jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
Watu humu tunacheka,kutaniana na hata kutukanana some time,lakini nje ya jf ni watu tofauti ukuta wetu ni hizi id tu,tunazotumia but itoshe kusema jamaa alipambana ila mungu ndo hivyo ameamua hakuna kitu kinatia maumivu na kumpa mtu mawazo kama kujua ugonjwa ninao umwa sekunde yoyote nakufa.Dah pole ulijuana naye kwenye connection ka zile story zako nini?
I wish I could join you guys.
Poleni sana
Dah kumbe zile nyuzi zake alikuwa anapambana kupata tiba, Mungu amrehemu aisee, kuwa na ugonjwa usio na hope ya kupona inaumiza, ndugu yangu amewahi wekewa figo mpya bado ana dunda ila alienda nje ya nchi, hapa duniani kitu cha thamani ni afya tu ukikosa solution ndio kuhangaika kokote kuleWatu humu tunacheka,kutaniana na hata kutukanana some time,lakini nje ya jf ni watu tofauti ukuta wetu ni hizi id tu,tunazotumia but itoshe kusema jamaa alipambana ila mungu ndo hivyo ameamua hakuna kitu kinatia maumivu na kumpa mtu mawazo kama kujua ugonjwa ninao umwa sekunde yoyote nakufa.
Money transfer successful! ----- TSH was sent to the mobile 255755155782. NMB ref:EC101024140401. Receipt No: 8HR75S3DP8F
Pole vumilia, lakini saa nane mbona muda uko limited sana dada. Mfano mie nimeona uzi saa hii, na nikiri tu siku hizi sikai na pesa kwa Mpesa, nikitaka kumtumia Mtu naenda na cash kwa wakala (ambaye angalau tumezoeana) ananisaidia kutuma.Leo nimeyavagaa, nitaogeshwa hatari.
Pole vumilia, lakini saa nane mbona muda uko limited sana dada. Mfano mie nimeona uzi saa hii, na nikiri tu siku hizi sikai na pesa kwa Mpesa, nikitaka kumtumia Mtu naenda ba cash kwa wakala (ambaye angalau tumezoeana) ananisaidia kutuma.
Hivyo muda wa kwenda ni wa lunch, mtuvumilie tutaochelewa kutuma. MiMi yangu itawafikia kutoka kwa wakala, mchana inshallah.
Sawasawa.Binafsi eneo la tukio nitaweza kuwepo mpaka saa Tisa Hivi
Baada ya hapo Amu au HoE Anaweza kupokea akapeleka msibani
JF huwa kuna syndicate za utapeli, I personally can sense it from far, lakini kwenye hili jamani liacheni kama haujawiwa kuchangia si lazima.
Si vizuri kuuhusisha msiba huu na utapeli. Kwanza tumepewa taarifa jana, mmeelekezwa kwao kwa wanaotaka kwenda msibani, mmeambiwa msogee muhimbili kwa waliopo au ibadani. Hata ID za wahusika, please ziheshimuni. Hiyo michango mnadhani itakuwa shingapi na wagawane shingapi? Grow up people!
Mkuu mimi naamini msiba upo hawawezi kumsingizia ila picha ya muhusika ingependeza zaidi wazidi kuwaaminisha watu wenye shaka juu ya huu msiba
Mimi naona hili swala linahitaji busara na uvumilivu, hapa JF asilimia kubwa tunatumia fake ID meaning kwamba kila mtu analinda identity yake na Jamii Forums ina jukumu kubwa pia la kulinda Identity za wanachama wake kwa sababu za kiusalama
Ningeomba tuheshimu hilo, wengi hatufahamiani bali tunakutana tu kwenye mijadala na tunaiacha hapa,linapotokea swala la msiba wa mwanachama ningeomba Jamii foruma iweke utaratibu wa kutangaza mwanachama aliefariki lakini swala la kuwachangisha wanaJF naona kama halijakaa sawa unless kuwe na mfuko unaoratibiwa na JF au moderators
Wale wanaofahamiana nje ya Jamii forum ni vizuri mambo ya nje ya JF yakaishia nje ya JF ili kulinda heshima na usiri wa muhusika, suala la msiba ni la kifamilia pamoja na ndugu wa karibu na marafiki walioshibana na sio suala public, kwa hiyo ningeomba wale marafiki wa karibu wa marehemu washirikiane bega kwa bega na ndugu pamoja na familia lakini tusifike mahali tukaoverreact au kubishana kwa sababu ya hili jambo.kumbuka kila mtu ana jisi anavyochukulia mambo ukizingatia kwamba haya ni mambo ya mtandaoni
Wale watakaoguswa kuchangia watachangia lakini naomba Maxence Melo hili suala uliangalia mara mbili na utoe mwongozo kama itatokea in future kwa sababu sioni kama limekua handled properly, kuna mapungufu mengi
Hapa jukwaani tuendelee kubaki kama tulivyo na hakuna haja ya kureveal Identity ya mtu au sensitive information misiba inapotokea.
Natoa pole sana kwa wafiwa na ninaomba tuungane kwa watakaoguswa kuchangia