RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Nadhani ajitolee mtu hapa JF aanzishe thread ya mapendekezo ya marekebisho, kila mtu aweke maoni yake humo ili watu wa tume iwe rahisi kuyapata...
 
hii rasimu 50% iko safi 50% ni upuuzi,rais amebaki kuwa kama mfalme,warioba ana matatizo kichwani,na pia nanusa harufu ya kuendelea kuwa na rais dhaifu madarakani hadi 2017 kutokana na makosa ya makusudi katika hii rasimu,and by that time zitto na january watakuwa 40 years old,hesabu za ------ zitakuwa zimetimia.
 
Mmmmh! Watu mna maono..! Hii inaweza kuwa kweli.
 
Hivi kwa nini watanzania huwa hatutaki kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa? WABUNGE WAWILI KILA JIMBO,MWANAMKE NA MWANAUME...! huu ni upumbavu wa hali ya juu. hapa naona wanataka katiba ihalalishe viti maalumu kwa njia nyingine. kwani kinachoongoza watu ni kuwa na jinsia ya kike au ya kiume au ni uwezo wa mtu?
 
kutakuwa na baraza la wawakilishi la tanganyika na zanzibar na viongozi wakuu watajulikana kama Gavana wa tanganyika.
 
Mimi sikubaliani na jina Tanzania Bara. Jina letu ni Tanganyika
 
Hii mambo ya men and women representatives hayafai. Mtu mmoja anatosha
 

We hasten to add that "Tanzania Bara" is not synonymous with Tanganyika. Indeed, Tanzania Bara is the same geographical region as Tanganyika Bara. It is the non coastal part of Tanzania. The opposite of "bara" is not island. It is coastal.
 
We hasten to add that "Tanzania Bara" is not synonymous with Tanganyika. Indeed, Tanzania Bara is the same geographical region as Tanganyika Bara. It is the non coastal part of Tanzania. The opposite of "bara" is not island. It is coastal.

Wewe unataka wakivunja muungano - watavunja, it is a matter of time- wachukue Tanga, Bagamoyo, Dar na Ukanda na maili 16 za pwani kwa sababu si "Tanzania bara" kihistoria .

Ndo yaleyale aliyochelea Nyerere.

Mara tu watu wa ukanda huu wa pwani nao waseme sie si wa bara wala wa visiwani, tunataka serikali yetu na sie!
 
Hawa wakuu wa mikoa na wilaya wasiwepo,na jaji angechaguliwa na wananchi nasio raisi,na wabunge wa kuteuliwa wasiwepo,Rais ashitakiwe ata akiwa madalakani.
 
Wakuu wa mikoa na wilaya wasiwepo,Jaji achaguliwe na Wananchi,Rais ashitakiwe ata akiwa madarakani,Wabunge wa kuteuliwa wasiwepo,Mawazili wachaguliwe nasio kuteuliwa.
 
Wadau nisaidieni hapa!

Kwa mujibu wa rasimu ya katiba mpya kuna Waandamizi wa serikali yetu ambao watatakiwa kuchaguliwa nje ya vyama vya siasa.

Kinachonitatiza ni kuwa sijawahi kukutana na mtu asiyekuwa na Political affiliation ya upande fulani kulingana na vyama vya siasa vilivyopo sasa nchini.

Kwa mfano Wanajeshi, Polisi au watu wa fani ya sheria na Mahakama wamejionyesha mara kadha kuwa na mvuto na vyama fulani vya siasa.

Je uteuzi wa nafasi hizi utafanyikaje ili kuwapata watu ambao kiitikadi ni 'nyutro' kabisa?
 
Wapo watu wengi tu ambao hawana affiliation na chama kimojawapo cha siasa. Inawezekana wakawa na vitu kadhaa ambavyo wanakubaliana na chama fulani lakini kukawa na vitu vingi tu ambayo hawavikubali katika chama husika. Wengi wetu tunapenda demokrasia na tunataka kuona mabadiliko (read: maendeleo), bila kujali sana yanaletwa na chama gani.

Wengine unaweza kuona wanafanya mambo fulani kwa ajili ya kulinda au kupata maslahi fulani ama binafsi. Na ndio hapa unapata wanaCDM waliomo CCM na pia wanaCCM waliomo CDM (kwa mfano tu!)
 
hapo mkuu inategemeana ila sidhani lakini TUKUMBUKE KINGUNGE NI MPAGANI NA HANA DINI YOYOTE,LABDA WATU KAMA HAO WANAWEZA KUEPO HAPA NCHINI.
 

Hii rasimu mbona tunaifurahia sana? Ngoma nzuri ni KATIBA ya TANGANYIKA a.k.a TANZANIA BARA. Hii ya MUUNGANO kama zitakuwepo serikali tatu haina tija sana. Tusubiri ya Tanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…