Rasimu ni maoni sio Katiba

Rasimu ni maoni sio Katiba

Mkandara

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,806
Reaction score
9,011
Kwa mara ya kwanza kabisa nitashiriki katika kongamano la KATIBA MPYA hapa kwa dhumuni maalum lenye kutoa fursa ya mawazo mbadala nje ya rasimu ama ile ilopendekezwa ambayo muda sii mrefu mchakato wake utaanza.

Ni matumaini yangu kuwa sii Wananchi wote walopata fursa ya kuchangia mawazo ama maoni yao katika dai la Katiba Mpya. Aidha wapo pia ambao maoni yao hayakupewa umuhimu kwa sababu hayakupata kuungwa mkono na watu wengi japo yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kuzingatiwa na ndio ikawa sababu kubwa ya kuahirishwa upatikanaji wa Katiba Mpya.

Katiba ni Sheria mama, haihitaji matakwa ya Vyama vya siasa, Utashi wa Viongozi ama matamanio ya Wananchi isipokuwa huzingatia HAKI, UHURU, FURSA, MIIKO na MAADILI ili kulinda UTU wa Mtanzania kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.

Binafsi, nitaorodhesha baadhi ya sehemu ambazo naziona zina utata lakini muhimu sana na zinahitajika kuangaliwa kwa makini sana ili tupate suluhisho la Katiba yenye kukidhi Mahitaji ya Jamhuri.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-

1. MUUNGANO
2. MUUNDO WA SERIKALI
3. MADARAKA YA RAIS
4. UKOMO WA VIONGOZI
5. VYOMBO VYA USALAMA
6. DEMOKRASIA
7. MIIKO NA MAADILI
8. UHURU NA HAKI ZA WANANCHI
9. MASLAHI YA TAIFA

Najaribu kukusanya mawazo yetu nikiwa na lengo la kutazama ni jinsi gani hata sisi tunaweza kufikia muafaka katika maono yetu kwa kuzingatia Utu na Maslahi mapana ya Taifa. Nitajikita zaidi upande wa pili kwa hiyo jiandaeni malumbano - HOJA hujibiwa kwa HOJA..

Karibuni - Tuanze na hoja ya kwanza.
 
Nimefungua mjadala huu ili sote tupate kujua yapi mapendekezo ya Wana JF katika kudai KATIBA MPYA. Kesho msianze kudai sijui Muungano hatuutaki, tunaitaka Tanganyika, sijui rais ana madaraka makubwa sana! Njooni tujadili sote hapa!

Isije tokea siku ya mchakato ndio mkaanza kuwa nyuma ya mashinikizo ya Ukanda, Vyama, na Wanasiasa.

Hoja yako inaweza toka eneo lolote kati ya hayo tisa tukaanza kuijadili.
Mimi kazi yangu itakuwa kutazama upande wa pili wa sarufi.
 
Hatua ya kwanza ni kujadili muundo na ushiriki wa kukusanya maoni hadi kuandaa rasimu bila wanasiasa kuhodhi uelekeo wake. Makundi yote yaamue hatma ya Taifa letu kwa uhuru.

Wanasiasa wana influence juu ya kupatikana kwa katiba lakini ni muhimu kuwe na mechanisms ya kuwadhibiti ajenda zao zisijekugeuka ndio ajenda za wananchi wote kwa kushawishi makundi yenye uelewa mdogo.

Rasimu ya Warioba ilifeli, sababu zinajulikana na fedha nyingi zilitumika. Ajenda na hatua kuelekea katiba mpya ziwekwe wazi badala ya wanasiasa kujifungia vyumba vya siri kutupangia hatma yake.
 
Umepigilia msumali na ndio sababu haswa ya kutaka mjadala maana inaonekana kuwa swala la Katiba Mpya linachukuliwa Kisiasa zaidi.
 
