RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

gharama sio kitu kama zinatumika kumchagua kiongozi bora bhana kama gharama za kujaza mafuta mashangingi zinatoka kwenye kodi za walalahoi why not uchaguzi.....
 
Kwa nini madaraka ya Raisi yapunguzwe, mimi kama Mtanzania sitaki yapunguzwe na nina haki, hivyo ni sawa tu kwa Upande wangu!

mkuu ni haki yako je huoni kama ndo kikwazo kwa kila kitu. mathalani waziri anateuliwa na rais ,makatibu wakuu wanateuliwa na rais je hapa nani atamwajibisha mwenzie ndo maana matatizo hayaishi kwenye hii nchi then mnasema chadema ndo wabaya kumbe ndo tatizo wa mfumo
 
Kuhusu ma RC na ma DC hilo si swala la muungano litajadiliwa na serikali husika kama kuna ulazima wa kuendelea kuwepo.
walitakiwa wafutwe rasmi hamna cha kujadili wala nini...........
 
Pamoja na mapendekezo mengi kwenye TUME kuwa mazuri, lakini bado kuna mapangufu makubwa, mfano madaraka ya rais bado hayajaainishwa vizuri, RAIS kuteua majaji, kwanini huo Mhimili usiteuwe wenyewe na mambo mengine mengi.

Swali langu je hii rasimu inaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kupigiwa kura ya NDIYO NA HAPANA?
Ndio maana inaitwa rasimu siyo final inapelekwa kwenye mabaraza ya Katiba kujadiliwa, ila ndo hivyo hayo mabaraza 98% ni makanda wa CCM! tegemea vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya kuibuka with flying clours!
 
Hakuna serikali ya Tanzania Bara, tunahitaji ya Tanganyika!
Kweli mkuu, inatakiwa katiba hii ya muungano itamke wazi serikali tatu ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar. Hapa wametegeshea ili wavune tena pesa za kuedit katiba ya muungano kwa kutoa jina Tanzania Bara na kuweka Tanganyika. Mwenye macho haambiwi tazama.
 
Kweli tume imeonyesha umahiri na uzalendo sasa tukubaliane kutokukubaliana liishe tatizo lilikuwa ni Tanganyika kujifanya wakoloni weusi, Warioba ameliona na ametoa suluhusho la kudumu katika hila ila sikubaliani naye kwenye mfumo wa makusanyo ya mapato, linahitaji mchanganuo mpana.
 
Sera za chama zinaweza kuwa mashairi matamu sana yenye watakelezaji wabovu. Ni heri tukachagua mtu kulingana na utendaji wake. Gharama za kurudia uchaguzi si tatizo kama zitangapangwa na kutumika vizuri.

Sio kweli ukiangalia kwa undani zaidi utaona kwamba, kama ikiwa hivyo ina maana wananchi watakikataa Chama kwenye Uchaguzi unaofuata, hivyo ili Chama kiweze kushinda ni lazima kihakikishe kinakuja na Sera nzuri na zinazokubalika na pia kuweka Mgombea ambaye anaweza kuzisimamia, chama ambacho kitaweka Wasanii basi Wananchi watakikataa Uchaguzi Mkuu!

Hivyo ni mfumo mzuri sana tu, hasa huko mbeleni.Hizo gharama za Uchaguzi ni kubwa sana tunaweza kuzifanyia mambo mengine!
 
Tume hii ni ya kuunda
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio ya kuunda katiba ya
Tanganyika kwani kwa sasa Tanganyika haipo, au hata ingekuwepo
wasingeunda rasimu ya katiba ya Tanganyika kwani hawana mamlaka hayo
kisheria. Kama rasimu hii waliyopendekeza itapita kwenye mabaraza ya
katiba na bunge maalum la katiba na suala la shirikisho likabaki kwenye
rasimu, kisha wananchi wakaipitisha kuwa katiba hapo ndipo serikali ya
Tanganyika itakuwa imeanzishwa rasmi. Hivyo mchakato wa kutengeneza
katiba ya Tanganyika utaanza. Kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambao wana katiba yao wanachoweza kufanya ni kufanya marekebisho na
kuona ni kwa namna gani katiba yao itaendana na Katiba ya shirikisho
lililoanzishwa.

umenitoa gizani mzee kumbe bado tuna safari ndefu lakini bora tuwe na katiba ya tanganyika.
 
Binafsi naona kama hii rasimu imejikita zaidi kwenye upande wa siasa zaidi na kuna mambo mengine naona kam ahayakupewa kipaumbele mathalani Mfumo wa Elimu, Afya, Utalii na nyanja nyinginezo zisizohusika moja kwa moja na siasa
 
kwa ufupi jaji warioba chini ya tume yake wametoa maamuzi magumu ambayo wengi hatukuyategemea wanastahili pongezi kubwa hawakujali maslahi ya maccm
 
Serikali ya muungano isiwe na mawaziri wanaozidi 15
Kwanin waseme mawaziri 15 wakati mambo husika ni 7? 1. Sheria, Katiba na Vyama vya Siasa 2. Fedha na Kodi 3. Ulinzi 4. Mambo ya Ndani na Uhamiaji 5. Mambo ya Nje (Tano tu)
 
mpaka katiba mpya kwanza itambue uwepo wa tanganyika ndipo tanganyika itaandaa katiba yake

Mkuu, endapo 2014 hii katiba itakamilika na kutambua uwepo wa Tanganyika, je watanganyika watachagua viongozi wao 2015? Watatumia katiba gani? Hiyo katiba itatengenezwa na nani? Je, itakuwa sawa kufanya uchaguzi wa shirikisho kisha wa Tanganyika baadae?
Mkuu hebu fikiria hapo...
 
Mi bado najiuliza katiba ya Tanzania bara itatengezwa lini. Wananchi wa Tanzania bara watachagua viongozi wao kwa sheria ipi?
Tuko ngoja nikusaidie kidogo, angalia mbali usiangalie karibu hawa Wazanzibar wameshatusumbuwa muda mrefu sana, sasa shortcut ya kuvunja muungano tumeshaipata, CCM haijawahi hata siku moja kuwaza serikali 3 wait n see hii ni zaidi ya movie.
 
Last edited by a moderator:
Kwanin waseme mawaziri 15 wakati mambo husika ni 7? 1. Sheria, Katiba na Vyama vya Siasa 2. Fedha na Kodi 3. Ulinzi 4. Mambo ya Ndani na Uhamiaji 5. Mambo ya Nje (Tano tu)

Mi nikisema hii katiba ni another useless paper, watu wananidhihaki...
 
Wakuu vipi mawaziri kutokuwa wabunge...rasimu inasemaje kuhusu hili?

Wamefanya kazi nzuri ila hapo kwa red ndo wamechemsha, yaani tutaendelea kuwa na mawaziri wanasiasa wanaoteuliwa kwa kujuana! daah, wanasiasa hawataki kuachia hizi nafasi löh!
 
Back
Top Bottom