RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Serekali tatu maana yake kifo cha muungano.


[1] Serekali ya Tanganyika itakuwa na nguvu kuliko serekali ya shirikisho.

[2] Serekali ya Zanzibar haina uwezo wa kuchangia gharama za serekali ya shirikisho.

[3] Serekali ya Tanganyika itachangia uendeshaji wa serekali ya shirikisho lakini pia itapendakuona serekali ya Zanzibar inachangia nini ?.

[4] Namwona Yetzin akiibukia ndani ya serekali ya Tanganyika na kuuvunjilia mbali shikisho la kinyonyaji.

(a) Zanzibar lazima walipe gharama za ulinzi na usalama sio kufurahia saluti za wanajeshi.

(b) Zanzibar lazima ichangie gharama za wabunge wake wanaiwakisha katika bunge la muungano.

(c) Rais wa Zanzibar akija Tanganyika atahesabika kama mkuu wa mkoa wa Pwani.

(d) Wazanzibar waliojazana Tanganyika watahesabiwa kama wageni ikiwa suala la uraia kila nchi itaamua itakavyo.Tayari Zanzibar wana uraia wa Tanzania na uraia wa Zanzibar,Tanganyika itabidi ianzishe uraia wa Tanganyika ha ha ha tukutane na Zanzibar EAC.

(E) Gharama na marupurupu ya viongozi wa Zanzibar kuanzia Rais na makamu wake wawili zitabebwa na wazanzibar wenyewe.Zanzibar italazimika kulipa bill za umeme kadri inavyotumia kususua TANESCO pia kumechangiwa na Zanzibar kutolipa bill.



(e)
 
Me sijaelewa kidogo!kwahiyo kutakuwa na rais wa tanganyika,rais wa zanzbar na rais wa tanzania?au inakuwaje?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Iwapo kipengele cha serikali tatu kitapitishwa pamoja na vile vyote vinavyohusiana na hicho, maana yake tutatengeneza majogoo matatu, mawili yakiwa na nguvu zaidi ya jogoo moja. Na usalama pekee wa hili jogoo moja ni pale yale majogoo mawili yakitawala kwa maelewano, kinyume chake jogoo kuu litakuwa halina nguvu huku likiendelea kutafuna kodi za wana nchi.

Suruhisho ambalo halina msuguano ni serikali moja. Imani yangu kule kwenye mabaraza tunaweza kupata maoni au mapendekezo mazuri zaidi.

Sipati picha ikitokea Rais bara (chadema), Rais zanzibar (Cuf), Rais Muungano (ccm)

Wataalamu tusaidie hali ikitokea itakuwaje?
 
Muda utatosha warioba alishasema 2015 katiba mpya lazima.alimaanisha ya shirikisho na ya tanganyika sana tume.Faster chikawe apeleke muswaada
 
Waaaaii sioni hata nilichopendekezaga mimi lakin naunga mkono hoja!!...acha nisepe nitarudi midamida..kuangalia waliopinga,maana hawakosekani hata kama jambo ni zuri,ving'ang'a wapo tuu huwaga!!
 
Me sijaelewa kidogo!kwahiyo kutakuwa na rais wa tanganyika,rais wa zanzbar na rais wa tanzania?au inakuwaje?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Nashauri huku Tanganyika tuachane na urais, tuwe na waziri mkuu na atokane na uwiano wa kura/viti vya ubunge.
 
Mkuu kwani katiba ni ya tanzania au tanganyika?

ni katiba ya JMT mkuu ila ndani yake itaundwa Taifa letu la Tanganyika iliyouawa mwaka 1964 sasa mimi swali langu tutakuwa watanganyika au watanzania? tutatambuliwa kwa utaifa upi??
 
  • IDADI YA MAWAZIRI

Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.

Hapa tu mimi pamenikuna!
 
Wadau, sijui kama tumeliona hili. Rasimu ya leo ni ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. kazi iliyo mbele yetu bila shaka ni ya kuandaa Katiba ya Tanzania Bara (Tanganyika). Je, muda huu unatosha kabla ya mwaka 2015?
Muda utatosha,maana si kazi kubwa kufuta maoni yaliyokuwa yanaihusu Zenji na kurudisha jina Tanganyika badala ya Tanzan-ia
 
Sijaona kitu change kunifariji ktk swala zima ya katiba mpya kwani wenye hisia zetu kamili hawapewi uhuru wa kutusemea. Wawape wapinzani kutoa mawazo yao kikamilifu, hao ndo wanaendelea kuwakilisha hisia zetu.
 
You have a point, although don't forget kuwa kuna wagombea huru ambao binafsi nadhani ndiyo watakuja kuwa tishio zaidi kwa chama tawala.
 
Jina Tanganyika hawajaltaja, wanasema serikal tatu yaani Zanzibar, shirikisho na Tanzania bara. Viti maalum wanapigwa ban, wabunge bara ni 60! Na zenj ni 25! Wakuteuliwa na rais 5! Kwel?
 
1."Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi."
2."Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa. "

Haya mambo mawili yanatakiwa kupitiwa upya!! tume sio huru na kumuachia rais kinga ni kumfanya asiwajibike!!
 
sijaona kipya hapa bado rais anapewa madaraka makubwa ya kuingilia mahakama,kweli hawa watu wanatumbua kodi zetu bure.
 
nimependa mawaziri wasiwe wabunge na spika
wa bunge asiwe mbunge
 
Ni nzuri na imefanya vizuri kutoweka mambo ya serikali za majimbo ambayo yangeweza kutugawa
 
Tume imejitahidi Rasmu ya Katiba kwa kiasi kikubwa imekaa vizuri, kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini mwetu, kupata rasmu kama hii si mchezo. Wamejitahidi.
 
Back
Top Bottom