
 
Wakuu naombeni estimates ya nondo mm16 kwenye column. Kuanzia kwenye footing mpaka ukuta. Ukuta ni 4.65(Msingi 1.5m +ukuta 3.15m)
 
Asante mkuu kwa maelezo mazuri. Je kama nimetumia mm16 kwenye column ni lazima msingi uwe na 16mm? Au naweza kutumia 12mm kwenye msingi?
Hapana, kwenye msingi usitumie kabisa nondo za 12mm kwenye nguzo maana huko ndipo kwenye mzigo mkubwa. Nondo huwa zinapungua (idadi au size) kwa kwenda juu, sio kuja chini.
Kiasi cha mzigo unaobebwa na nguzo za second floor ni tofauti na kiasi cha mzigo unaobebwa na nguzo za first floor ndio maana unaweza ukakuta nguzo zimeanzia chini na nondo sita sita lakini juu zikamaliza na nondo nne nne
 
Maelezo yako yote yamenifaa. Ila kwenye msingi nilimaanisha ring beam foundation. Kama nimetumia column 16mm je ring beam zitaweza kutumika 12mm?
 
Maelezo yako yote yamenifaa. Ila kwenye msingi nilimaanisha ring beam foundation. Kama nimetumia column 16mm je ring beam zitaweza kutumika 12mm?
Kiujumla jengo lolote la ghorofa, nondo za milimita 12 huwa zinatumika katika slab, kuta za lift na ngazi. Kwenye Ground beam, wengine huwa wanaforce kuweka nondo za milimita 12 lakini wanafunga nondo sita sita (juu tatu, chini tatu), sio nne nne.
 
1. Size ya base ni 1m
2. Nguzo ni nondo 4 za mm16
1. Vitako
Ili kuavoid wastage, kata vipande vya futi nne nne ambapo katika kila nondo moja nzima utapata vipande 10 na kila base itakuwa ina vipande 12 kwa spacing ya 150mm kila upande (6pcs kwa 6pcs). Hapo katika kila vitako vitano, vitakuwa vinatumia nondo 6 nzima

2. Nguzo za msingi (Startet column)
Kama eneo lako ni flat, kata vipande vya mita nne nne ambapo katika kila nondo moja nzima, utapata vipande vitatu. Katika kila nguzo 3, utatumia nondo 4.

3. Nguzo za Ground floor
Hapa pia fanya kama no. 2 hapo juu, kila kipande kiwe na urefu wa mita nne nne

Kiufupi kila nguzo moja itatumia nondo 4 (kitako, nguzo ya msingi, na ya ground floor)
 
Asante sana mkuu, maelezo yako yamenyooka hata nisie fundi naelewa
 
Back
Top Bottom