Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
It is vey funny kuendeleza ufalme wa Rais.tanzania mpya inazaliwa wakuu, very funny
Kwa nini madaraka ya Raisi yapunguzwe, mimi kama Mtanzania sitaki yapunguzwe na nina haki, hivyo ni sawa tu kwa Upande wangu!
walitakiwa wafutwe rasmi hamna cha kujadili wala nini...........Kuhusu ma RC na ma DC hilo si swala la muungano litajadiliwa na serikali husika kama kuna ulazima wa kuendelea kuwepo.
Ndio maana inaitwa rasimu siyo final inapelekwa kwenye mabaraza ya Katiba kujadiliwa, ila ndo hivyo hayo mabaraza 98% ni makanda wa CCM! tegemea vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya kuibuka with flying clours!Pamoja na mapendekezo mengi kwenye TUME kuwa mazuri, lakini bado kuna mapangufu makubwa, mfano madaraka ya rais bado hayajaainishwa vizuri, RAIS kuteua majaji, kwanini huo Mhimili usiteuwe wenyewe na mambo mengine mengi.
Swali langu je hii rasimu inaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kupigiwa kura ya NDIYO NA HAPANA?
Kweli mkuu, inatakiwa katiba hii ya muungano itamke wazi serikali tatu ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar. Hapa wametegeshea ili wavune tena pesa za kuedit katiba ya muungano kwa kutoa jina Tanzania Bara na kuweka Tanganyika. Mwenye macho haambiwi tazama.Hakuna serikali ya Tanzania Bara, tunahitaji ya Tanganyika!
Sera za chama zinaweza kuwa mashairi matamu sana yenye watakelezaji wabovu. Ni heri tukachagua mtu kulingana na utendaji wake. Gharama za kurudia uchaguzi si tatizo kama zitangapangwa na kutumika vizuri.
shirikisho, tanzania bara na serikali ya znz
Tume hii ni ya kuunda
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio ya kuunda katiba ya
Tanganyika kwani kwa sasa Tanganyika haipo, au hata ingekuwepo
wasingeunda rasimu ya katiba ya Tanganyika kwani hawana mamlaka hayo
kisheria. Kama rasimu hii waliyopendekeza itapita kwenye mabaraza ya
katiba na bunge maalum la katiba na suala la shirikisho likabaki kwenye
rasimu, kisha wananchi wakaipitisha kuwa katiba hapo ndipo serikali ya
Tanganyika itakuwa imeanzishwa rasmi. Hivyo mchakato wa kutengeneza
katiba ya Tanganyika utaanza. Kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambao wana katiba yao wanachoweza kufanya ni kufanya marekebisho na
kuona ni kwa namna gani katiba yao itaendana na Katiba ya shirikisho
lililoanzishwa.
Kwanin waseme mawaziri 15 wakati mambo husika ni 7? 1. Sheria, Katiba na Vyama vya Siasa 2. Fedha na Kodi 3. Ulinzi 4. Mambo ya Ndani na Uhamiaji 5. Mambo ya Nje (Tano tu)Serikali ya muungano isiwe na mawaziri wanaozidi 15
mpaka katiba mpya kwanza itambue uwepo wa tanganyika ndipo tanganyika itaandaa katiba yake
Tuko ngoja nikusaidie kidogo, angalia mbali usiangalie karibu hawa Wazanzibar wameshatusumbuwa muda mrefu sana, sasa shortcut ya kuvunja muungano tumeshaipata, CCM haijawahi hata siku moja kuwaza serikali 3 wait n see hii ni zaidi ya movie.Mi bado najiuliza katiba ya Tanzania bara itatengezwa lini. Wananchi wa Tanzania bara watachagua viongozi wao kwa sheria ipi?
Kwanin waseme mawaziri 15 wakati mambo husika ni 7? 1. Sheria, Katiba na Vyama vya Siasa 2. Fedha na Kodi 3. Ulinzi 4. Mambo ya Ndani na Uhamiaji 5. Mambo ya Nje (Tano tu)
Wakuu vipi mawaziri kutokuwa wabunge...rasimu inasemaje kuhusu hili?