Poleni wote mlioguswa na msiba huu, poleni wale mliojitolea kusimamia na kuratibu uchangishaji/utoaji rambirambi. Lakini nimeguswa kwa namna ya pekee sijui kwa nini.
Nahisi kama jf tumeidhalilisha familia ya marehemu, the deceased didn't deserve this, kisa buku buku zetu ndio tuwadhalilishe familia kiasi hiki aisee? Ni kama vile marehemu aliomba akifa tumchangie wakati sio, inaumiza sana.
Kuna namna hizi mambo zinahitaji uratibu wa kiofisi, sio kwamba waliohusika kuratibu walikosea au matapeli, no! Ila kwa vile imani kwenye pesa sasa hakuna. Binafsi nikikata kamba hizi mambo kwa kweli hapana, those who know Eli/ERoni personally wanaweza kutoa taarifa, Ila privacy itakuwa jambo lenye heri sana, this isn't fair.