Kwa upande wangu naamini katika serikali 1 sio 3 wala 2

Kama tumeamua kuungana basi tuungane hadi rohoni pia tuwe mwili m1

Haya mambo ya kuwaza serikali mbili au tatu ni kuwaongezea gharama waTanzania.
Kuwa na Serikali MOJA ni hoja ambayo ingependwa na wananchi wengi lakini haina nguvu ya Kisiasa(Kiutawala) kwa sababu sisi bado tuna Fikra za Kutawaliwa ambazo ndio chimbuko la UBAGUZI. Sioni uwezekano wa Tanzania kuwa na Serikali 1 zaidi ya pendekezo la Serikali 3 ambazo zinaakisi Ubaguzi ulotanguliwa na mipaka ya mkoloni
 
Wanaowaza serikali mbili na tatu kwa upande wangu nawaona wakiangalia zaidi madaraka zaidi ya umoja.

Ndio maana nasema kama kweli tunataka tuwe kitu kimoja tuwe na serikali 1,TRA iwe na nguvu hadi Zanzibar.

Tuungane kiroho zaidi yaani tuwe wa1 kabsa hizi serikali mbili au tatu zimekaa kibaguzi sana na zina manung'unuko mengi sana ambayo kila upande unaona hautendewi haki.

Kwa upande wangu nawaona Wazanzibar ni ndugu zangu kabsaa na nataka tuwe na serikali 1 kusiwe na ubaguzi wa ukinunua kitu Zanzibar unakuwa kama vile umekinunua Uganda.
 
nimekuelewa pengine tupate mwenye hoja ya 2 au 3. Hata mimi naamini Uwepo wa Serikali 2 ndio kumezua Uzanzibar haswa pale rais akitoka bara.

Leo hii sijasikia kabisa kero za Muungano lakini subiri kesho atakapo kuwa Rais kutoka Bara.

Hii ni dalili tosha kabisa kwamba serikali 2 zimetugawa watu wa bara na visiwani japo Wazanzibar wanadai muungano wa shirikisho, hawataki Bara kuimeza Zanzibar! Hoja kuu ni NCHI sio WATU.

Lakini kama tumeweza kufuta kabisa UTanganyika kiasi kwamba wabara wote wanajiita Watanzania bila shaka kuna uwezekano wa hata UZanzibar kuondoka tukiwa na Serikali moja.

Lengo na sababu haswa ya MUUNGANO ni kuunganisha watu wake, laa haina maana kuwa na Muungano ambao bado unawatenganisha Watu wa huku na kule.
 
Kwa mara ya kwanza kabisa nitashiriki katika kongamano la KATIBA MPYA hapa kwa dhumuni maalum lenye kutoa fursa ya mawazo mbadala nje ya rasimu ama ile ilopendekezwa ambayo muda sii mrefu mchakato wake utaanza.

Ni matumaini yangu kuwa sii Wananchi wote walopata fursa ya kuchangia mawazo ama maoni yao katika dai la Katiba Mpya. Aidha wapo pia ambao maoni yao hayakupewa umuhimu kwa sababu hayakupata kuungwa mkono na watu wengi japo yalikuwa na umuhimu mkubwa wa kuzingatiwa na ndio ikawa sababu kubwa ya kuahirishwa upatikanaji wa Katiba Mpya.

Katiba ni Sheria mama, haihitaji matakwa ya Vyama vya siasa, Utashi wa Viongozi ama matamanio ya Wananchi isipokuwa huzingatia HAKI, UHURU, FURSA, MIIKO na MAADILI ili kulinda UTU wa Mtanzania kwa Maslahi mapana ya Taifa letu.

Binafsi, nitaorodhesha baadhi ya sehemu ambazo naziona zina utata lakini muhimu sana na zinahitajika kuangaliwa kwa makini sana ili tupate suluhisho la Katiba yenye kukidhi Mahitaji ya Jamhuri.

Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-

1. MUUNGANO
2. MUUNDO WA SERIKALI
3. MADARAKA YA RAIS
4. UKOMO WA VIONGOZI
5. VYOMBO VYA USALAMA
6. DEMOKRASIA
7. MIIKO NA MAADILI
8. UHURU NA HAKI ZA WANANCHI
9. MASLAHI YA TAIFA

Najaribu kukusanya mawazo yetu nikiwa na lengo la kutazama ni jinsi gani hata sisi tunaweza kufikia muafaka katika maono yetu kwa kuzingatia Utu na Maslahi mapana ya Taifa. Nitajikita zaidi upande wa pili kwa hiyo jiandaeni malumbano - HOJA hujibiwa kwa HOJA..

