TANZIA Rambirambi za mwanachama mwenzetu Warumi

TANZIA Rambirambi za mwanachama mwenzetu Warumi

Status
Not open for further replies.
Juma1967,

1:ndugu mbona hilo swala ni la hiari,kwa watakaopendezwa.kwa aliyepo muhimbili na angependa tufahamiane au kujumuika pamoja anaweza nicheki dm still niko muhimbili,huenda huyo anaweza kufanya hayo utakayo ila si mimi.

2:si kila mtu ni mnywaji wa hayo matapu tapu ndugu yangu,na mwenye busara hukaa kimya au kufikiria aongeacho kulingana na sehemu husika,wengi tupo humu jf tukiamini tunakutana watu wenye upeo,maono na kujielewa.jf siyo fb ndugu yangu
 
Dah pole ulijuana naye kwenye connection ka zile story zako nini?
I wish I could join you guys.
Poleni sana
Watu humu tunacheka,kutaniana na hata kutukanana some time,lakini nje ya jf ni watu tofauti ukuta wetu ni hizi id tu,tunazotumia but itoshe kusema jamaa alipambana ila mungu ndo hivyo ameamua hakuna kitu kinatia maumivu na kumpa mtu mawazo kama kujua ugonjwa ninao umwa sekunde yoyote nakufa.
 
Habari za asubuhi,

Nadhani kutoa rambi rambi ni hiyari ya mtu, na hakuna aliela zimishwa kuchangia kwa ajili ya msiba,
Naona watu wana mu attack amu kuwa anataka kutapeli hiyo siyo kweli jamani. Mimi jana nilikua msibani kwa warumi na leo pia nitakuwepo hili swala hakuna utapeli hata kidogo na kama kuna mtu atahisi kuwa ametapeliwa kwa namna yoyote naomba hata mimi niwe responsible on that.

Hili jambo ni ukweli na tunajaribu ku support familia kwa namna tunayoweza, lakini its really sad the response unapata kwa watu. Watu tutaogopa kueleza matatizo yetu hapa aisee kwa namna hii.
 
Watu humu tunacheka,kutaniana na hata kutukanana some time,lakini nje ya jf ni watu tofauti ukuta wetu ni hizi id tu,tunazotumia but itoshe kusema jamaa alipambana ila mungu ndo hivyo ameamua hakuna kitu kinatia maumivu na kumpa mtu mawazo kama kujua ugonjwa ninao umwa sekunde yoyote nakufa.
Dah kumbe zile nyuzi zake alikuwa anapambana kupata tiba, Mungu amrehemu aisee, kuwa na ugonjwa usio na hope ya kupona inaumiza, ndugu yangu amewahi wekewa figo mpya bado ana dunda ila alienda nje ya nchi, hapa duniani kitu cha thamani ni afya tu ukikosa solution ndio kuhangaika kokote kule
 
Umaskini tabu sana jamani tuukatae kwa nguvu zote.
Hivi umelazimishwa kuchanga?? Kama wewe ulikua humjui wapo wanaomjua, kama wewe hufahamiani na wanajukwaa wenzio wapo wanaojuana, sioni ishu ya kutoa mapovu teele wakati hata ungekua unamjua si ajabu usingechanga vilevile.

Toa kiasi ambacho hakitaathiri kipato chako, kama huna kausha, kama huwajui/huwaamini kausha tu.
Yaani watu wazima hivo eti mpaka mods waje wawape muongozo aisee, kwani lazma mwende kama wanajf si muende kama marafiki.
Narudia mnaowajua na kuwaamini changeni, wenye wasiwasi na kuona uzi ni wa kitapeli mnakausha tu, sio poa kabisa wengine wanamdhihaki hadi marehemu sio vizuri tuwe na utu basi.
 
Leo nimeyavagaa, nitaogeshwa hatari.
Pole vumilia, lakini saa nane mbona muda uko limited sana dada. Mfano mie nimeona uzi saa hii, na nikiri tu siku hizi sikai na pesa kwa Mpesa, nikitaka kumtumia Mtu naenda na cash kwa wakala (ambaye angalau tumezoeana) ananisaidia kutuma.

Hivyo muda wa kwenda ni wa lunch, mtuvumilie tutaochelewa kutuma. MiMi yangu itawafikia kutoka kwa wakala, mchana inshallah.
 
