Rasimu hii haijakidhi matakwa ya Watanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa mchakato wa kukusanya na kuaandaa rasimu ulibakwa na walio madarakani. Zaidi ya mwaka mzima wanafanya kazi na kulipwa mamilioni ya shillingi harafu wanakuja na rasimu ambayo imewacha watanzania wakijiuliza lipi jipya hapa?
Japo kenya wamepata katiba mpya kwa kumwaga damu, katiba yao ilikidhi matakwa na mahitaji ya kenya kwa miaka 50 ijayo. Tanzania aibu tupu... katiba hii mpya haiwezi kutosegeza hata miaka 2 mbele. Inakuwaje rais apewe nafasi 5 za kuteua wabunge? Haki hii ni ya watanzania kuchagua na lengo ni kuondokana na vyeo hivi vya kuteuliwa. Mambo ya uraia katika nchi nyingi duniani yameandikwa ndani ya katiba kwa kuwa ndiyo sheria mama. Warioba vipi tena? Anasema eti itungwe sheria ya uraia? Hopeless guy and his team. Hatuna katiba mpya maana haiwezi kupita kwenye kura ya maoni, wameacha mianya mingi wakati watanzania walitoa maoni yao. Vipi kuhusu, TAKUKURU, CAG, AG, DPP, raslimali zetu, mambo haya yanatakiwa ya ainishwe kwenye katiba. Katiba isipo yatamka nani atayasimamia?
I'm very dissappointed in Warioba and his team. Wametuaibisha watanzania, kumbe nao wanafikiri kwa tumbo.