Karibuni - Tuanze na hoja ya kwanza.
Muundo wa muungano wa ukweli ni wa serikali 3; serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanganyika, na Serikali ya Muungano

Tanganyika ishughulike na mambo yake kama ilivyo sasa kwa Zanzibar kisha kuwe na serikali ya kushughulikia mambo ya pamoja
 
URAIS
1. a) Watu wanaogombea urais wasiwe wanachama WA chama cha siasa. Kwa kuwa majukumu ya urais hata akipita huwa ni rais WA wote hili litaepusha vivutano isiyo na maana na ubaguzi. Mfano Magufuri alionesha waziwazi kupendelea chama chake na kuwataka wananchi wasiwachague wengine Bali chama chake na alisema hatapeleka maendeleo wakichagua mwingine! Yeye atakuwa mwezesha uzalendo na maendeleo ya nchi na mbeba utamaduni, desturi, maono na dira ya taifa.

1b) kutakuwepo dira ya taifa na Sera ya taifa ya maendeleo kwa muda WA kipindi cha kinacholingana na kipindi cha urais ktk miaka 5 au 10. Na kitengo maalum cha kusimamia dira na Sera ya maendeleo kitakachofanya kazi kizalendo na kupenda maendeleo ya nchi. Kabla ya kupanga kitapokea mapendekezo kutoka kwa wananchi mojakwamoja au kupitia wawakilishi. Wakati WA kapeni mgombea urais na ubunge na udiwani hakutakuwa Sera zao au za vyama bali wataeleza kwa wananchi namna wayakavyotekeleza na kusimamia na kuwezesha utekelezaji WA dira na Sera ya taifa itakavyokuwa ili kupigiwa kura. Hii itaondoa uholela WA rais kupanga na kutenda aonavyo tu au kwa kutumia tu Sera ya chama chake tu isiyoendana maranyingi na dira na Sera ya kitaifa kama ilivyo sasa.

2. Urais utapaswa kuwekewa masharti mahususi na sifa mahususi za MTU anayeutaka urais. Na atalipwa sana ili asiwe na tamaa ya kufanya rushwa na ufisadi.

3. Rais hatahusika na uteuzi WA wakuu WA mihimili mingine. Mihimili itajichagulia wakuu wake bila rais kuhusika ili kuwezesha Uhuru WA maamuzi kiweredi sio kama rais apendavyo. Hii imeoneshwa na jaji mmoja aliyelalamika kuwa kuna kiongozi WA serikali alichana hukumu yake ambayo haikumpendeza. Na kuondoa dhana ya mhimili WA serikali kujichimbia zaidi kama magufuri alivyosema.

4. Ubunge na udiwani uwe kwa kupitia chama au wagombea huru.uraisi hauna chama. Yeye WA wote(watanzania wenyechama na wasiona vyama)

NB. MAONI HAYA YANALENGA UMOJA NA UZALENDO KWA TAIFA SIO KAMA SASA UMOJA HAKUNA NA UZALENDO HAKUNA( ISHARA NI MIVUTANO, UDIKITETA,UBAGUZI, UFISADI NA MENGINE MENGI TULIYOPITIA HASA AWAMU YA MAGUFURI
 
Labda nikuulze hivi. Mambo ya Tanganyika ni yapi hayatekelezwi leo? na Je, kuwepo Serikali 2 kinachopungua hapo ni kipi kama sii jina la Tanganyika maana kama ni utawala wa Mawaziri tunao mpaka manaibu na manispaa.

Labda nikupe fununu kidogo, tu. Nchi zilogawana majimbo zjna Serikali kubwa sana kwa maana ya Watumishi wake. Mfano, tukiwa na Serikali 3 hiyo Tanganyika italazimika kuwa na Wabunge 428 badala ya 214 ili.kuwakilisha majimbo yao kwenye Bunge la JMT na Bunge la Tanganyika. Tutalazimika kugharamia viongozi wote ngazi ya Tanganyika na ngazi ya Kitaifa.

Kwa nchi maskini kama yetu kesho tutadai Majimbo maana mikoa ya Kanda ya ziwa au kusini watapata hoja kwa sababu 2. Kwaza utajiri wao wa dhahabu au gas! Na pili Kujitawala! Hili neno kujitawala hubeba ubaguzi ulonakshiwa. Je, tuko tayari kupambana na hali hiyo ikitokea?

Kama nilivyosema. Lengo la kuunganisha NCHI hizi mbili ni WATU kama vile wazazi wawili wanapofunga ndoa basi kizazi chao huwa na Ubin mmoja. Tukianza kusema kuna Qatanzania na Wazanzibar, Itakuja Wasukuma na Wazaramo maana unarudisha kuitazama zaidi mipaka badala ya Watu..
 
URAIS
1. a) Watu wanaogombea urais wasiwe wanachama WA chama cha siasa. Kwa kuwa majukumu ya urais hata akipita huwa ni rais WA wote hili litaepusha vivutano isiyo na maana na ubaguzi. Mfano Magufuri alionesha waziwazi kupendelea chama chake na kuwataka wananchi wasiwachague wengine Bali chama chake na alisema hatapeleka maendeleo wakichagua mwingine! Yeye atakuwa mwezesha uzalendo na maendeleo ya nchi na mbeba utamaduni, desturi, maono na dira ya taifa.

1b) kutakuwepo dira ya taifa na Sera ya taifa ya maendeleo kwa muda WA kipindi cha kinacholingana na kipindi cha urais ktk miaka 5 au 10. Na kitengo maalum cha kusimamia dira na Sera ya maendeleo kitakachofanya kazi kizalendo na kupenda maendeleo ya nchi. Kabla ya kupanga kitapokea mapendekezo kutoka kwa wananchi mojakwamoja au kupitia wawakilishi. Wakati WA kapeni mgombea urais na ubunge na udiwani hakutakuwa Sera zao au za vyama bali wataeleza kwa wananchi namna wayakavyotekeleza na kusimamia na kuwezesha utekelezaji WA dira na Sera ya taifa itakavyokuwa ili kupigiwa kura. Hii itaondoa uholela WA rais kupanga na kutenda aonavyo tu au kwa kutumia tu Sera ya chama chake tu isiyoendana maranyingi na dira na Sera ya kitaifa kama ilivyo sasa.

2. Urais utapaswa kuwekewa masharti mahususi na sifa mahususi za MTU anayeutaka urais. Na atalipwa sana ili asiwe na tamaa ya kufanya rushwa na ufisadi.

3. Rais hatahusika na uteuzi WA wakuu WA mihimili mingine. Mihimili itajichagulia wakuu wake bila rais kuhusika ili kuwezesha Uhuru WA maamuzi kiweredi sio kama rais apendavyo. Hii imeoneshwa na jaji mmoja aliyelalamika kuwa kuna kiongozi WA serikali alichana hukumu yake ambayo haikumpendeza. Na kuondoa dhana ya mhimili WA serikali kujichimbia zaidi kama magufuri alivyosema.

4. Ubunge na udiwani uwe kwa kupitia chama au wagombea huru.uraisi hauna chama. Yeye WA wote(watanzania wenyechama na wasiona vyama)

NB. MAONI HAYA YANALENGA UMOJA NA UZALENDO KWA TAIFA SIO KAMA SASA UMOJA HAKUNA NA UZALENDO HAKUNA( ISHARA NI MIVUTANO, UDIKITETA,UBAGUZI, UFISADI NA MENGINE MENGI TULIYOPITIA HASA AWAMU YA MAGUFURI
Niongezee Kwa kusema tu, mgombea uraisi asiwe amejihusisha nachama chochote Kwa Zaid ya miaka 10 mpaka 15 kuelekea uchaguzi.
 
Ninekusoma lakini huoni kama unapendekeza Ukomunist wa.iana yake? Tofauti yake umeondoa neno CHAMA lakini kama rais atakuwa hana CHAMA ina maana hana ITIKADI isipokuwa Kufuata KATIBA ambayo haina mrengo. Hii itakuwa kanyaga twende.