Pole vumilia, lakini saa nane mbona muda uko limited sana dada. Mfano mie nimeona uzi saa hii, na nikiri tu siku hizi sikai na pesa kwa Mpesa, nikitaka kumtumia Mtu naenda ba cash kwa wakala (ambaye angalau tumezoeana) ananisaidia kutuma.

Hivyo muda wa kwenda ni wa lunch, mtuvumilie tutaochelewa kutuma. MiMi yangu itawafikia kutoka kwa wakala, mchana inshallah.

Binafsi eneo la tukio nitaweza kuwepo mpaka saa Tisa Hivi

Baada ya hapo Amu au HoE Anaweza kupokea akapeleka msibani
 
JF huwa kuna syndicate za utapeli, I personally can sense it from far, lakini kwenye hili jamani liacheni kama haujawiwa kuchangia si lazima.

Si vizuri kuuhusisha msiba huu na utapeli. Kwanza tumepewa taarifa jana, mmeelekezwa kwao kwa wanaotaka kwenda msibani, mmeambiwa msogee muhimbili kwa waliopo au ibadani. Hata ID za wahusika, please ziheshimuni. Hiyo michango mnadhani itakuwa shingapi na wagawane shingapi? Grow up people!
 
Achana nao
 
Mkuu mimi naamini msiba upo hawawezi kumsingizia ila picha ya muhusika ingependeza zaidi wazidi kuwaaminisha watu wenye shaka juu ya huu msiba

Anayeamini aamini asiyeamini asiamimi. Sio mashindano.

Wewe kama unatoa toa kwa amani iwe kama sadaka tu.

Warumi alipenda anonymity ingependeza ibaki hivyo hivyo.

Ingekua juu yangu location ya msiba, jinsia, na umri vyote nisingetoa zaidi ya taarifa tu kwamba mwenzetu kalala usingizi wa mauti basi. Sio lazima kila mtu aamini.
 
Mimi naona hili swala linahitaji busara na uvumilivu, hapa JF asilimia kubwa tunatumia fake ID meaning kwamba kila mtu analinda identity yake na Jamii Forums ina jukumu kubwa pia la kulinda Identity za wanachama wake kwa sababu za kiusalama

Ningeomba tuheshimu hilo, wengi hatufahamiani bali tunakutana tu kwenye mijadala na tunaiacha hapa,linapotokea swala la msiba wa mwanachama ningeomba Jamii foruma iweke utaratibu wa kutangaza mwanachama aliefariki lakini swala la kuwachangisha wanaJF naona kama halijakaa sawa unless kuwe na mfuko unaoratibiwa na JF au moderators

Wale wanaofahamiana nje ya Jamii forum ni vizuri mambo ya nje ya JF yakaishia nje ya JF ili kulinda heshima na usiri wa muhusika, suala la msiba ni la kifamilia pamoja na ndugu wa karibu na marafiki walioshibana na sio suala public, kwa hiyo ningeomba wale marafiki wa karibu wa marehemu washirikiane bega kwa bega na ndugu pamoja na familia lakini tusifike mahali tukaoverreact au kubishana kwa sababu ya hili jambo.kumbuka kila mtu ana jisi anavyochukulia mambo ukizingatia kwamba haya ni mambo ya mtandaoni

Wale watakaoguswa kuchangia watachangia lakini naomba Maxence Melo hili suala uliangalia mara mbili na utoe mwongozo kama itatokea in future kwa sababu sioni kama limekua handled properly, kuna mapungufu mengi

Hapa jukwaani tuendelee kubaki kama tulivyo na hakuna haja ya kureveal Identity ya mtu au sensitive information misiba inapotokea.

Natoa pole sana kwa wafiwa na ninaomba tuungane kwa watakaoguswa kuchangia
 
Dada umeongea point sana
Watu humu hawaaminiki bora hao kina max wangesimamia hilo swala na pesa ikapelekwa
 
Umaskini unawafanya watanzania wengi kuwa wanyama na wakatili.

Hakuna aliyelazimishwa kuchangia,hii ni hiari yako mwenyewe,isiwe sababu ya kumuona mwingine mwizi au tapeli,kwani umelazimishwaa?!

Acheni kuwakwaza watu wanaofanya jambo ambalo lipo wazi na dhahili kwasababu ya ugumu wa moyo wako.

Mnaoratibu zoezi, hongereni sana na Mungu abariki kazi mnayofanya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom