Ngoja tujijuzee, then wakati watu wanoatoa hoja, tufanye unyambulisho yakinifu. Prof. Asante kwa kuiweka hapa, sasa ni kazi kwetu. Natoa wito wanajamii tuisome, tuipitie kipengele kwa kipengele, ili tujue tunavyoongozwa, na miiko ya uongozi, pamoja na haki zetu. Cha msingi siyo kuipinga, bali ni kuirekebesha pale tunapoona hapatufai, tutaweza kufanya hivyo kwa kutoa hoja za kuijenga Tanzania na wala si kwa kugoma, ama kuikataa.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba, tayari gharama kubwa imeshatumika, hatuwezi kuita tena Bunge Maalumu, bali ni kufanya marekebisho zile sura ambazo hazijakaa sawasawa.
Nawakilisha