Ya Magufuli inatojana na kuwepo Demokrasia maana kila Chama kinataka.kuwa madarakani. Iwe Upinzani au Chama tawala, demokrasia ina ukakasi wa ubaguzi baina ya vyama na watu.

Walomchukia Magufuli bila shaka pia walikichukia Chama kwa sababu asingeweza kuitekeleza Ilani ya Chama chake pasipo viongozi watekelezaji kutoka chama chake. Hii asili ya kuwa na demokrasia ya vyama vingi ambayo wabunge huteuliwa na Wananchi kwa kuzingatia ilani ya Chama husika.

Pili, Tatizo lake linaweza kutupa rais alotokana na Umaarufu wake wakati hana sifa ya Uongozi. Pili itatupa uwezekano mkubwa wa kuwa na rais Dikteta kwa sababu faslafa ni yake yeye alojitungia.

Hapa kuna hatari ya maneno ya mzee Mwinyi kuwa kila Zama na Kitabu chake. Binafsi napingana kabisa na fikra hizi kwa sababu haiwezekani nchi yetu kupata maendeleo ama kufanikisha miradi ikiwa kila rais anayeingia madarakani anakuja na mipango yake.
Wewe unaonaje, Ina make sense?
 
Rasimu ya Warioba irudi mezani, tufanye marekebisho kidogo,

Tuutafute mfumo mzuri wa kuwapata wajumbe wa Bunge maalum la Katiba mpya.

Kisha ipigwe kura ya maoni, na izaliwe KATIBA mpya.

Bring back our WARIOBA 💪💪💪.
 
nimekuelewa pengine tupate mwenye hoja ya 2 au 3. Hata mimi naamini Uwepo wa Serikali 2 ndio kumezua Uzanzibar haswa pale rais akitoka bara.

Leo hii sijasikia kabisa kero za Muungano lakini subiri kesho atakapo kuwa Rais kutoka Bara.

Hii ni dalili tosha kabisa kwamba serikali 2 zimetugawa watu wa bara na visiwani japo Wanzanzibar wanadai muungano wa shirikisho, hawataki Bara kuimeza Zanzibar! Hoja kuu ni NCHI sio WATU.

Lakini kama tumeweza kufuta kabisa UTanganyika kiasi kwamba wabara wote wanakjiita Watanzania bila shaka kuna uwezekano wa hata UZanzibar kuondoka tukiwa na Serikali moja.

Lengo na sababu haswa ya MUUNGANO ni kuunganisha watu wake, laa haina maana kuwa na Muungano ambao bado unawatenganisha Watu wa huku na kule.
Ahsante Mkandala hebu fikiria mkoa wa Arusha ulikussanya kodi TRA bilioni 450 bilioni na bila kujumuisha utalii na 2022 na Zanzibar bilioni 250 yet Zanzibar wana wabumge 80 bungeni NA MKOA WA arusha una wabunge 10 Dodoma ni mtu gani wa Arusha atakubali hali hii? KAMA WANA CHA KUCHANGIA MUUNGANO HUU BASI NI WAJIBU SII KUGAWIWA TU WEMGI WA BARA HAWATAKI HALI HII
 
Rasimu ya Warioba irudi mezani, tufanye marekebisho kidogo,

Tuutafute mfumo mzuri wa kuwapata wajumbe wa Bunge maalum la Katiba mpya.

Kisha ipigwe kura ya maoni, na izaliwe KATIBA mpya.

Bring back our WARIOBA 💪💪💪.
Rasimu ya Warioba ipo, wewe kama mwananchi una mawqzo gani tofauti katika mapwndekezo ya sura ibara zike. Kumbuka sisi wote tuna mitazamo tofauti na hatukubaliani kwa mengi na ndio maana rasimu ile ilisukumwa uvunguni. Je, leo hii tutawezaje kupata suluhu katika Mambo yale yale yalokwama mwanzoni pasipo hata kuwafikia Wananchi.
 
Back
Top Bottom