Kwa mara ya kwanza kabisa nitashiriki katika kongamano la KATIBA MPYA hapa kwa dhumuni maalum lenye kutoa fursa ya mawazo mbadala nje ya rasimu ama ile ilopendekezwa ambayo muda sii mrefu mchakato wake utaanza.
Ni matumaini yangu kuwa sii Wananchi wote walopata fursa ya kuchangia mawazo ama maoni yao katika dai la Katiba Mpya. Aidha wapo pia ambao maoni yao hayakupewa umuhimu kwa sababu hayakupata kuungwa mkono na watu wengi japo yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kuzingatiwa na ndio ikawa sababu kubwa ya kuahirishwa upatikanaji wa Katiba Mpya.
Katiba ni Sheria mama, haihitaji matakwa ya Vyama vya siasa, Utashi wa Viongozi ama matamanio ya Wananchi isipokuwa huzingatia HAKI, UHURU, FURSA, MIIKO na MAADILI ili kulinda UTU wa Mtanzania kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.
Binafsi, nitaorodhesha baadhi ya sehemu ambazo naziona zina utata lakini muhimu sana na zinahitajika kuangaliwa kwa makini sana ili tupate suluhisho la Katiba yenye kukidhi Mahitaji ya Jamhuri.
Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-
1. MUUNGANO
2. MUUNDO WA SERIKALI
3. MADARAKA YA RAIS
4. UKOMO WA VIONGOZI
5. VYOMBO VYA USALAMA
6. DEMOKRASIA
7. MIIKO NA MAADILI
8. UHURU NA HAKI ZA WANANCHI
9. MASLAHI YA TAIFA
Najaribu kukusanya mawazo yetu nikiwa na lengo la kutazama ni jinsi gani hata sisi tunaweza kufikia muafaka katika maono yetu kwa kuzingatia Utu na Maslahi mapana ya Taifa. Nitajikita zaidi upande wa pili kwa hiyo jiandaeni malumbano - HOJA hujibiwa kwa HOJA..
Karibuni - Tuanze na hoja ya kwanza.