Jamani habari zenu. Nimekuwa busy kidogo na shughuli za kujenga Taifa na kwa sasa niko Mpanda kikazi.
Kuhusu huyu muungwana tunayetaka aachie ngazi naomba kuwamegea mawili matatu ambayo bila shaka tukichanganya na mengi yalisemwa juu yake yanaweza kabisa kutusaidia kufikia uamuzi.
Huyu jamaa ni mcheshi, hupenda kujichang'anya watu, ni mtu mkarimu sana, husikiliza kwa makini sana, huchambua mambo kiundani kabla ya kutoa uamuzi, si mwoga hata kidogo kutoa ushauri, ana management skills and ability, anakubali mabadiliko.
Kwa taarifa yenu toka amechukua kitengo hicho kumekuwa na mabadiliko makubwa sana. Ameleta ufanisi katika kazi kwa kuwapa vijana wake vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi na kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi.
Mambo haya ya kuwafichua wezi na mafisadi ni moja ya juhudi zake kwani si mtu anayependa uchafu kama huo hata kidogo. Kuna vitu anasemwa kwamba hakufanya wakati alipokuwa London kama Field Officer, kuna ushaidi kwamba hakufanya kazi yake?. Ni imani kubwa sana alifanya kazi yake lakini hakusikilizwa na hasa kama mapesa yaliyokuwa yanawekwa huko Great Britain yalikuwa ya dili la Rada na katika kipindi cha Mkapa (Mbabe). Ningeomba tumuhukumu kwa kufuata haki na vilevile tumpe muda kwani ni muda mchache sana toka amechukua ofisi.