bunge la muungano litakuwa na wabunge 75 tu. baraza la wawakilishi litakuwa kama kawa na tanganyika itakuwa na wabunge wake ambao watakuwa na bunge lao kama lilivyo baraza la wawakilishi zenji
Watanzania wanapenda mazingaombwe sana; kwa kadiri ambavyo nimefuatilia kwa juu juu na nikiendelea kusubiri kuona rasimu yenyewe ya hiyo Katiba mwitikio wangu ni tahadhari.
Ninaomba nichukue fursa hii kumpongeza joseph sinde warioba kwa kumaliza kukamilisha rasimu ya katiba na hasa kututengenezea katiba isiyolenga kutubagua watanzania kwa misingi mbalimbali mf. ukabila,udini nk. Japokuwa kunamapungufu ya hapa na pale lakini ninaimani mabaraza ya katiba yatafanya kazi yake vizuri na kurekebisha mapungufu hayo. HONGERA SANA WARIOBA
kifo cha ccm kimewadia,sasa rais kushtakiwa na bunge,viti maalum hakuna, pamoja na mengi mazuri kali ni kuwa mbunge akifariki,mrithi atatoka chama alichokuwa aliyefariki,hapa kuna tatizo kwani ni sawa na kuamini wananchi walichagua chama na si mtu kwa sifa na uwezo wake,pia ni kuamin anayepewa nafasi anakubalika na pia ni kuwanyima haki za msingi watu wanaopenda na wenye nia ya kuleta maendeleo. My intake: Tusitishwe na gharama za uchaguzi kwa kumteua mtu asiyefaa.
Hapo umeneno wana assume kama vile hakutakuwa na mgombea binafsi asiyekuwa na chama huyo nani atamrithi, au watatakiwa kuacha wasia wa nani atarithi kiti chake, hili jambo ni la ovyoo, demicrasia lazima iheshimiwe, watu wachague viongozi hii nchi democrasia ndo inakua hata kupiga tu kura watu bado hawajitokezi kuache kuweka vichocheo vya kukuza voter apathy nchini ni kosa kubwa! Akifa/akijihudhuru au kwa namna yoyote nafasi ya kuchaguliwa yoyote ikibaki wazi lazima uchaguzi ufanyike, hii ndo gharama ya democracy!
Jina Tanganyika lisikuchanganye kwani hata hilo jina lenyewe ni la wajerumani (siyo waafrika waiolichagua) na sijui walitoa wapi hilo jina hawa wajerumani! Nchi nyingi zimebadili majina ya nchi zao na hivyo jina si hoja ya msingi sana tunaweza hata kuwa na jina lingne badala ya hilo la tanganyika ambalo pengine hata wewe hujui asili yake ila unashahabikia tu! Hoja ya msingi hapa ni taifa huru lenye katiba bora na uongozi madhubuti! na nadhani hata kwenye maoni hili suala la jina la nchi (Tanganyika) lijadiliwe na kutoa nafasi ya kupendekeza jina lingine kama itaonekana kuna sababu za msingi za kufanya hivyo!what is this animal "tanzania bara"????????????????????????????????????????
We need our tanganyika, i cant wait kuwa mwana tanganyika jaman.
Acha kukurupuka kanga weee!!! Siyo kudandia gari kwa mbele! Sikiliza lecture yote kwanza kabla ya kuanza kuuliza ugolo!Hapo ni ujinga mtupu. Jimbo kuwa na wabunge wawili kwa maslahi ya nani na kuwakilisha nani? na raisi anakuwa na wabunge kuwakillisha nini?. inamaana tutakuwa na wbunge zaidi ya 700 na gharama za kufuga wadudu hao zitalipwa nani.Wanawake wanaweza na wamekwisha jiwezesha waingie kupambana.Lazima mihimili hii iwe tofauti.
Mkuu naelewa. Ninachoona mimi ni kuwa huu mchakato wa katiba umefanywa ovyo kabisa ili 2015 ama tusiwe na uchaguzi, au tutumie ile ile katiba ya zamani.
Hebu jiulize; Mwaka 2014 hii katiba ya shirikisho ikikamilika, je 2015 Watanganyika tutapiga kura kuchagua viongozi wetu kwa kutumia sheria ipi? Tutatumia katiba ipi? Hiyo katiba itatengenezwa lini? Tume ya kutengeneza hiyo katiba itaundwa na nani? Endapo "Tanganyika" hatutafanya uchaguzi 2015, Je tutachagua raisi wa shirikisho na wa Zanzibar? Baada ya hapo Tanganyika itakuwa inaongozwa na nani (Kumbuka serikali ya shrikisho itahusika na mambo 7 tu)?
Hapo kwenye mawaziri nakupinga kidogo. Raisi lazima awezekupanga safu yake. Muhimu ni bunge liweze kuthibitisha uteuzi huo. Sasa hata akishindwa kuteua mawaziri itakuwaje hapo?
Tunakoenda ni mbali na ni kugumu zaidi kuliko tulipo sasa!
tumebimefanya kazi nzuri ila hapo kwenye wabunge wawili kila jimbo hapana hatuwezi kukubaliana na upuuzi wa namna hii, hii ni katiba kwa miaka 50 ijayo isiandikwe kuwasaidia kina sophia simba kurudi bungeni na kuwaachia watoto zetu urithi mbaya kana kwamba tulikuwa mazezeta. Nasema no wabunge wawili kwa jimbo moja.
Tungevunja na Muungano kabisa ili hawa Wazanzibar waendelee na mambo yao kule visiwani ikiwemo Serikali kulazimisha watu hata wasio waislam kushirika mambo ya Waislam kama kufunga biashara za chakula, kutokula hadharani as if ni nchi ya Kiislam, GO ZANZIBAR GO!!!!!!!!Link 1. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/100638-shirikisho-ndani-ya-shirikisho.html
Link 2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiinimacho-cha-muungano.html
Leo ni siku ambayo Jaji Warioba ameamua/amelazimika kuondoa usanii wa "Tanzania bara"/"wabara". Warioba anaondoka na ukiini macho wake. Tanganyika inasikika tena.
Leo ni siku mbaya kwa MJJ na Maalim Nguruvi3. Naomba mjizoeshe tena kuitaja "Tanganyika"
Wadanganyika tunabadili jina hili rasmi na kuchukua hadhi yetu,"Watanganyika"
Tanganyika Tanganyika, nakupenda kwa moyo wote.
Je shirikisho la Tanzania litatokana na majimbo mawili au nchi mbili?
Tanganyika na Zanzibar zitakuwa nchi ndani ya muungano au zitakuwa ni majimbo ya muungano?
Mizengo Pinda-"Zanzibar si nchi"
J: Kikwete " Zanzibar ni nchi ndani, sio nchi nje"
"Tanganyika ni nchi.Tanganyika si nchi ndani, ni nchi nje." - Rasimu ya Katiba mpya.
Sasa Katiba ya Tanganyika itatengezwa lini? ama ndio hiyo? hahahahahah, kazi kweli kweli, ikiwa ni serikali tatu. sasa hapa ndio niliposema Think Tank hii inaiona Zanzibar Nachingwea, Zanzibar Kwanza kubembelezana baadae.
Zanzibar nao watataka serikali ya pemba na unguja